Sexual act is a psychological act, ndo maana huwezi kulifanya tendo hilo na ndugu wa karibu kwasababu akili inakataa. Ili uweze kupata hamu ya kufanya hivyo lazima akili ikubali na isitosheke na yule uliyenaye, ni sawa na kusema utamu wa pipi mate yako na utamu wa sex psychology yako! ukiitawala akili yako hiyo utawaona wanawake wote, kasoro mkeo, kama dada zako. Jambo hilo linawezekana kama utakubali kukaa chini ya nguvu iliyo kubwa kuliko akili yako nayo ni nguvu ya imani, wewe ni mkristo? ukristo unasemaje juu ya tendo hilo nje ya ndoa?wewe ni mwislam? uislamu unasemaje juu ya uaminifu kwa mwenzi wako wa ndoa? kama ungekuwa mkristo kama mimi pengine ungeweza maana kwa kumwamini kristo na kuzingatia kuwa nikitoka nje ya ndoa namhuzunisha na namwumiza ungeweza kutulia na huyo mrembo wako. Mimi nimeweza kukaa kwenye ndoa for almost 3 years na sijawahi toka na mwanamke mwingine na sina hamu kwasababu nimechagua kuishi maisha hayo. Fanya uamzi wa busara, ogopa kumuumiza mwenyezi Mungu kwa kufanya aliyokukataza, utaweza tu!Mithali 6:32 inasema "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.