Natamani Misiba ya Wahaya iwe mingi kwani inatusaidia sana Kuimarisha Afya zetu kwa Vyakula na Kuoka Bajeti zetu za Kimaisha

Natamani Misiba ya Wahaya iwe mingi kwani inatusaidia sana Kuimarisha Afya zetu kwa Vyakula na Kuoka Bajeti zetu za Kimaisha

Nitaomba katika hilo hilo Gazeti unionyeshe hayo ' Matusi ' ili nami niyajue ila ninachojua tu ni kwamba neno Mjinga lipo mara 12 katika Kitabu Kitakatifu cha Biblia na neno Pumbavu / Mpumbavu lipo mara 24 katika Kitabu hicho hicho Kitakatifu cha Biblia hivyo kama maneno hayo mawili ambayo Mimi hupenda mno na sana kuyatumia ya Mjinga ( Ngumbaru ) na Mpumbavu ( Popoma ) ni ' Matusi ' basi nadhani hayo ' Matusi ' nitakuwa nimejifunza kwa Baba Muumba / Maulana / Mola / Mwenyezi Mungu mwenyewe.
Dah hahah!!!

Sawa mkuu yaishe.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Miaka ya 80 mpk 90+, alifariki mkulya mwenye title yake huko maeneo ya Masaki kama sio Mikocheni. Kulikuwa na vyakula vya kutosha na vinywaji (bia za hapo ilala TBL za chupa) kwa wingi.
Mara paap tajiri RUGEMARILA akatia timu pale msibani akaanza kupiga yowe! eti mama yangu weee hapa mahali sio salama, hawa jamaa watauana sasa hivi maana wakilewa wataanza kupigana na kuumizana kwa hizi chupa. Akatoa amri bia zote zilizopo pale zikusanywe na zipakiwe kwenye pickup. Baada ya kumaliza zoezi hilo, ikaingia canter imejaa bia za kopo za Heineken na amstell, watu wakanywa na kusaza.
Huo ndio utani wa wahaya na wakulya.
 
Na ndicho nakifanya Mkuu na huwezi amini naandika hapa lakini nipo katika Huzuni kubwa na Majonzi makubwa. Jembe la Uhakika limeondoka na sijui kama litatokea Jembe jingine kama Marehemu Ruge Mutahaba a.k.a Jasiri Muongoza Njia.
Mungu ni mwema hakika apendi tuwe na uzuni zaidi ya kumuomba na kuzidisha Sala... Atatupatia mwengine INSHALLAH.
 
Halafu kuna Mhaya mmoja Msibani alikuwa ananiangalia kwa umakini mno huku pia akiniogopa na mara kwa mara alikuwa akiniuliza nataka Kula au Kunywa nini. Sijui alinishtukia kuwa labda Mimi ndiyo ' Mtani ' wake / wao GENTAMYCINE. Jamani Wahaya chelewesheni ' Kumzika ' Ruge kwani huu Msiba unaokoa sana ' Bajeti ' zetu za Kimaisha hapa mjini.
Haa ha ha ha; kitu kimoja ambacho labda unisaidie we Mkurya, hivi swahiba wa Ruge si Mkurya/Mtani wa marehemu? Itabidi Wahaya wakae vizuri wasije wakadhurumiwa URITHI pale CMG, yule dogo aliyesoma historia ya baba yake sijui mama yake ni kabila gani aise?
 
Pumbavu ni wana Ukoo wako wote pamoja nawe. Wahaya ni Watani zetu wakubwa mno na hakuna Watu ninaowapenda kama Watani zangu Wahaya, Waha, Wanyiramba, Wanyaturu, Wakara na Warangi. Na isitoshe nimeleta hapa huu ' Uzi ' ukiwa ni Jukwaa la Utani. Halafu ni nani aliyekuambia kuwa katika Msiba Watu hawaruhusiwi Kutaniana? Hivi Wewe ' Takataka ' unajua dhana nzima ya ' Utani ' kuwepo katika Jamii ya Watanzania? au unadhani Mimi GENTAMYCINE sijaumia na siumii Kufariki Kwake Ruge Mutahaba?

