Pole sana na tatizo hili ila nimefurahi kusikia kuwa unatafuta msaada ili uachane na tabia hiyo mbaya sana.
Ni muhimu sana kufahamu kuwa usagaji ni dhambi, na dhambi ni utumwa (Yoh. 8: 34 - [FONT=Lucida Sans Unicode, MS Arial Unicode, Comic Sans MS, Verdana, Arial, Helvetica]kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi). Wewe mwenyewe kwa kuwa ni mtumwa huwezi ukajitoa kwenye utumwa huo. Ni Yesu Kristo pekee mwenye uwezo wa kukutoa katika utumwa wa dhambi zote (Yoh. 8: 36 - ... basi mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli).
Unachotakiwa kufanya sasa kutubu dhambi zako zote ikiwa ni pamoja na usagaji kwa kumaanisha kuziacha kabisa, sio uache usagaji uanze uasherati na uzinzi na wanaume, hapana (Mithali 28: 13 - Afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali aziungamaye na kuziacha atapata rehema). Kisha mwambie Bwana Yesu akuwezeshe kuzishinda dhambi hizo, yeye ni mwema na mwaminifu sana atafanya. Mfano wa sala ya toba ni huu hapa:
"Mungu wangu, nakuja mbele, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi. Natubu zangu zote kwa kumaanisha kuziacha kabisa. Sitaki dhambi kuanzia leo. Naomba unisamehe. Naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Naomba unipe uwezo wa kushinda dhambi ya usagaji na dhambi nyingine zote ili niishi maisha yanayokupendeza wewe kuanzia leo. Asante Bwana kwa kuwa umenisamehe na kuniokoa, katika jina la Yesu, Amen".
Ukisali sala kama hii kwa kumaanisha utaokoka na kupewa uwezo wa Kushinda usagaji na dhambi zote (Yoh. 1:12 - Bali wote waliompokea aliwapa uwezo kwa kufanyika watoto wa Mungu ...".
Kisha tafuta kanisa wanalohubiri wokovu na uwezo wa kushinda dhambi, epukana na mahali ambapo dhambi haikemewi kwa wazi wazi na wasioamini habari ya uwezo wa kushinda dhambi. Kumbuka Zab. 16: 3 - [/FONT]Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,Hao ndio niliopendezwa nao. Mungu anapendezwa na watakatifu walioko duniani.
Kwa ushauri zaidi unaweza kuni-pm