Habari zenu waheshimiwa,JPili inasemaje?kwangu ni mbona tu na nina mpango wa kwenda kupunga upepo pale beach.
Ni hivi nina ndugu yangu kaingia kutoka Mafia yaani bado mshamba kwelikweli sasa nilikuwa nina mpango wa kuanza kumchangamsha.
Kuna jamaa alinipa ushauri nimpige picha akiwa na pensi kashika chupa ya koka kola kubwa huku kaweka pozi ya dole tupu,nimpige picha mbili moja yangu moja yake kama kumbukumbu,kwahiyo akianza kujanjaruka niwe wala siuumii kichwa kwani naweza nikamuumbua kwa kutumia picha hiyo.
Binafsi nilikuwa nina mpango wa kumkabisha kwa mateja wamkatekate visu ila wasimuue halafu nimpeleke hospital akatibiwe akitoka ataanza kulijua jiji kidogokidogo.
Narudi kwenu marafiki zangu ambao ndio nyie,je plan hizo ni nzuri kuzitekeleza? au kuna njia nyingine mbadala za kumuingiza mtu mjini?