Nataka nizae mapacha

Nataka nizae mapacha

Discoverer

Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
58
Reaction score
12
Wataalam na wanazuoni mliko jamvini. Nina mtoto mmoja mwenye miaka miwili sasa. sijawahi kutumia aina yoyote wa njia za uzazi wa mpango na wala uzazi wangu hauna shida.

Kwa sasa nina plan kupata ujauzito wa pili ila ningependa nizae mapacha. Kwenye familia yangu na upande wa mwenzagu hakuna historia ya mapacha.

Je nitumie njia gani au dawa gani??? Naomba ushauri
 
DISCOVERER

Ukitumia madawa utaumia, maana akina Sangoma hawatakwambia kwamba dawa haipo! Watakupa mizizimizizi tu!

Lakini kwa ufahamu wangu, hakuna dawa ya MAPACHA, na hali kwako inakuwa ngumu zaidi, maana hakuna historia hiyo katika Koo zenu!

Pia kutotumia dawa yoyote ya Uzazi wa Mpango vilevile haina impact kubwa kwamba labda inaongeza uwezekano wa wewe kupata mapacha.

Kwa imani yako, mwombe Mungu wako, maana Mungu wetu ni tajiri wa kila kitu!
 
utapata mawazo mengi sana kwa hii mada hapa....ila best thing ni kuenda kwa washauri wataalamu ambao watakupa njia za kutoa dozi za mapacha......
 
Hapo mama ni timing tu vitu vikichungulia tu megwa.
 
Wataalam na wanazuoni mliko jamvini. Nina mtoto mmoja mwenye miaka miwili sasa. sijawahi kutumia aina yoyote wa njia za uzazi wa mpango na wala uzazi wangu hauna shida. Kwa sasa nina plan kupata ujauzito wa pili ila ningependa nizae mapacha. Kwenye familia yangu na upande wa mwenzagu hakuna historia ya mapacha. Je nitumie njia gani au dawa gani??? Naomba ushauri

Kwa nchi zilizoendelea waweza kuwazaa hao mapacha. Njia wanayotumia ni ya kukupandikiza mayai yaliyopevuka ni wewe kuchagua unataka watoto wangapi. Kule Houston, TX kuna mama mmoja alikuwa na ka hobbie kama kako yeye aliomba wampandikize mayai nane, sasa hivi analea hao watoto wake. Pesa yako tu ndugu 'mvumbuzi'.
 
kama alivyosema huyu jamaa hakuna historia ya mapacha kwenu wala kwa mumeo ni ndoto hiyo tena ya kusahau.

Nakushauri tu uzae uzazi wako wa kamoja kamoja ila uwabananishe sana wanaweza wakawa mapacha wa kubumba.
 
...... Kule Houston, TX kuna mama mmoja alikuwa na ka hobbie kama kako yeye aliomba wampandikize mayai nane, sasa hivi analea hao watoto wake. Pesa yako tu ndugu 'mvumbuzi'.

Ndugu mheshimiwa, unaongelea sehemu gani?
 
Hapo mama ni timing tu vitu vikichungulia tu megwa.

Fidel80 umesoma jina la mtoa mada lakini, anaitwa DISCOVERER sasa sijui anataka kumwambia nini Sir GOD kuwa huyu mmoja mmoja unayenipa watanichosha na kitumbo kila mara?

Au nimuulize mtoa mada kama kuna sehemu amepata bonus kuwa akipata twins ameula?

Otherwise namshauri kuwa kwanza amshukuru MUNGU kwa huyo mmoja aliyempata na kwamba hana tatizo la uzazi otherwise hasimjaribu MOLA anaweza akapigwa four twins akaanza kuomba tena msaada wa kuwalea.
 
utapata mawazo mengi sana kwa hii mada hapa....ila best thing ni kuenda kwa washauri wataalamu ambao watakupa njia za kutoa dozi za mapacha......

