Natamani kujifunza udereva

Natamani kujifunza udereva

mr man city

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
467
Reaction score
319
Wakuu,

Kabla sijafika ofisi za VETA Mwanza naomba madereva mnishauri hapa.

Nahitaji mwaka huu usiishe niwe nimepata angalau ujuzi wa kuendesha magari haya ya kawaida tu pamoja na leseni yake.

Nimeona VETA ndio chuo kinaonekana cha uhakika. Hizo course zinatumia muda sana maana bado niko na kazi ya kufanya, na nianzie course gani kwa kuwa naona licence zina madaraja tofauti.

Mimi sina idea yoyote ya kuendesha gari. Ndio nataka nianze moja nipate ujuzi. Huwa napata tabu sana nikiambiwa chukua gari uendeshe na sina ujuzi. Location ni Mwanza.
 
Nenda veta kama ipo hapo mwanza usome basic mwezi mmoja ukijaribiwa ukafaulu utapata daraja D!
Utajikuta ni dereva
 
Back
Top Bottom