Nataka nijue kusoma Quaran


Khawaarij hawa, kuanzia baba yao usama bin laden na watoto wake ndio hao akina rogo
 
Makazi yangu mara nyingi nipo Moshi, Mbeya mjini na Iringa mkuu...nipe ushauri
Kwa Mbeya nenda Msikiti Mkuu pale upo umbali mfupi kutoka Stendi kuu ya Mabus Mbeya kuna ustaadhi pale na vijana wanaishi pale pale ndani ya eneo la msikiti watakusaidia sana.
 

ikiwa una nia ya dhati kuujua uislam basi nikupe hongera sana kwa msimamo na maamudhi uliofikia, hilo sio kosa hata waislam wametakiwa kuamini na kusoma vitabu vinne (1-Tawrat - Moses book, 2-Zabour- David, 3-Injil - Issa/Yesu, 4-Quran-Muhammad S.A.W) ikiwa ni katika nguzo ya Imani.
Ushauri wangu tafuta Sheikh ambae amekua akisomesha ndani ya msikiti tafsir ya Quran na ukiwapata wale wazee watakusaidia zaidi. Quran imekuja kwa lugha ya kiarab lakini haina maana kujua lugha ya kiarab ndio kuijua kuisoma Quran
Jaribu kufuatilia mawaidha hasa yanayohusu historia ya dini hizi ili ujiongezee maarifa zaidi mfano huyu Sheikh Othman Maalim:
 
Ukiwa seriously Sana ni miez mitatu usipokuwa serious miez sita na ukiwa mvivu mwaka
 

Kama ni mwepesi sana inaweza kukuchukua 3 weeks ukawa tayar umeshaanza kusoma,
Na kuanzia mwaka mmoja ukawa umei memorize yote,kiasi kwamba hata mtu anahubiri au anafundisha akikosea tu,tayar ushajua hapa kakosea.
TANBIHI,jitahidi upate sehem sahihi na mwalimu sahihi
 
Allah Akbar kijana mwenzangu nakukaribisha katika dini ya manabii(mitume)Mwenyezi mungu akufanyie wepesi
 
Hebu rudia kuandika tena.
 
Nenda ubalozi wa Saudia kawaambie shida yako au Ubalozi wa Sudani ni rahisi sana kupata short course ya mwaka 1 au kama mhitimu wa degree nenda kauluzie utaratibu wa scholarship za post graduate zikoje utaambiwa
 
Nenda madrasa au mskiti wowote wa karibu yako utapata private tutor.

Mtandao pia una site nyingi sana za kufundisha Qur'an lakini ni vyema ukapata basics face to face.

Ni wepesi sana kusoma Qur'an na Kiarabu. Hususan kwa anaefahamu Kiswahili.
Nilitaka nishangae mada kama hii ikupite
 
Bila kubamizwa makofi na ustadh utachukua miaka mingi Sana ,mtume mwenyewe alikabwa na jibril
 
Mkuu nimekuelewa sana. Mimi binafsi siyo muumini wa dini yoyote baada ya kukulia katika ukristu nkuufuata tangu nikiwa mdogo. Na nilibahatika kusoma katika shule za seminari nimesoma biblia na nilipata A katika mtihani wa Taifa. Nimesoma Seminarini miaka sita lakini nimeamua kubaki kama mtu ninayeamini Mungu yupo ila sina imani na dini yeyote na wanangu wanalijua hilo ila sina wasiwasi na mtu kuamini anachokitaka na nimeweka wazi kwa wanangu wafuate wanachokitaka. Mmoja kaamua kuwa muislam wengine wakristu.

Ila hua napenda sana kuongea na watu kama wewe ambao wanasema ukweli kwa maana kufundisha watu bila kukashifu ama kujifanya kama wao ndiyo kamili kuliko wengine. Kama Watu wote wa dini wangekua kama wewe sisi wengine tungebaki waumini wazuri lakini ukiona mtu anakshifu mwenzie bila kutoa sababu za kumvutia mtu ahamie kwake hapo ndipo ninakwazika.

Kwanini naita dini ni utapeli sina maana ya kukashifu wanaofuata bali viongozi wengi ni wababaishaji. Hainijii akilini kwanini mkristu wa Roma ajifanye ni bora zaidi ya mkristu m pentecostal vivyo hivyo m pentecostal amuone Mroma si bora. Ukiingia Uislam vilevile Suni anajiona ni bora zaidi ya Shia mpaka kupigana vita na kuuana. Nini unakipata kwa kumuua m Shia sababu wewe ni Suni na vice versa. Ni biaahara pekee watu hugombana. Mwanza waumini walimpiga Askofu Maeneo tofauti misikitini watu wanagombana. Dini si ndiyo ilitakiwa kufanya watu waishi kwa kupendanna sasa ugomvi unalwtwa na nini?
 
Yes mkuu ndyo mana na mimi namsisitizia mtoa mada atafute sehemu salama akasomee na sio kwa kila shekhe tu.

Dini (uislamu)una maandiko mengi ya vita vita,hilo jambo linafanya mtu atakae kupotoa apotoe kwa namna aitakavyo lakini makusudio sio hayo.wale wanaojiripua wale ukweli ni kuwa wanatumia Quran hii hii tunayotumia sisi na aya wanatoa humo humo lakini jeee aya zimekusudiwa kama ambavyo wao wanzitumia? Utakuja kuona ni ufahamu wao mfinyu na jazba walizosoma kwa watu wajinga wajinga wanaojiita waislamu.

Hivyo mkuu naungana na wewe na hata hii dini ninayoiabudu(islam)haiko vile watu wanaifikiria,mfano tuuu ikatokea tanzania ni nchi ya kiislamu basi uislamu umekataza kubomoa makanisa na utawaacha watu waendelee kuabudu humo na ni wajibu kwa dola ya kiislamu kuwapa ulinzi watu hao ambao wanaishi kwa amani na waislamu.

Hizi dini tukiziendea vibaya na kwa pupa ndo tunawatoa watu kama kina OSAMA BIN LADEN na wahuni wengineo ambao wanajivika uisilamu na wattu wanawatizama wao.

Binafsi niliamua kusoma dini na kuichambua kwa Qadri ya akili yangu huku nikiwa sitoki nje ya misingi hyo,na sasa hivi nafurahia maisha na dini yangu kinyume na waislamu wengi leo wanaojipa tabu kutaka kwenda somaliaa,kujiripuaa,kujitoa muhanga,kufanya maandamano n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…