Nataka nimuwahi my wife wangu

Nataka nimuwahi my wife wangu

kuna siku nilimtembelea ragfiki yangu nyumbani kwake.
Jamaa akaniagizia Serengeti mbili na yeye akajiagizia soda, house girl akatumwa kununua.
Muda si muda akaingia mama mwenye nyumba, na haukupita muda si mrefu hausigeli akawa analeta bia mezani.
Yule mama akaanza kufoka kuwa nyumba yake haiwezi kugeuzwa baa, akamkunja shati mume wake na kumwambia "hebu mtoe huyo kinyangarika mwenzako" niliondoka kimya kimya na sitaki tena kumtembelea mtu yoyote nyumbani kwake. Kama ni vikao, tutafanyia bar kama kawa.

mwanamke mjinga huivunja nyumba yake kwa moikono yake mwenyewe.
Jamani eti huyu naye ni mke bora au bora mke?
 
Wanawake wana nguvu sana hnimeshuhudia boss wangu akipigwa makofi na nyumba ndogo yake ofisini asubuhi,vibao 2 na anamwili ka nyumba na nyumba ndogo ni kimodo ila mtu mzima kwa!kwa! Na akatulia. Wanawake wana nguvu sana,na ndio wanaongoza dunia. Hata mkuu wa majeshi na manyota yake yote akifika chumbani kwa mkewe manyota mkanda silaha vyooote anatupa chini.....
 
kama makubalinao ni kutoleta bia ndani ya nyumba yeye aliletaya nini? ni rahisi sana, kwangu mimi mr. hanywi pombe na hakuna pombe inakanyaga nyumbani kwetu. sasa imagine mume wangu arudi akute na mashost nimewanunulia bia si varangati kaka.

Jifunze kuheshimu maadili ya nyumbani mwenu hasa yale mliyojiwekea. Suala la kufanya hivyo mbele yako huyo mama alikiuka maadili, nahisi ana ukichaa kama siyo kinamuanza, hakufunzwa na wazaziwe atafunzwa na ulimwengu.
 
hata kama, je kuna faida gani ya kuibua ugomvi mbele ya mgeni?
Je nini athari zake kwa siku za usoni?
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Back
Top Bottom