Nataka nimuingize mjini

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
16,717
Reaction score
13,176
Habari zenu waheshimiwa,JPili inasemaje?kwangu ni mbona tu na nina mpango wa kwenda kupunga upepo pale beach.
Ni hivi nina ndugu yangu kaingia kutoka Mafia yaani bado mshamba kwelikweli sasa nilikuwa nina mpango wa kuanza kumchangamsha.
Kuna jamaa alinipa ushauri nimpige picha akiwa na pensi kashika chupa ya koka kola kubwa huku kaweka pozi ya dole tupu,nimpige picha mbili moja yangu moja yake kama kumbukumbu,kwahiyo akianza kujanjaruka niwe wala siuumii kichwa kwani naweza nikamuumbua kwa kutumia picha hiyo.
Binafsi nilikuwa nina mpango wa kumkabisha kwa mateja wamkatekate visu ila wasimuue halafu nimpeleke hospital akatibiwe akitoka ataanza kulijua jiji kidogokidogo.
Narudi kwenu marafiki zangu ambao ndio nyie,je plan hizo ni nzuri kuzitekeleza? au kuna njia nyingine mbadala za kumuingiza mtu mjini?
 
picha ya koka kola ndo yenyewe

halafu akae akinyooshea kidole tv......
 
Kwani kuna haja gani ya yote hayo??? Wewe mjini uliingiaje??
 
Picha ya koka na noti mpya mkononi Inatosha kumuwashawasha siyo Topaz za wahuni wa mjini
 

Utu hauna cha kujanjaruka mkuu, akija gundua ulimfanyia hivi makusudi utakuwa umeweka alama mbaya sana ktk kumbukumbu yake. Ipo siku naye anaweza kuja kumfanyia hivyo mtoto wako au mkeo au utakuwa umemfundisha nae aige hiyo tabia akiona maisha ya mjini magumu kama unavyoona sasa.

Kumtoa ushamba ni kama kumsomesha mtoto shule ya msingi, anaanza la kwanza taratibu mpaka la saba hapo ndio atapata elimu nzuri itakayo msaidia. Usimvushe madarasa, bali kuwa mvumilivu kadri anavyoendelea kujifunza taratibu
 

hufai kuwamo kwenye jamvi hili coz una mawazo mgando.
 

Hamna noma sitomvukisha darasa atasoma taratibu mpaka aelewe
 
mchawi sio lazima awe na tunguli.
 
una matatizo zaidi ya unavyofikiria :A S 112:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…