Nataka niifukie 9,200,000

Kama unavyoshauriwa bora kununua mazao mimi nalima naona changamoto sana bora robo ya hela lima uone utakachopata ili mwaka unaofatia ujue changamoto ulizoziona utakabiliana nazo na kiwango kikubwa cha hela bora uwekeze katika kununua zaidi na kuuza mazao yasiyo haribika yakikaa muda mrefu
 
Asante
 
Nataka niingize kiasi tajwa kwenye kilimo Cha mazao ya muda mfupi,siku 90-180 mavuno,lengo ni kupata 30,000,000 ili nifanye mambo fulani,Ni zao lipi linaweza kunifikisha kwenye kwenye lengo?
Wazoefu kujeni nahitaji mawazo yenu.
Usilime braza... Km una uhakika wa masoko we nunua tu mazao

Vinginevyo labda km una vyanzo vya mapato vingine tofauti na iyo unayoitaka kuizika
 
Usilime braza... Km una uhakika wa masoko we nunua tu mazao

Vinginevyo labda km una vyanzo vya mapato vingine tofauti na iyo unayoitaka kuizika
Yah ninayo shughuli nyingine,hiyo 9.2M imetokana na hiyo shughuli,nilikuwa na akaunti ya malengo miaka kadhaa hatimaye kimepatikana hicho kiasi nataka nivunje kibubu,lengo nipate 30M ndani ya miezi 3-6 .
 
Ukiweza tafta eneo lililo karibu na Maji mwagilia kwa generator Au scheme ya umwagiliaji Lima mpunga fuata utaalam Lima hata 10 acre nakuhakikishia kola acre una uhakika wa kupata Gunia kuanzia 30 za mpunga
 
Asante sana
 
Eka

Eka 1 upate gunia 30 za mpunga? Wapi hii Mkuu?
 
Eka
Eka 1 upate gunia 30 za mpunga? Wapi hii Mkuu?
Popote pale utakapolima kwa kuzingatia sheria na kanuni za Kilimo
Kwenye mpunga utavuna mavuno mengi.
Fanya hivi
Kuwa na uhakika wa Maji au(kilimo cha Umwagiliaji) tumia mbegu bora improved variety, pannda kwa nafasi inayotakiwa, ,tumia Mbolea , zibiti magugu nakuhakikishia hutajuta
 
Endelea na kazi ikiyokufanya upate hio 9,200,000 mwenzio mimi 6,000,000 niliingia shamba hata kumi haijarudi na kazi iliyonifanya nipate 6,000,000 nayo ishakufa kwakuwa fungu halipo Na haha kukopa taasisi za fedha HIVYO YAPIME JIANDAE NAYO YAJAYO
 
Jamaa pima mwenyewe lipi ambalo utalimudu kwa asilimia kuanzia 80%.

Shughuri za kilimo zinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana. Kuna mambo ya mbolea, madawa, kupalilia na kuvuna. Yoote hayo yanahitaji taimingi. Ukikosea/kuchelewa kidogo tu ndo tayari inaweza pelekea hasara furani.

Km umeshawahi kulima hapo awali na kufanikiwa basi unaweza kuanzia hapo.

Kuwekeza kwenye Kilimo ni poa sana but zingatia hayo hapo juu.

Wadau wamekushauri juu ya uchuuzi.
Nami pia naonelea uanzie hapo. Tafuta fremu chagua bidhaa yako unayoona inahitajika ama utaweza kuiuza vizuri kinyume na majira/rivals wako.

Tafuta hiyo bidhaa mahali inapopatikana kwa wingi na kwa ubora. Pia half of your servings ndiyo uielekeze huko kwenye trading. Itakayobakia unaextend kwa biashara nyingine ya tofauti.

Hakikisha unajua legal procedure zote za kuformalize biashara unayoiwazia kabla hujaanza hatua moja. Hii itakusaidi kutogo bana na wasimamizi wa kanuni na taratibu za biashara ambapo pia inaweza kugharimu uhai wa biashara yako.

Kwa mawazo yangu yenye makengeza naomba kuwasilisha.[emoji120][emoji120][emoji120]
 
[emoji2958]
 
Endelea na kazi ikiyokufanya upate hio 9,200,000 mwenzio mimi 6,000,000 niliingia shamba hata kumi haijarudi na kazi iliyonifanya nipate 6,000,000 nayo ishakufa kwakuwa fungu halipo Na haha kukopa taasisi za fedha HIVYO YAPIME JIANDAE NAYO YAJAYO
Daaaa mtihani
 
Nataka niingize kiasi tajwa kwenye kilimo Cha mazao ya muda mfupi,siku 90-180 mavuno,lengo ni kupata 30,000,000 ili nifanye mambo fulani,Ni zao lipi linaweza kunifikisha kwenye kwenye lengo?
Wazoefu kujeni nahitaji mawazo yenu.
Viazi mviringo njombe, ila mwisho wa kupanda ni jun
 
Yah ninayo shughuli nyingine,hiyo 9.2M imetokana na hiyo shughuli,nilikuwa na akaunti ya malengo miaka kadhaa hatimaye kimepatikana hicho kiasi nataka nivunje kibubu,lengo nipate 30M ndani ya miezi 3-6 .
Njo ulime njombe parachichi miaka 3 unaanza kuvuna.Hapo utapanda heka nane.parachichi ndio habari ya nyanda za juu, kilo moja buku jero, achana na mazao ya msimu yatakuumiza kichwa.
 
Tuanzie hapa kwanza, Je umekubali kuchakaa mwili na akili?

Biashara ya Mazao inataka Undundame haswa lasivyo utakuja kulia lia lia iwe kama ndoto.

Kiufupi ukitaka kuruka lazima ubonyee chini, sasa hapo kwenye kubonyea ndio mtihani.
 
Njo ulime njombe parachichi miaka 3 unaanza kuvuna.Hapo utapanda heka nane.parachichi ndio habari ya nyanda za juu, kilo moja buku jero, achana na mazao ya msimu yatakuumiza kichwa.
Gharama zake zikoje kwa heka?kuanzia kununua shamba Miche kulima kupanda nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…