Nataka ninunue bidhaa online lakini sina kitambulisho chochote, inawezekana?

Nataka ninunue bidhaa online lakini sina kitambulisho chochote, inawezekana?

24 Hours

Member
Joined
Feb 18, 2022
Posts
41
Reaction score
76
Habari,

Nataka kuagiza bidhaa online kwenye site kubwa kama amazon, ebay, aliexpress n.k lakini sina kitambulisho chochote kile, ila nina namba ya simu tu ambayo ni ya mtu.

Sitaki yeyote aniagizie wala sitaki kutumia sanduku la posta la mtu mwingine. nachotaka nikiagiza bidhaa inifikie pasipo kupitia posta wala kuulizwa kitambulisho, inifikie kupitia namba ya simu. mtaa ninaokaa ni uswahilini, hapajakaa kimtaa na kimpango mji, nikimuelekeza mtu kiramani hawezi kuelewa.

Sasa nipeni elimu wakuu kama inawezekana
 
nachotaka nikiagiza bidhaa inifikie pasipo kupitia posta wala kuulizwa kitambulisho
  • Haitowezekana.
  • Sababu, kwa maelezo uliyoyatoa njia ya usafirishaji itakayotumika ni 'express' kwa bidhaa zako zote.
  • Ambapo kwenye ku_clear mzigo ni lazima kuna hatua itahitajika
#1. TIN namba ya jina iliyotumika kwenye usafirishaji wa mzigo wako
#2. Utahitajika uambatanishe moja ya kitambulisho kati ya Driving licence au kitambulisho cha taifa ili kuthibitisha taarifa #1.
sina kitambulisho chochote kile., ila nina namba ya simu tu ambayo ni ya mtu
Kwa maisha ya sasa hakikisha umiliki.
  • Kitambulisho kimojawapo. [ Driving Licence / National ID / Passport ] Ni muhimu sana.
  • Uwe na bank account, sababu kuna baadhi ya huduma mtandaoni hutumia bank statement kama kigezo cha address verification ili upate huduma.
bidhaa online kwenye site kubwa kama amazon, ebay, aliexpress n.k
Kwa sasa hauna vigezo/kigezo cha kuagiza bidhaa online. Hakuna jinsi kariakoo itahusika zaidi kuagiza bidhaa zako na hutopata usumbufu wowote.
 
nina namba ya simu tu ambayo ni ya mtu

sitaki yeyote aniagizie
wala sitaki kutumia sanduku la posta la mtu mwingine. nachotaka nikiagiza bidhaa inifikie pasipo kupitia posta wala kuulizwa kitambulisho
Duu ni kwanini umefikia maamuzi haya, yasiyo endana na uhalisia.

- Je wajua kuwa ni kosa kisheria kumiliki na kutumia namba ya simu ya mtu mwingine? Una kesi ya kujibu hapa.

Mfano hai:
- Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii utakumbuka moja ya kosa aliloshitakiwa Idrisa wakati ule, ukiacha lile kosa la msingi la 'kutabasamu/kucheka' ilikuwa ni umiliki na kutumia namba ya simu ya mtu mwingine.
 
itahitajika
#1. TIN namba ya jina iliyotumika kwenye usafirishaji wa mzigo
maelezo yote nimekupata, ila hapo ☝☝☝.

ina maana kama una kitambulisho na sanduku la posta, inabidi LAZIMA uwe na TIN number kwa ajili ya usafirishaji mizigo?
 
TIN number
  • Huwezi kupata huduma ya Sanduku la posta bila ya kuwa na TIN number.
  • TIN number Ndio kigezo cha kwanza.
ina maana kama una kitambulisho na sanduku la posta
Kwa taarifa yako hakikisha unamiliki mapema iwezekanavyo vifuatavyo
  • Namba ya NIDA [ /kitambulisho kabisa ]
  • TIN number
Ndipo sasa fikiria maswala mengine.
 
Duu ni kwanini umefikia maamuzi haya, yasiyo endana na uhalisia.

- Je wajua kuwa ni kosa kisheria kumiliki na kutumia namba ya simu ya mtu mwingine? Una kesi ya kujibu hapa.

