Natamani ex wangu anitafute

Natamani ex wangu anitafute

Mimi na huyu mwanaume tulikaa kwenye mahusiano kwa miaka 7. Baada ya kumaliza chuo, ilikuwa ngumu sana kupata kazi. Mimi nilibaki nyumbani nikawa nafanya kazi kwenye duka la baba yangu. Nilikuwa napata hela kidogo kidogo, namtumia yeye aliyekuwa Dar akijitafuta. Pamoja na umbali, lakini tulihakikisha kuwasiliana mara kwa mara na mara nyingi alikuwa ananionyesha kunipenda sana.

Kwa bahati mimi nilipata kazi benki moja hivi. Nilianza kama wale wadada wa kuzunguka mtaani kutafuta wateja, kisha nikaja kuajiriwa sehemu ya mikopo.

Yeye alifurahi na tukawa na mipango mingi. Mshahara wangu wa kwanza nilimpa ili yeye kutoka alipokuwa, kuja huku nilipo. Tukaanza kuishi pamoja na hela iliyobaki akafungua biashara. Mwanzo kila kitu kilikuwa vizuri kwani kulikuwa na upendo, lakini baadaye nilianza kumuona kama mzigo. Kila nikitoka asubuhi weekend kazini, namuacha nyumbani kwani yeye biashara yake ilikuwa ndogo, hivyo hakuwa na sababu za kuamka asubuhi.

Na kama unavyojua kazi za benki, unakuta mara nyingi kutoka ni saa moja usiku mpaka saa mbili, hivyo nikirudi nyumbani namkuta yupo tu.

Ingawa hakuwa akiomba pesa kwa kuwa ana biashara, lakini nilikuwa namkasirikia bila sababu. Nilijikuta naanza kumchoka na kumuona kama mzigo. Nikaanza kumfanyia visa, kutoka bila kumuaga, kuchelewa na mara nyingine kulala nje nikimwambia kuwa niko kwenye safari ya kazi. Kwa wakati huo, sikuwa nachepuka lakini nilipenda kuondoka kulala kwa marafiki zangu ili tuweze kutoka usiku.

Siku moja kulikuwa na sherehe ofisini, kuna bosi wetu alikuwa anaondoka hivyo tulikuwa tunamuaga. Nilimuambia na asinisubiri kwani itakuwa usiku nitalala kwa rafiki yangu. Ingawa hakupenda lakini kwa kuwa mimi ndiyo nilishakuwa mwanaume hapo, alikuwa hana namna. Nilienda na nilipofika huko nilizima kabisa simu yangu kwani alikuwa ananitafuta kila mara mpaka ikawa kero.

Kila baada ya muda alikuwa anapiga simu ili kujua kama sherehe imemalizika au la, nilimdanganya simu imeisha chaji, baadaye nikazima. Hapo nilipata uhuru kidogo kufurahia. Basi katika kuondoka nilipanga kwenda kulala gesti kwani rafiki yangu ambaye nilipanga kwenda kulala kwake, mwanaume wake alikuwa amekuja. Basi kuna mfanyakazi mwenzetu yeye ana gari, hivyo alituzungusha kutupeleka wanawake wote, mwisho akataka kunirudisha nyumbani, nikamwambia hapana, mimi sijisikii kurudi kwangu, nataka kwenda kutulia na kwa kuwa kesho ni Jumapili nataka kupumzika.

Aliniuliza wapi, nikamwambia gesti fulani. Hakufikiria mara mbili, alinipeleka mpaka pale, akanidindikiza mpaka mapokezi. Nilipotaka kulipa, akaniambia hapana, akalipa kisha akataka kuondoka. Hakutaka kulala na mimi, hakuonyesha hata kama ana hamu na mimi. Kuna kitu kama kilinipiga, kwanini hataki kulala na mimi? Kwanini haonyeshi hata kunitamani? Mimi ni mbaya?

Nilikuwa nimekunywa wine tu lakini nilijifanya kama nimelewa, nikamuomba basi aniingize chumbani maana sidhani kama nitajua hata chumba changu ni kipi. Nilimuambia wakati anataka kuondoka, hakusita, alinipandisha ngazi mpaka ghorofa ya pili kwani hakukuwa na lift. Akanipeleka mpaka kunifungulia mpango nikaingia ndani.

Mimi nilijirusha kitandani nikapanua miguu huku gauni langu la kifupi likimwagika upande juu na kuacha uchi. Nilijifanya kama sioni ila nilikuwa nikimuangalia kama ananitamani au la. Hakuonyesha dalili za kunitaka hivyo nikanyanyuka na kujifanya natapika. Alirudi, akafunga mlango na kunisaidia mpaka chooni. Kufika nilijikaza mpaka nikatapika kweli. Alikaa pale kama dakika kumi nikiendelea kutapika, kisha akarudi kitandani.

Nilijifanya kama sijitambui. Nilivua nguo zote mbele yake na huo ndiyo ukawa mwanzo wetu. Nililala na yule mwanaume yeye bila kupanga na mimi nikiwa nimejipanga.

Asubuhi niliamka, nilimlaumu kwanini kanifanyia hivyo wakati yeye anajua ana mke wake. Ndiyo, nilijua kuwa kaoa, kwani mke wake ingawa yuko mkoa mwingine, lakini mara nyingi huja ofisini na kila mtu anajua, kwani ni mchangamfu sana. Nilimtazama kwa mshangao, nilijilalamisha huku nikimtaja mke wake. Yeye alikuwa kimya, akaniomba nisiongee na mtu, lakini huo ndiyo ukawa mwanzo wa mahusiano yetu.

