Natamani kama Traffic wangekuwa wanavaa ving'amuzi wawapo barabarani

Natamani kama Traffic wangekuwa wanavaa ving'amuzi wawapo barabarani

Omnibu

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
404
Reaction score
399
Salamu kwenu waungwana wa JF. Kusema ukweli imefikia hatua traffic polisi wetu wawapo kazini hasa barabarani kuwa kero na usumbufu usio kuwa na sababu.

Kila baada ya km 1 au 2 unakutana na traffic zaidi ya 4 au 5 na kila mmoja yuko busy kutaka kukusimamisha ni kama vile wanafanyiana timming ya kukusimamisha.

Mfano mzuri ni barabara za arusha mjini na viunga vyake kwa kweli wanakera, na akikusimamisha cha kwanza ni salamu za kutengeneza mazingira then anakupiga mzinga umwachie kitu kidogo, thats why nikatamani wakiwa na vi camera vilivyounganishwa kwenye system za head office zao inaweza kutupungizia usumbufu huu barabarani.Au basi

Ifike wakati na sisi twende kidijital kama nchi za wenzetu gari zote zipitie inspection za kwenye mitambo maalum na iki pass hapo ipewe stika inayoonyesha haina kasoro. Kwa gari za private muda wake inakuwa mwaka mmoja na gari za kibiashara ziwe miezi sita.

Pia kuwe na camera za barabarani zitakazo check speed limit ya eneo husika , kutambua gari kama ina valid insuarence na pia kutambua magari yanayodaiwa faini za polisi nk. Kazi ya traffic polisi iwe ni kufanya mambo mengine ya kiusalama barabarani kama kuvusha watoto na wazee, kuongoza inapobidi kwenye traffic light hasa panapokuwa na foleni ndefu , kuongoza na kusimamia misafara ya wakubwa wanapopita barabarani nk.

Pia kila chombo cha moto yaani magari na vinginevyo vinavyotumia barabara viwe na mfumo wa kidigital yaani contact address ya mmiliki hivyo kikifanya kosa la barabarani mmiliki anapata taarifa direct kwenye simu yake au penginepo atakapotaka yeye kupokea taarifa zake.

Kwa haya na mengineyo yakifanyika usumbufu wa kusimamishana bila sababu barabarani utaisha kabisa.
Niwatakieni wakati mwema.
 
Back
Top Bottom