Mfano hai:
- Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii utakumbuka moja ya kosa aliloshitakiwa Idrisa wakati ule, ukiacha lile kosa la msingi la 'kutabasamu/kucheka' ilikuwa ni umiliki na kutumia namba ya simu ya mtu mwingine
nimeuliza kwa niaba ya mtu, hapa ninapokaa nimeulizwa hilo swali nikakosa jibu, nikaja kuuliza huku ili nipate jibu la uhakika.
 
Huwezi kupata huduma yoyote zaidi ya kuzikwa na manispaa siku ukifariki.
Dah!

Tunapoelekea, vitambulisho, hasa cha taifa kitakuwa ndiyo kila kitu, itakuwa huwezi kupata huduma yoyote ya kiserikali bila ya kitambulisho
 
  • Huwezi kupata huduma ya Sanduku la posta bila ya kuwa na TIN number.
  • TIN number Ndio kigezo cha kwanza.

Kwa taarifa yako hakikisha unamiliki mapema iwezekanavyo vifuatavyo
  • Namba ya NIDA [ /kitambulisho kabisa ]
  • TIN number
Ndipo sasa fikiria maswala mengine.
shukrani mkuu, hapo sina swali tena
 
  • Haitowezekana.
  • Sababu, kwa maelezo uliyoyatoa njia ya usafirishaji itakayotumika ni 'express' kwa bidhaa zako zote.
  • Ambapo kwenye ku_clear mzigo ni lazima kuna hatua itahitajika
#1. TIN namba ya jina iliyotumika kwenye usafirishaji wa mzigo wako
#2. Utahitajika uambatanishe moja ya kitambulisho kati ya Driving licence au kitambulisho cha taifa ili kuthibitisha taarifa #1.

Kwa maisha ya sasa hakikisha umiliki.
  • Kitambulisho kimojawapo. [ Driving Licence / National ID / Passport ] Ni muhimu sana.
  • Uwe na bank account, sababu kuna baadhi ya huduma mtandaoni hutumia bank statement kama kigezo cha address verification ili upate huduma.

Kwa sasa hauna vigezo/kigezo cha kuagiza bidhaa online. Hakuna jinsi kariakoo itahusika zaidi kuagiza bidhaa zako na hutopata usumbufu wowote.
Habari Yako , me nahitaji mawakala wanaoagiza vitu moja kwa moja china niwatumie Ila nna namba ya nida na TIN number naombeni msaada mniunganishe nao tafadhali
 
Sio tunako elekea.

Ipo hivyo kwa sasa, Kitambulisho cha Taifa ni muhimu sana.
aliexpress wanavyoweka bei zao zinachanganya. hata sijaelewa bei ya picha a na b
AliExpress A.jpg
AliExpress B.jpg
 
  • Huwezi kupata huduma ya Sanduku la posta bila ya kuwa na TIN number.
  • TIN number Ndio kigezo cha kwanza.

Kwa taarifa yako hakikisha unamiliki mapema iwezekanavyo vifuatavyo
  • Namba ya NIDA [ /kitambulisho kabisa ]
  • TIN number
Ndipo sasa fikiria maswala mengine.
Kufungua box sio lazima uwe na TIN unless uwe unafungua kwa ajili ya kampuni. Kama ni mtu binafsi si lazima.
 
Mwaka 2008 wakati bitcoin inaanzishwa, ilijitokeza fursa ya kujipatia sarafu kwa kuchimba (mining) kupitia computer bure. Wachache waliamini wakachimba ila wengi walipuuzia kwa kuwa hazikuwa na thamani ya pesa (monetary value) kwa wakati huo. Wale waliochimba wamenufaika kwa kuuza sarafu walizochimba.

Miaka 14 baadaye imejitokeza tena fursa ya kujipatia coin za RENEC kwa kufanya mining.

1. Kujisajili na kuchimba ni bure.
2. Hakuna ulazima wa kumuunga mwenzako.
3. Coin ikizinduliwa waweza kutoa pesa kwa njia ya simu au benki.

Kama upo willing, nicheki DM kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga njoo DM ni buure bila hata 50

Pia waweza kutembelea ukurasa wa instagram Heisslyman Msaba
 
Back
Top Bottom