Natamani kuoa, ila mambo haya ndo yananikwamisha

Natamani kuoa, ila mambo haya ndo yananikwamisha

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Mm ni mwanaume nilie kwenye my late 20's, niliwahi kuwa na girlfriends in my late teens, Ila baadae, baadhi ya girlfriends nliokua nao niliwaacha, because sikua na malengo nao, wanajamii wengi na ndugu na marafiki wananisisitizia nioe, mm huwajibu kuwa sijakaa sawa kifedha, ila kiuhalisia hicho ni kisingizio changu, ukweli ni kuwa hata sahivi nikiwa bilionea, swala la kuoa kwangu bado litakua ni gumu mno, kwasababu haya ndio mambo ninayokutana nayo.

1) Wanawake ninaowataka mm, wengi wao wako kimaslahi, yani mdada najaribu kumtongoza, lakini nagundua anachofata kwangu ni pesa tu, hana hisia na mm, kiukweli mm sijisikii vizuri kupendewa hela na mwanamke, na sidhani kama kuna binadamu yoyote chini ya jua hili anafurahia kupendewa hela, wanawake wengi wana-fall kwenye hii category, yani wako very fake..

2) Napata attention kutoka kwa baadhi ya wanawake, kuna baadhi ya wadada wanaonesha kunitaka kimapenzi, ila daah nikiangalia muonekano wa hao wanawake, huwa natamani kulia machozi, yani hawana hata average looks. Hawanivutii kabisaaaa, hata nikijaribu kujilazimisha kuwataka, roho yangu inakataa kabisa, hivyo naishia kuwapotezea, maana kwa ninavojijua nikiwa nao kwenye mahusiano, nitakuwa najitesa.

3)Saa ingine nikimtaka mwanamke toka moyoni, process ya kumtongoza inakuwa ni kama kung'oa jino bila ganzi, utakuta namshobokeea mdada, ila unakuta mdada hajui kama nipo dunia hii, yani unakuta she doesn't give a f*ck, unamshobokea leo, mnaongea wee, kesho mtu hakukumbuki..mdada unakuta ana play head games kibao (wanaume wenzangu mnanielewa hapa)

4) EXTRA POINT: Last but not least, kama binadamu wa kawaida natamani kupata mtoto, ila saa ingine kichwani nafikiri kumleta mtoto duniani ni kumleta kwenye mateso, kwasababu dunia hii imejaa umaskini, maumivu, vita, magonjwa, bado ukifa na dhambi ndogo tu uende ukachomwe kwenye moto wa milele, kama binadamu Kabla ya kuzaliwa tungekuwa tuna uwezo wa kuchagua kuzaliwa duniani au laa baada ya kuoneshwa dunia jinsi ilivyo, mimi binafsi ningekataa katukatu kuja duniani..cha ajabu hii dunia hata ukiwa pesa nyingi bado sio suluhisho, unaweza kuwa tajiri lakini, matatizo Plus maumivu yako palepale..

Kwa hizo point 3 za mwanzo nilizotoa hapo juu, hivi wanajamvi hata leo nikiwa bilionea nitaoa kweli??, sijajua nakwama wapi, kuna mwanaume humu JF anapitia, au alipitia hiki ninachopitia??
 
Namba nne,matatizo ya Dunia huwezi kuyamaliza,yalikuwepo,yapo,na yataendelea kuwepo kwa miaka zaidi ya 1000 ijayo.Huna Cha kufanya,tafuta pesa,jijenge,leta mtoto apate huduma nzuri.Life Haina garantii,unaweza ukawa na pesa kama Bkheresa,ukapata mtoto,akizaliwa tu,unafirisika,na unapoteza kila kitu,fikiria Lumumba wa Congo wakati anaenda kuuwawa,watoto wake walikuwa Bado wadogo chini ya miaka 5,aliwaza vipi kuhusu maisha yao!?
Mandela je?jera miaka 27!!
Life is all about taking risk,thats what makes it worth living.
Namba moja,kuhusu Kupata mdada atakae kupenda kutoka moyoni bila kuangalia una nini!!!hapo utakuwa huwatendei haki wakina dada,Upendo wa ndani sio tukio,ni mchakato,
It's not an event it's a process,mtu amuki asubuhi akakupenda kutoka moyoni!!inachukua muda kujenga hicho kitu,hata huyo unayemuona anapenda pesa,ukimpa nafasi,na kumuonyesha mapenzi yako,utashangaa,na usijidangsnye,kwa maisha ya sasa,ndoa ni makubaliano tu,hakuna aliye tayari kufa kwa ajiri ya mwenzie,
Njoo na mapenzi weka mezani,mwenzako ataona tu,naye atatoa yake.
Kabla hujachukua uamuzi wa kuoa,
OMBA MUNGU SANA.
Angalizo"usipende kwa asilimia 100,penda lakini uwe tayari kuachia,just in case,human are unpredictable!!
Bila hivyo,mdogo wangu utakufa kwa stress.usitafute furaha ndani ya mwanadamu,ukiacha watoto wako tu.
 
