Nunua au tengeneza vitoroli vya chuma vyenye mataili ya baiskeli vitatu (kimoja huanzia Tsh 150,000 hadi 200,000) kisha wakabidhi vijana wawe wanafanyia kazi na kukulipa kiasi fulani cha fedha kwa siku au kwa wiki. Mfano ukiwa unapata Tsh 2,500/- kwa kila kitoroli kwa siku, kwa vitatu utakuwa na Tsh 2,500 X vitoroli 3 X siku 30 = Tsh 225,000/- kwa mwezi. Ukiwa serious unaweza kutengeneza vitoroli vipya kila mwezi kila unapopata mapato hadi ukawa navyo vya kutosha na kuwakabidhi vijana katika maeneo mbalimbali kulingana na eneo ulipo. Chukulia mfano ukiwa navyo 100, kwa mwezi utakuwa unaingiza kiasi gani?