Nataka nimsaidie kisiri rafiki mlinzi shilingi milioni 1.2 kwa mategemeo ataacha ulinzi anaolalamka unamtesa ili afanye biashara. Je, nitarajie hilo?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
nimejenga mazoea na mlinzi anaelnda sehemu jirani, mara kadhaa mida ya jioni huwa tunajuliana hali

Katika stories kuna siku aliwah kuniambia kazi inamtesa sana, Usiku ni lazima aingie kazini saa 12 jioni mpaka kesho yake alfajiri saa 12

Analalamika kampuni inapewa laki 6 yeye anaachiwa laki 1 na elf kadhaa

Mchana anafanya biashara nyingine ndogondogo na vibarua

Ninataka kumsaidia ila kwa siri, ndivyo nilivyo, huwa napenda mtu awe free nikimsaidia bila kuhisi deni lolote juu yangu, mahusiiano ya kirafiki yaendelee kwa uhuru

Nimpeata wazo nimsaidie, Kiasi kilichopo ni shilingi milioni 1.2, mategemeo ni yeye ataacha kazi hiyo,

Je nitegemee kwamba ataacha kazi na kujikita zaidi kwenye biashara ?

Nina hofu asije kuiona kama zawadi ya kujipongeza badala ya kufanyia maendeleo

Machache yaliyonipa msukumo wa kumsaidia
  • Hachezi kamari,hanywi Pombe wala havuti bangi
  • Mara kadhaa namkuta anasoma kitabu cha dini yake
  • Kaoa
  • mara kadhaa nimekutana nae mchana akiwa kwenye mihangaiko ya biashara
 
Wewe una akili za kimakonda Makonda.
 
Ana uwezo wa kufanya biashara gani? Pesa siyo tatizo, tatizo ni business idea
 
Ingia jukwaa la ajira kawape hiyo pesa Yako kama umekosa Cha kuifanyia Kuna watu wanasota hata mia 500 hawana unampa pesa mtu mwenye ajira kwani mpaka analipwa hiyo laki 1 yeye haoni au anafanya kazi kama nguruwe anavyokula vitoto vyake tu bila maslai
 
Kutoa ni vizuri ila maadam umekuja hapa kuuliza
Naona hiyo biashara anayofanya aidha ungemuongezea bidhaa badala ya cash au kama amepanga mlipie mwaka mzima kodi na iliyobaki ataongeza bidhaa mwenyewe
Hata ukifanya ziada kidogo sio mbaya

Ila cash huwa matatizo yanakuwa mengi sana kwa binadamu anaweza kujipa holiday au ampeleke mama hospital kubwa
 
Usimpe yote kwa mkupuo mdadisi kdogo kwamba anaona akipata sh.ngapi atapanua biashara anayofanya sasa na kuacha huo ulinzi,naamini haiwezi fika hyo unayotaka kumpa, ukimpa ukiona anaendelea fresh unamuongeza kdogo, umeshajua anafanya biashara ndogo ndogo, kumpa hyo 1.2 lazima itapotea, mpe kwa mafungu huku akikua taratib, kila laheri kwenye kumkopesha Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…