Mara nyingi nilienda kwake, nampikia na kumfanyia kila kitu. Ni mwanaume ana pesa, ananihudumia, ananinunulia kila kitu. Kweli kwa mara ya kwanza nilijisikia niko na mwanaume. Nilizidisha vituko kwa mwanaume wangu mpaka ikafika hatua nikamwambia mimi sikutaki.

Nina mwanaume wangu anayenipenda, hivyo siwezi kulea mwanaume. Nilimtamkia maneno mengi ya shombo, pamoja na kwamba hakunifanyia chochote ila alikuwa ananiomba sana msamaha, aliniomba mpaka kulia, lakini mimi sikujali. Kwa akili yangu nilikuwa naamini kuwa huyu ananiomba msamaha kwa sababu ana njaa, hivyo simtaki.

Aligoma kuondoka, lakini kuna siku nilirudi nyumbani nikachukua vitu vyangu na kuhamia kwa yule mume wa mtu. Kipindi hicho alikuwa ananiambia kakorofishana na mke wake, na kweli kila siku walikuwa wakigombana. Kwa akili yangu niliamini watatengana. Sikujua kama wanagombana kwa sababu yangu, kwani mwanaume alikuwa hataki aje tena huku tulipo.

Baada ya kuchukua vitu vyangu, mwanaume wangu hakuwa na maneno, aliondoka na sikumtafuta tena. Nilimblock kila sehemu. Yeye pia hakunitafuta. Haikupita hata mwezi, nilijikuta nina mimba. Nilimwambia mwanaume, akaniambia hakuna shida, yeye anataka mtoto, na kuna siku alinambia anataka kumuacha mke wake kwa ajili yangu.

Nilihudumia mimba na nikawaambia nyumbani kuwa nina mchumba wangu na nina mimba, hivyo nikakaribia kujifungua atakuja. Tulipima ultrasound na kugundua kuwa nina mapacha watatu—watoto wawili wa kike na mmoja wa kiume. Mwanaume alionyesha kufurahi kwani yeye na mke wake wana watoto wawili wote wa kike.

Ujauzito ulipofikisha miezi 7, nilimkumbusha mwanaume kuhusu ndoa yetu, akaniambia yeye kuna mambo anapitia kwenye familia yake, hivyo nisubiri nikishajifungua.

Kweli nilipaniki, nikaanza kufuatilia na kuchunguza simu yake. Nikagundua kuwa anamuomba mke wake msamaha. Kumbe mke alishaondoka kwenye nyumba yao waliyojenga wote na karudi kwao kwa sababu ya mwanaume kubadilika. Sikumuuliza mwanaume, nilichukua namba ya mke wake, nikampigia simu na kujitambulisha.

Nikamuambia mimi ni fulani, niko na mume wake, akanijibu, "Mbona najua muda mrefu? Nimeshaambiwa kila kitu." Akaniambia, "Lakini nimekwachia mwanaume, nimeamua kuendelea na maisha yangu. Maombi tu, muambia mwanaume wako asinisumbuee anipe talaka wewe, si una mimba yake sasa? Kwanini ananing’ang’ania?"

Hapo ndipo niliharibu. Mwanaume kusikia nimemtafuta mke wake, alibadilika sana, alinitukana sana, kuniita malaya, mjinga, na kila aina ya matusi. Aliniambia hawezi kunioa kwani hata watoto hajui kama ni wake. Alisema, "Tunasubiri ukijifungua ndiyo tupime DNA."

Nilijua kama utani, ila haukupita mwezi hata kabla ya kujifungua. Kumbe tayari alikuwa akifuatilia uhamisho, alichukua kila kilichokuwa chake bila hata kuniaga, aliondoka.

Kweli nilipambana mpaka kujifungua wanangu watatu. Ni wafanana na baba yao, copy kabisa. Aliposikia nimejifungua, alinitafuta kuniomba picha, nilimtumia, nikaamini labda atajirudi, ila alijibu meseji moja tu: "Ni watoto wangu, nitalea, lakini sasa hivi napambana na ndoa yangu, mke wangu arudi."

Hakunitafuta tena na mimi sijamtafuta. Wanangu sasa hivi wana miaka 3. Niliingia online, nakuta X wangu kafunga ndoa. Wafanyakazi wenzake wa TRA walikuwa wanampa zawadi. Imeniuma sana, kumbe baada ya kuachana na mimi alihangaika sana huko matani, kisha akaja kupata kazi TRA.

Natamani hata kumtafuta kumsalimia, kumuomba msamaha, lakini naumia hasa nikimuangalia mke wake. Ni mzuri kuliko mimi, hata kujiamini kumtafuta siwezi. Mimi ni single mother wa watoto watatu. Anajitahidi kuwapenda sana wanangu, lakini bado nina hasira kila nikifikiria ameoa.

Natamani X wangu anitafute hata niwe mchepuko wake tu. Mimi niko tayari, ilimradi niwe na amani!
Screenshot_20241208-094242.jpg
 
Pole ndugu yangu kama ni kisa cha kweli.
Unaweza kutukanwa saana lakini sote ni binadamu, tu wenye kupungua ili mwenyezi Mungu awe mkamilifu.

Ingeweza kumkuta yoyote hata mimi ila imekuangukia wewe, pole usijali maisha yaende tu .
Kumbuka jitihada hazizidi kudra, tunafanya yote tuwezayo ila mkamilishaji ni Mungu.
 
Ctrl + C
Ctrl + V

Screenshot_20250224_211407_Instagram.jpg
 
Wewe si unataka mfanyakazi mwenzako wa benki?
 
Back
Top Bottom