Safi na hongera sana kwa uthubutu. Hujachelewa kabisa, fanya tathimini angalau ya siku tatu wahi mapema kabisa mida ya saa kumi pale mlango mmoja. Katika hizo siku tatu angalia vile wanafanya na utafute mwenyeji katika hizo mishe. Naimani katika hizo siku tatu utakuwa umepata kitu, hizo siku tatu usichukue mzigo we nenda kwa ajili ya kusoma namna wanavyo fanya na kupata uenyeji vizuri pia wadau kadhaa.
Baada ya hapo ingia mzigoni sasa, chukua bidhaa ambayo unaona inatoka kwa urahisi huko kitaa. Pita kitaa ukiuza viwalo vyako, usiogope unapo enda kwa mteja akagoma kununua ni sehemu ya mchezo husika. Muhimu we kaza tu, fanya kwa miezi mitano ndani ya mwaka huu naimani hiyo 100k itakuwa imezaa sana.
Sote kwa pamoja tukifika mwezi wa kumi panapo majaliwa nitafute nikupe heka tatu huko Mpanda-Katavi upige kilimo cha mahindi, utakuja kunishukuru. Maishani ni ukutane na watu sahihi tu, wengi tunafeli kwa kuwa na watu wasio sahihi.