Habari zenu wana Jamii Forum. Mimi ni mgeni humu. Ila si mgeni ki hivyo nimekuwa natembelea bila kuwa member. Nimeamua kujiunga ili nipate kushauriwa kwani shida niliyonayo siwezi kushare na mtu ninaye mjua.
Mimi ni mdada wa miaka 32. Ni mrembo sana yaani wale mnaoita 8 figure. Sijisifii ila hilo nimeona nilitamke ili muweze kuielewa vizuri mada yangu.
Nilitokea kumpenda sana kijana mmoja na kuja kugundua baada ya miezi miwili kuwa ni mume wa mtu. Kaka ni muislamu hivyo havai pete na kwa kuwa ni kijana sikuweza kudhania kuwa ni mume wa mtu na kwa kweli ningejua nisinge mpa moyo wangu.
Tatizo niligundua kuwa kaoa wakati nimeshampenda. Na ni yeye mwenyewe alinitamkia kuwa nina mke baada ya kujua sitaweza kumwacha kwani nilikuwa nimekolea.
Tumekaa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka na nusu sasa mpaka pale mkewe alipokuja kugundua. Mimi mkewe nilikuwa nimeshamjua. Ni mdada msomi na ana kazi nzuri sana ila ni wa kawaida na aniingii hata nusu kwa uzuri kwa hiyo nilijua tu kuwa mumewe atakuwa ananipenda mimi zaidi na labda kuna siku nitakuwa mke wa pili kwani ni muislamu.
Tatizo limeanza miezi miwili iliyopita. Jamaa alinipigia simu akanambia mkewe amejua kuwa tuna uhusiano, kwa hiyo mimi na yeye basi kwani hataki kuvunja ndoa yake. Nimeumia sana imagine mwaka na nusu na nimeshampenda sana. Nimejitahidi kumfuata ofisini kwao secretary wake ananambia jamaa kasafiri wakati gari naliona nje ya ofisi. Nimempigia simu simpati naona amebadili namba.
Hivi kweli wanaume mnaweza kuwa wakatili hivi? Kibaya zaidi mkewe kutwa ananipigia simu na kunitisha kuwa atanifukuzisha kazi. Mimi sijali kufukuzwa kazi kwani ninampenda sana huyo mwanaume.
Nishaurini nifanyeje kwa wale wenye uzoefu wa kuwa vimada na wale wenye nyumba ndogo.
Msinitukane jamani. Mimi sijawahi maishani mwangu kutembea na mume wa mtu zaidi ya huyu na sikuwahi kuwaza kuwa yatanikuta. Hivi nyie wanawake wa kwenye ndoa uwa mnawaroga wame zenu? Iweje mtu niliyekuwa nampagawisha the other day leo aseme sitaki kukuona tena kisa tu mkewe kajua?
Na huyu mkewe nimfanyeje aache kunifuata fuata. Maana amekuwa ananipa vitisho kila kukicha mpaka nahofia uhai wangu. Mumewe mwenyewe kesha niacha na yeye bado analeta mikwara wakati nikimwangalia hata ngumi moja namuua.
Hii thread imenisikitisha sana, you know, inaonyesha ujinga wetu wanawake!!! sometimes sisi wajinga sana na wanaume most of the times wanacapitalize kwenye huu ujinga wetu. Imagine mtu anatembea na mume wa mtu halafu hajutii anachokifanya anajidefend kana kwamba ana haki. Dada huyu huyu mgoja aolewe mumewe awe na kimada ataenda mpaka kwa mganga wa kienyeji because mkuki kwa nguruwe mtamu.......
We dada wapo wa dada ma mawowo yao wamelost hamna anayewaingiza ndani ya nyumba, my god sasa why umeachwa na hiyo figure 8????unadai umekuwa ukimpagawisha siku zote!!! yeye ndio elikuambia au unaishi kwa assumptions!!! do you think hips ndio kegezo tosha cha kumpagawisha jamaa, we kweli hata hukufundwa unaweza kuwa na hiyo figure 8 kitandani mambo hayaendi bibi wewe, mwanamke kiuno babu we makalio majaliwa, kuna mwana JF kakuambia you are not a wife material, from your action truly you are not!!! that's why pamoja na figure 8 yako bado hujaolewa while kuna wasichana 24s wanaolewa??? from your attitude my dia huwezi pata wako. Halafu unajifanya unamdharau mkewe:A S 101: ha ha ha jamaa amerudi kiotani babu nashangaa mpaka sasa unaendelea kusoma hz thread hujajiuwa bado!!!!!!!! I have a very deadly poison please give me your address nikupostie!!!!
halafu unaomba usitukanwe!!!!!!! why!!!! you deserve it, kutembea na mume wa mtu tegemea chochote from kutukanwa to kuvunjwa miguu, kumwagiwa acid etc. on top of that unawaita wanaume wakatili????? who told you they are!!! yani ujinga wako unadump kwa watu wengine!!!
Nikuambie kitu na hiyo shape yako utakaa nayo unazurura mtaani jamaa wanachovya then wanarudi kiotani hapo ndipo utakapajua ukweli!!
My advice to you msimchezee kabisa huyo mwanamke, mwogope kaa naye mbali umevuna kwenye shamba lake, we jifanye mbabe atakuharibu sura na jamaa ndo umeshampoteza!!!!!!!!!!!!!!!