Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Kilichotokea kipo kwenye mipango na wote wahusika wameshirikiana katika kutengeneza hili tukio, Simba na Yanga zinatumika na serikali katika kupumbaza watu, katika kupenyeza ajenda zao za kisiasa na katika kuwafanya watu wasahau kuhoji mambo ya msingi kama kuna matukio nyeti.
Kwanini nasema kimepangwa;
1) Simba na Yanga wamecheza mechi nyingi sana derby lakini hakuwahi kutokea huu utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa. Yanga anafanya mazoezi yake mwanzo mwisho kwenye kambi yake maalumu huku na wao Simba hufanya mazoezi yake katika kambi yake maalumu kisha watakutana uwanjani katika mechi husika. Imekuaje leo mambo yabadilike ghafla kwa Yanga na Simba kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja utakaotumika katika mechi?
2) Kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa jana kufanyika maridhiano kwa timu ya Simba kupewa ruhusa ya kuingia uwanjani kufanya mazoezi yao ya mwisho kwavile meneja wa uwanja alikuwepo hivyo ilikuwa ni swala la maridhiano kwa kuruhusu waingie ndani, hao wazee walioshukiwa ni waganga wangehamriwa wabakie nje kwasababu sio sehemu ya wahusika.
3) TFF wameonesha kuhairisha mechi sababu kuu ni uzembe wa watu kushindwa kutoa taarifa kwa meneja wa uwanja, maofisa wa mechi na timu mwenyewe kuwa watautumia uwanja kwa siku ya Ijumaa.
Hapa taasisi zote tatu zimeshiriki kuwachezea mashabiki na wapenzi wa mpira uhuni, Simba hawakuwa na sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi, baada ya Simba kuzuiwa haikiwa sababu ya wao kugomea mechi na TFF na bodi ya ligi nao walipaswa kuonesha nguvu zao kwa kusimamia kanuni na sheria kwa sababu zinazoweza kupelekea mechi kuhairishwa.
TFF na bodi ya ligi wamedhihirisha wazi zipo kwaajili ya manufaa ya Simba na Yanga na sio chombo kinachoweza kusimamia haki kwa timu zote na ndio maana tumeshuhudia Azam na timu zingine zikicheza mechi back to back mfululizo ila wao Simba na Yanga ni malaika wanapewa wiki nzima zijiandae na mechi.
Timu zingine zinachezeshwa mechi mchana wa jua kali kabisa ila Simba na Yanga timu ya mtaji wa serikali watayayuka kwenye jua kali wao wanachezeshwa jioni au usiku.
Hili tukio ingekuwa ni timu tofauti na Simba na Yanga tungeona vifungu vya sheria vikifanya kazi. Sio ajabu kuona hizi timu mbili zikibeba mabango, ziki print tisheti kwa ujumbe wa wana siasa wa chama kilicho madarakani ni kwavile ni mtaji wa serikali.
Simba, Yanga na TFF unaofanyia uhuni mpira wetu kwa mambo yenu ya kisiasa