Labda kama anataka kupandwa mimba kama kusia mbegu shambani. Na kimsingi hii ni kumnyima mumewe haki yake ya tendo la ndoa. Yeye apige huyo mmoja mmoja tu mpaka atakapofikisha hiyo idadi aliyoipanga
 
Huyu anatest zali la mentali ooh! watu wanatafuta watoto wanakosa yeye analeta gozi gozi la mapacha.
 
Huyu anatest zali la mentali ooh! watu wanatafuta watoto wanakosa yeye analeta gozi gozi la mapacha.
hahhahahah Carol mbona wamshambulia hivyo mwenzio mummy? mwache bwana kama ana fantasy hiyo basi mwache aitafute ikishindikana atainua mikono, sidhani kama ana lengo la kumkufuru Mungu au kwamba hatosheki na alichopewa sometimes inakuwa ni fantasy tuu.labda anataka akizaa wawili wawe watatu apumzike.
 
Ukitaka mapacha fuata njia hii, siku ya 8-12 utapata mapacha wa kiume watupu, siku ya 13-16 mapacha wa kike tu.

Chakufanya ukitaka jinsia yoyote fanya tendo la ndoa ktk siku yoyote nilizotaja hapo juu, kisha tumia kwa wingi soya ktk wiki 12 za mwanzo,

Soya itasababisha yai lilorutubishwa kugawanyika haraka na kupata mapacha wa jinsia mojawapo,

Ili upate mapacha wa jinsia tofauti, wasiliana nami ktk private massage.
 
kwetu tuna history ya mapacha,naweza kukusaidia nawe ukawapata...kwi kwi kwi
 
we zaa kawaida tu.
ongeza mmoja anatosha, unataka mapacha wa nini?
we megwa tu kawaida ok!
 
Kuzaa mapacha ni mpango wa Mungu wala wewe huhitaji kupanga iwe hivyo.
Ukifuatilia mada zilizopita ambazo zinaeleza jinsi mapacha wanavyopatikana utaona ni bahati nasibu tu.
Mapacha wanapatikana baada ya yai kugawanyika na ninavyoelewa mimi hakuna anayeweza kuligawanya ila inatokea bahati tuu.
 
Ukitaka mapacha fuata njia hii, siku ya 8-12 utapata mapacha wa kiume watupu, siku ya 13-16 mapacha wa kike tu.

Chakufanya ukitaka jinsia yoyote fanya tendo la ndoa ktk siku yoyote nilizotaja hapo juu, kisha tumia kwa wingi soya ktk wiki 12 za mwanzo,

Soya itasababisha yai lilorutubishwa kugawanyika haraka na kupata mapacha wa jinsia mojawapo,

Ili upate mapacha wa jinsia tofauti, wasiliana nami ktk private massage.

Ama kweli wajinga ndio waliwao. Eti yai lililorutubishwa litagawanyika haraka na kupata mapacha. Yaani yai (moja) lililorutubishwa na mbegu moja tayari ni mtoto mmoja huyo, halafu ligawanyike - yaani mtoto agawanyike mara mbili?
Hiyo ni sayansi ya ajabu - labda ungemwambia afanye cronning, vinginevyo naona unajenga njia ya kukutana nae faragha.
 
Muone Daktari akushauri kitaalamu - unaweza kupata mapacha hata zaidi ya wawili kwa kutumia dawa za kuongeza uzazi -fertility drugs kama Clomid, Metformid. etc..ila uwe tayari - kisaikolojia na hata kiuchumi bila kusahau kiafya kupata watoto hata 8! si unataka watoto wengi?
 
Discoverer, jas go to google n type 'how to conceive twins naturally' utapata majibu kibao!
Warning: Haya majibu
- Hayana guarantee
- Yanategemea sana mambo mengine meeeeengi kama historia, umri, afya yako n.k
- Yapo too advanced, uku kwetu utaalamu huo haujafika n.k
So u beta take ushauri wa walio wengi kuepusha frustrations-we pata mimba kawaida atoke wa kwanza uzae tena!
 
Back
Top Bottom