Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
Wakuu tumeshuhudia watu wakipigana vikumbo kugombea nafasi kadhaa ndani ya CCM na wengine kuhonga vitumbua ili tu wapate kuchaguliwa wajumbe wa mkutano mkuu au NEC mimi nataka nijue kuwa mjumbe wa NEC CCM kuna faida/maslahi gani mpaka ifike hatua watu wanatishana na bastola? Je kuna marupu rupu na posho ma/kubwa kwenye uwakilishi wa ujumbe wa NEC? Ni nini haswa faida kuwa mjumbe wa NEC mpaka mtu anadiriki kutumia mamilioni ya shillingi ili awe tu mjumbe je anapata faida gani? Akina zomba, Ritz, Rejao, Kibunango na wengineo naombeni nifahamu faida zake.