Nakumbuka miaka ya 90 huko wakati wa Msiba wa Kaka yake Mwalimu Nyerere ( R.I.P ) pale Butiama ( waliokuwepo watanirekebisha ) Watani zetu hawa hawa Wahaya wakati Jeneza liko mbele walikuwa Wahaya fulani wawili wakawa wanalikalia huku wakilifanyia ' dhihaka ' za kila aina na wakisema kuwa Wazanaki na Mwalimu Nyerere tumemtoa ' Kafara ' Marehemu kisha wakasema Marehemu haendi Kuzikwa hadi kupatikane Pesa fulani na nakumbuka Hayati Mwalimu ilibidi pale pale awaite Wazee wa Kimila pamoja na hata Mzee Butiku ili Hela ya Watani ipatikane na wapewe na hilo lilifanyika haraka sana na wakapewa hizo Pesa na kuruhusu Marehemu akazikwe Mwitongo.

Ili uone kuwa Utani una Faida kubwa kuliko uwazavyo Mpumbavu Wewe ile Hela ambayo Watani zetu Wahaya waliiomba Sisi tulidhani labda wanataka tu kwenda ' Kuitumbua ' lakini huwezi amini Watani zetu hawa Wahaya ile Hela pamoja na zao ( walizochangishana ) wao kwa wao walienda Kununua Ng'ombe na Mahitaji mengine ya pale Msibani ndipo Sisi wengine ambao bado tulikuwa wadogo tukaujua umuhimu wa Utani hasa kwa Makabila ya Tanzania zaidi ya 120.

Siku zingine acha kuwa Mpumbavu tafadhali na hawa Watani zangu Wapendwa Wahaya, Waha, Wanyiramba, Wanyaturu, Wakara na Warangi nitaendelea ' Kuwatania ' hadi Siku ile na Mimi naingia Kaburini Kulazwa na bado nasisitiza hakuna Watu ninaowapenda na kuwaheshimu kama Watani zangu hao na ndiyo maana hata wakinisema ( wakinichana ) huwa nakuwa mpole kwani ni Wajomba na Shangazi zetu.

Pumbavu.
Una muda wa kuchezea we p.unguani , wosia unamuandikia Nani humu

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Wapare ni wachumi wa kuzaliwa lakini cha ajabu wanaweza practical tu theory inawatupa chini. Wangepasi theory hazina na benk kuu wangekua ni Mgonja, Mshana, Mziray....

Mzee Grey Mgonja alipotua hazina nae akakosea mahesabu.

😎
 
Huyu Ruge Pamoja Na Misifa ya Kabila lake nashangaa hakuwa Na Account rasmi ya jina lake Kwenye Mitandao ili kushindana followers

Nawaza Sifa Za Ruge angekuwa nazo Haji Manara Sijui Kama kungekalilka

Mtoto wa Prof Na Dkt

Kazaliwa mbele kabisa yaan Posta mpya ya US

Halafu kichwa kimejaa Madini

Mkwanja wa kutosha

Tungemkoma Yule Zeruzeru kwa nyodo
Hapo ndio inadhihilika kuwa tunawaonea wivu (Makabira 5) yanayoleta maana ya Wahaya.

Hawa watu sioni tatizo lao....

Kabira Mwanadamu.
 
Una ' Utani ' nao wa ' Kiasili ' kama Mimi au unawatafuta tu ' Ubaya ' Mkuu? Shauri yako na hapa JamiiForums wapo wengi tu hivyo ' utawakoma ' na anza Kujiandaa ' Kisaikolojia ' kwani najua hawatakuacha hivi hivi.

Eti Mexence natania? Wahaya wana uchoyo wa asili katika chakula, si utani.
 
Wapare ni wachumi wa kuzaliwa lakini cha ajabu wanaweza practical tu theory inawatupa chini. Wangepasi theory hazina na benk kuu wangekua ni Mgonja, Mshana, Mziray....


Yaani Mshana huyu huyu wetu wa JF ni mtaalam wa uchumi kweli au? Eti Mshana Jr wewe ni mwana uchumi au mchawi tu wa njia ya kidigitali?
 
Back
Top Bottom