Subiri ufike walau 30+ akili ikomae utajua nini unataka. Muda huu endelea kufanya mambo mengine.
Wakati unasubiri inaweza tokea ukapata mtayeelewana, wajati mwngine haya mambo huja automatic.
 
Kwa namna nimekuelewa mleta mada ni kuwa una struggle kupata mwenza wa kufanya nae maisha.

Na unataka specific yule ambaye ataendana na fikra zako au matarajio yako. Kuna mdau hapa ameongea madini sana pale juu.

Kakwambia kupenda ni process especially kwa mtu ambaye ulimfuata wewe. Kumbuka na yeye ana hisia kama wewe so unapomfuata unataka awe tayari kuvutiwa na wewe automatically bila wewe kutia effort yoyote.

Pengine kuna dosari upo nayo aidha kitabia, kimwenendo ambayo inawa turn off hawa mabinti. Au pengine una aina ya maisha ambayo haiwavutii kutaka kuingia na wewe.

Mahusiano ni kama kuvua samaki , lazima uwe na chambo ili kuvutia samaki.

Lakini pia mahusiano ni kama biashara lazima ujue namna ya kuvuta wateja wa aina ya bidhaa au huduma unayouza. Ukisema ukasirike na kususa kwann wateja hawaji utapoteza focus ya kujua nini kimepungua au kukosekana hadi wanashindwa kuja.

Umeongelea swala la watu kuwa na pesa ila hawana furaha, ofcourse ni kweli hiyo ipo sana tu. Na ni matokeo ya kufanya maamuzi,au mipango kwa kukurupuka au bila kufuata taratibu. Hata wenye pesa pia ni binadamu na wana character flaws ambazo hazivutii wengine.

Unaweza kuwa na pesa ila kama kauli, mwenendo wako,tabia zako, mipango na maamuzi yako na shughuli zako ni za kukera wengine hakuna atakae vutiwa kuwa karibu yako.

Nadhani ni vema ujitathimini ni kipi ambacho kinafanya hao unaowapenda wasiwe interested na wewe. Je huwa unapowafuata unawaingia kwa malengo gani?!

Wewe una malengo gani na hao mabinti hadi wakuone muhimu?! Kumbuka haya ni maisha kwao pia why sasa yaende kwa terms zako bila kuwaelewa wanataka nini?!


Nakuja ...... Ngoja nichaji sim kwanza.....
 
kanuni ni moja tu.....jifunze kumpenda anae kupenda...
Hii kitu nilidhani ni rahisi,lakini ni jambo gumu sana kumpenda mtu eti kwasababu anakupenda
NI RAHISI sana ukiufundisha ubongo wako ukubari kuwa unavyo vipenda sio haki yako vinavyokupenda ndivyo unavyo stahiiri...kwa hiyo uambie ubongo wako ukubariane na matokeo kupenda mtu asie kupenda ni kujiingiza kwenye moto wewe mwenyewe...yanini uteseke wakati yupo anae kupenda as long ni kuwa binaadam bado tunaumbwa na ninaamini kuwa hakuna binaadam mbaya....
 
kanuni ni moja tu.....jifunze kumpenda anae kupenda...

NI RAHISI sana ukiufundisha ubongo wako ukubari kuwa unavyo vipenda sio haki yako vinavyokupenda ndivyo unavyo stahiiri...kwa hiyo uambie ubongo wako ukubariane na matokeo kupenda mtu asie kupenda ni kujiingiza kwenye moto wewe mwenyewe...yanini uteseke wakati yupo anae kupenda as long ni kuwa binaadam bado tunaumbwa na ninaamini kuwa hakuna binaadam mbaya....

Hahahh kwangu mie huwa ni ngumu hii

Ubongo wangu huwa unaniambia tangu mwanzo "huyu kiumbe huwezi kumpenda" so haipo namna nitampenda eti sababu amenipenda
 
Hahahh kwangu mie huwa ni ngumu hii

Ubongo wangu huwa unaniambia tangu mwanzo "huyu kiumbe huwezi kumpenda" so haipo namna nitampenda eti sababu amenipenda

Kuna mdada sifahamiani nae sana, sikuwahi mtongoza (kumwambia kuwa nampenda ingawa kiuhalisia namtaka) kuna siku tulikutana njiani, nikampa biskuti ndogo ya tshs mia mbili, baada ya siku 2 rafiki zake wote wanajua nilichomfanyia..Sasa sijajua niende nikamwambie namtaka kimapenzi, maana mmh kukataliwa si kuzuri sana.. Joanah
 
Game ni moja tuu
“ usioneshe kukitaka sana kitu”
Acha kitu/ mtu kije unexpectedly hasa mwanamke.

Hata ndoa, mwache Mwanamke ainitiate huo mchakato, jifunze kuwa passive hata kwenye mambo ambayo unayataka... wewe unamalizia tuu...

Ukimwonyeshea shida yoyote mwanamke( mapenzi sana, unmtaka kindoa, nk)analose interest na wewe hapohapo.

Kula anaekuja huku ukisubiri type yako ijilete kimasihara.
 
Back
Top Bottom