Natamani kusoma Mechanical Engineering, naomba ushauri

Natamani kusoma Mechanical Engineering, naomba ushauri

David11

Member
Joined
Mar 15, 2024
Posts
28
Reaction score
19
Mimi mdogo wenu nimemaliza kidato cha nne mwaka Jana na ufaulu wangu ni kama ifuatavyo

Phy D math D chemia C Biology C.

Huo ndio ufaul wang na Nia yangu ilikuwa ni kwenda chuo nikasomee mechanical engineering badala ya kwend advance maan combination zinabalance arts na mm Sina Nia ya kusoma arts
 
Mechanical engineering soko la ajira linetawaliwa na mafundi wasio na elimu.

Ufundi hautazami cheti bali ni ujuzi wa kufufua mitambo ama engine zilizofeli.

Hivyo waajiri hawaoni umuhimu wa kuajiri mechanical engineers wengi. Maana wanajua kazi zinafanywa na mafundi wa mitaani tu wenye uzoefu wanaajiri engineer mmoja tu wa kuzugia
 
Ndugu yangu ni lazima apitie veta asugue miaka mitatu, apate cheti ndio aende huko asugue tena mitatu kupata diploma, ndio akasome hio digrii uliyomshauri
Hamna kitu kama iko.

Screenshot_20240723-230709.png

Entry qualifications za Diploma izo DIT.
 
Yaani shwaaa anaruka tu mpaka diploma na form four?
Yeah 3 years Ordinary Diploma. Najua unamaanisha 1st year ni Technician Certificate, 2nd year ni Full Technician Certificate na 3rd year ndio Diploma. Ingawa kila mwaka ni exit, ila uwa tunasema tu Diploma. Pamoja man.
 
Ndugu yangu ni lazima apitie veta asugue miaka mitatu, apate cheti ndio aende huko asugue tena mitatu kupata diploma, ndio akasome hio digrii uliyomshauri
Aisee heri nifungue kaduka hata ka reja reja nitafute mia mia mbili, hii mpaka unafika hiyo degree ushaanza kuchungulia 25 - 30 ndio uanze kujitafuta na ajira tena una possibility ya kusugua miaka 3 - 5 benchi, hapo bado huna uhakika wa kutoboa miaka 50 au 45 minimum, bongo nyoso sana.
 
Back
Top Bottom