"Nataka niwe Fisadi!!!"

"Nataka niwe Fisadi!!!"

Choveki

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2006
Posts
458
Reaction score
171
Matamanio yangu (kuwa fisadi)

Natamani, natamani, na mimi niwe fisadi
Natamani, natamani, na mimi niwe zaidi
Natamani, natamani, na mimi niwe kaidi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wandugu!

Kwa kuwaliza wabongo, nataka niwe fisadi
Nije wapiga madongo, yaliyo ya kigaidi!
Hata mkila udongo, majani au zaidi!
Fisadi au kaidi, nitawaliza wabongo!

Mwenzenu natamania, ninaongeza juhudi
Nitauza Tanzania, halafu niwe hasidi!
Dharau ya kuringia , tafanya kwa makusudi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wabongo!

Najua hilo ni dili, yaani kuwa fisadi
Hata mkini jadili, mwenzenu nitawanadi
Hesabu za kikatili, napiga niwe fisadi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza Wabongo!

Na wala sina huruma, ni sifa yangu fisadi
Halafu tena nasema, nauza hata vya jadi
Nasema mtanikoma, msichezee kaidi!
Fisadi ama kaidi, nitawaliza Wabongo!

Na kila chenye thamani, mwenzenu nita kinadi
Sitoufanya utani, hata mpate shahidi
Fidia ya ki mjini, nitawatoza na kodi
Fisadi ama kaidi ,nitawaliza wabongo!

Mseme hili na lile, na wala sito jirudi
Mpige hata kelele, mfie kwenye migodi
Niuze hata vya kale, halafu mje vikodi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wabongo!

Kaditama ya tamati, kikomo changu fisadi!
Misitu pia na miti, kati ya nitavyonadi
Ni mwisho wa zangu beti, si mwisho wa ukaidi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wabongo!

"Fisadi Chipukizi"
 
Kaka/dada wewe mafisadi watarajiwa huwa wanaweka nia 2 mioyoni. Dah, sasa wewe waanika kila ki2 hadharani! Nani asiyependa kukamata ma-bilioni bila jasho?!
Nani asiyependa auziwe house ya sirikali karibu na beach kwa bei ya kutupwa?
Nani asiyependa auziwe mgodi kwa bei chee?! Wote ufisadi twaupenda jamani, ila wengine twamuogopa mungu. Kwa kua umeweka hadharan ndoto zako ovu, hata mie naungana na waungwana wengine kuku2k..a
B..LOCKS we
 
kwa mtazamo wangu mimi huyu mwandishi wa shairi/ngonjera hii anajaribu kueleza maudhui na matamanio wanayokuwa nayo mafisadi,siamini kama yeye mwenyewe kabisa anatamani kuwa fisadi na atundike hapa jukwaani hiyo nia yake.
kinachonifanya niamini hivyo ni uchaguzi wake wa sehemu ya kutundika hiyo ngonjera au shairi,[jukwaa la lugha]
anyaway siwezi kuusemea moyo wake ila huo ni mtazamo wangu tu.
 
Matamanio yangu (kuwa fisadi)

Natamani, natamani, na mimi niwe fisadi
Natamani, natamani, na mimi niwe zaidi
Natamani, natamani, na mimi niwe kaidi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wandugu!

Kaditama ya tamati, kikomo changu fisadi!
Misitu pia na miti, kati ya nitavyonadi
Ni mwisho wa zangu beti, si mwisho wa ukaidi
Fisadi ama kaidi, nitawaliza wabongo!

"Fisadi Chipukizi"

ombi lako lijibiwe, ewe mja wa manani
kwani utamanilo, hakika ni la msingi
maana ukizikamata, malofa utatutesa
wenetu utawalamba, kiasi watakukoma.

amina....milele...na iwe....
 
Choveki, shairi lako ni zuri sana! ...Nimelipenda. Umertuonyesha jinsi matapeli wanavyopanga kutuvurugia uchumi wetu watanzania, na jinsi vitendo vyao vilivyo kero kwa jamii!
Kwa mtu mwelewa wa shairi lako ana mengi sana ya kujifunza hapa, tuletee mengine mkuu tupate hasira za kuwamwaga hawa pakamwitu!
 
Back
Top Bottom