Nataka Serikali moja tu ya Muungano, sitaki mbili wala tatu

Nataka Serikali moja tu ya Muungano, sitaki mbili wala tatu

Ishu sio chadema wala CCM,ishu tunatakiwa tuwe na serikali moja,taifa moja na nchi moja ya Tanzania,yenye Rais mmoja,Bunge mmoja,na dola moja!na sio mbili mbili kama sasa huyo ndio ubaguzi mkuu unatuletea kero za MUUNGANO!!

Tukiwa wamoja wenye haki sawa wote hakutakua na kero za MUUNGANO tena nchini!!!

Kero hizi ni matokeo ya serikali mbili,Bunge mbili,mahakama mfumo mbili yaani mbili mbili WAKATI wengine wanataka tatu tatu ambayo sio KABISA!!

Tukianza tatu tatu tunaua mawazo ya NYERERE na karume kuungana!!
Chazo cha yote ni DP world imewavuruga kweli kweli
 
Tumekuwa maskini kama nchi Kwa sababu ya muungano! Walioshauri na kulazimisha tuungane Sasa wanatucheka! Na sababu za kuungana zilikuwa za kijinga Kwa Dunia ya Leo, ni bora kuutamatisha huu muungano..
 
Huu muungano ni jinamizi lisiloeleweka na tena waTanganyika ni wavumilivu sana wangekuwa na roho kama za wazanzibar siku nyingi wangeshauvunja
 
Muungano ni ujinga na hauna maana kila mtu afanye yake.Muungano ndio unapelekea mtu mmoja kuuza cha mwingine bila hata huruma.Haya mambo ya Muungano yaishe Wazanzibar wametufundisha kitu kimoja kikubwa sana
 
Mi nadhani kukubali uwepo wa serikali mbili au tatu ni kuvunja muungano wetu, Serikali unatakiwa iwe moja tu wala si vinginevyo.

Kinachoitwa kero za Muungano ni matokeo ya serikali mbili za kibaguzi zilizopo

Tunapaswa tuwe na Rais mmoja na makam wake kutokea mahali popote pa muungano bila kujali uzanzibari wala utanganyika!

Niwaombe viongozi wakuu wa mihimili ya dola waanze kufikiria serikali moja tu ya muungano na sio mbili wala tatu!

Asanteni.
Naunga mkono hoja Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja? na Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

P
 
Bill Clinton alikuwa anasema hata kama Democrats na Republicans wanapingana,lazima tukubaliane jambo moja,kwamba kila mtu anahitaji kula.
Kwa hiyo isitokee hali kwamba Chama
kimoja kikiwa kinawazuia wafuasi wa chama kingine kupata riziki.
Utasikia biashara za Mbowe zimeshambuliwa,utasikia Sugu kashindwa kujenga hoteli Mbeya mpaka imebidi Magufuli aingilie kati.
Ndiyo matatizo yanayotokea,mnabishana,serikali moja,serikali mbili,serikali tatu;watu wana njaa,we umeng'ang'ania tu , Muungano Muungano,mpaka wanakuambia wanataka kuvunja Muungano.
 
Niwaombe viongozi wakuu wa mihimili ya dola waanze kufikiria serikali moja tu ya muungano na sio mbili wala tatu!
Hili hulipati kwa hawa waliopo sasa; kwa sababu ni wanufaika wakubwa wa muundo huo wa muungano.
Angalia ngonjera wanazofanya kuhusu Katiba Mpya, usidhani kuna jambo lingine lolote linalowatia hofu zaidi ya huo Muungano; na ndiyo sababu kubwa ya kuzungushana hivi.

Angalia baadhi za wizara, kama hiyo ya Mambo ya nje, matatizo yake yote yanatokana na kulembalemba kwingi kwa hao hao viongozi. Kila mwezi wanabadili mawaziri wa wizara hiyo, wakidhani lembalemba zao za kuridhisha upande mmoja wa muungano zitanyamazisha kelele ndani ya wizara hiyo.

Mkuu, 'NAMBA', nami niongeze sauti kuunga mkono hiyo serikali moja, ila mimi nakwenda mbele zaidi, kama hawataki ondoa Muungano usiokuwa na manufaa kwa upande mmoja wa muungano huo.

Serikali tatu ni maigizo tu yaleyale ya kuwa na muungano usiokuwa na maana yoyote.

Kwa hiyo, unachotakiwa sasa kutusaidia nacho kwenye mada yako hii, tupe mapendekezo ya namna gani tutafikia lengo hilo zuri la serikali moja. Usiishie tu kuhimiza.
 
Back
Top Bottom