Oke, hata mtu akikulaumu sasa atakuwa anakuonea dadangu. Waliokushauri kubadilisha simu naungana nao 100% Huyo mwanaume wala usihangaike sana naye, atakutafuta siku moja kama kweli ulimpa moyo wako kwa kina, kwani alipoyagida si alijuwa anaye mke nyumbani? Wewe ndio hukujua. Kwa taarifa yako hata yeye ndoa yake imekula kwake, maana furaha waliyokuwa nayo mwanzo haipo na haitakuja tena. Hata ajieleze vipi hataaminika.
Kama umejisifia mwenyewe kwamba uko gado kishenzi, basi yeye alikuzibia tu njia zako kwa mtu uliyeandaliwa na Mungu wako. Binadamu yeyote hukosa na kamwe kosa lako sio la kustahili kuuwawa au kufa. Nijuavyo wanawake wote hupenda kama ulivyofanya kwa kujimimina moyo wako kwa mpenzi wako na ndicho kinatakiwa hata wanaume wafanye. Lakini alikikosa kwa mkewe alichokipata kwako. Hajakuacha ila amelazimika kutii kiapo chake na labda waliapizana kutoongeza mke mwingine ndio maana hataki kuivunja ndoa yake, isije ikawa kuna viapo vua ukoo hapo na labda kuishi kwa bwana huyo kunategemea mkewe kwa asilimia kubwa, akivunja maviapo ndio kifo chake. Mhurumie pia kwa sababu huumii peke yako bali yule bwana naye anaumia ile mbaya kukosa ulichomzoeza na hana ujanja.
Jitulize na uanze kuangalia dunia ilivyo mviringo, atakuja anayekufaa na utashangaa kwa nini ulichelewa kumpata. Ulimpenda sana huyo sababu haukuwa na alternative ya kulinganisha naye. I tell you, all men are good to women if they find a matching pair. Usimpe mtu hazina yako kabla hujamfahamu sawasawa. Jipe nafasi ya kumjua vizuri unayefikiri unapatana naye. Ama sivyo akuambie waziwazi kwamba matatizo yake ni nini na kikomo chenu ni wapi (Mipaka) ili kama ni kugida kwa kuondoa kiu tu ieleweke na kama ni kwa misingi ya kujenga nyumba pamoja ieleweke. Kama anataka kuchukuwa hati miliki juu yako, usimpe mali ghafi mpaka kwanza amefika nyumbani kwa wazazi wako nawe umefika kwao kujitambulisha. Hapo tena uwe makini, maana wengine ni jasiri kiasi kwamba watafanya yote hayo na bado kisogoni anakuwa na hesabu tofauti. Apewe hifadhi yako pale tu anapokuwa ameleta alichoambiwa kuleta kwenu na wazazi wako, ndio ujijue kwamba mnatakiwa kupozana wakati mnakaribia kuungana. Hakuna uchumba wa miaka unaofanikiwa sana mkiwa mnagidana kila siku. Kwani mnaoana kwa ajili ya nini kama sio migido nayopeana. na haja gani kuharakisha kuoana kama anapata kwako hata bila kuoana?
Ukijiua utakuwa mjinga, maana yeye ataendelea kuishi na ataendelea kudanganya wengine kwa foleni, wewe utabadili cheo na kuitwa marehemu. Huyo utakayempata kwa design niliyokuambia, msijifiche, jianikeni kwamba mna lengo zuri. Kwake nenda mchana kweupe na kwako aje mchana kweupe kila mtu ajue nyie mko pamoja. Unapojificha ndio maana mwanaume anaweza kugida wanawake watano walio marafiki sana na wao wasijuane kama wanamhudumia mtu mmoja, kila mmoja akijifanya amepata kumzidi mwenzie kumbe wote ni nyama ile ile ila mapishi ndio tofauti. Mtawekwa foleni mpaka mkome ubishi. Siku mnapotambua mnaanza kugombana na kuumizana kila mmoja akidai mwenzake anamwibia.
Habari ndiyo hiyo.