Natamani kununua Subaru Impreza, nini changamoto zake?

Natamani kununua Subaru Impreza, nini changamoto zake?

switch Off

Member
Joined
Oct 30, 2019
Posts
48
Reaction score
186
Habari wakuu

Nilikuwa na wazo la kununua Toyota IST kwaajili ya mizunguko yangu ya kazi, lakini ghafra mawazo yangu naona yanabadilika na kuhamia kwenye Subaru impreza ...nimetokea kuipenda hii gari pia hazitofautiani sana bei na toyota IST ..

SWALI
Je, kuna uwezekano wa kuipandisha juu hii gari na isipoteze mwonekano wake maana ipo chini sana?

Kama kuna changamoto yoyote kwenye gari hii naombeni mniambie.
1591435733827.png

Subaru Impreza
 
Funga rim na tairi kubwa kwa ushauri mzuri ili tairi zisiwe zinagusa body. Ikizidi km 120,000 uwe una monitor oil levels kila baada ya km 2000, zina jambo la kuanza kula oil. Sioni changamoto nyingine ya maana, gari nzuri
 
Vuta hicho kitu, mi ninayo mwezi wa 6 sasa sijaona bado changamoto yoyote! Kuinyanyua kidogo inawezekana na kiwe kitu cha kwanza kufanya ikifika.
 
Mkuu unanishawishi pia ninatumia premio ila nataka nibadili to mentioned one.
 
Funga rim na tairi kubwa kwa ushauri mzuri ili tairi zisiwe zinagusa body. Ikizidi km 120,000 uwe una monitor oil levels kila baada ya km 2000, zina jambo la kuanza kula oil. Sioni changamoto nyingine ya maana, gari nzuri
Nashukuru umesema jambo sahihi, kuna kipindi watu niliwaambia hili jambo lakini wakaanza leta ujuaji, shida ya Subaru zote kwanzia 2009 kurudi nyuma ndo habari ya head gasket issues, tena Subaru za nyuma ya 2000 ndo za kukimbia kama ukoma
 
Nashukuru umesema jambo sahihi,kuna kipindi watu niliwaambia hili jambo lakini wakaanza leta ujuaji,shida ya Subaru zote kwanzia 2009 kurudi nyuma ndo habari ya head gasket issues,tena Subaru za nyuma ya 2000 ndo za kukimbia kama ukoma
Kweli Subaru nyingi zina shida ya head gasket na kama sio oil kuleak.. basi inaweza kuchanganyika na coolant.. issue ni kwenye muundo wa engine zake horizontal pistons
 
Kweli Subaru nyingi zina shida ya head gasket na kama sio oil kuleak.. basi inaweza kuchanganyika na coolant.. issue ni kwenye muundo wa engine zake horizontal pistons

Ila sana ni model za chini ya mwaka 2009 na zikishafika ya km 120,000 ndio hizo shida huweza kutokea
 
Gari poa sana.. mimi ninayo mwaka wa pili huu! Changamoto labda iko chini sana, hizi bara bara zetu za mtaan ni shida.. ikifika fanya kuinyanyua uendelee kula maisha!
Hapo juu umesema unayo mwezi wa sita sasa, lakini hapa unasema unayo mwaka wa pili..
Mbona hueleweki?

Sent from my SM-J105H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom