Siku ya mchezo rais alikuwepo kule Arusha kwenye kilele cha siku ya mwanamke. Na kwa jinsi mambo yalivyo hadi sasa rais anapiga kampeni japo muda bado, hivyo anatumia sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya wananchi kujinadi na kutafuta kuungwa mkono.
Mechi ya YangaSC vs Simba ni mojawapo ya majukwaa atakayoyatumia kijitangaza kuelekea uchaguzi mkuu. Wewe ulitegemea mechi ichezwe akose kuhudhuria kama mgeni rasmi? Au unadhani washauri wake hawajui kwamba kwa namna yoyote ile mechi ingechezwa na kwa matokeo yoyote yale ni lazima yangefunika hotuba/ kampeni yake aliyohutubia Arusha?
TFF & bodi ya ligi, pamoja na SIMBA na Yanga walikuwa hawana namna ya kulazimisha mechi kichezwa kwani hawana huu ubavu kwa sababu wote wapo chini ya serikali kupitia wizara ya michezo iliyo chini ya rais.
TFF si chombo huru na hiyo ndiyo sababu ya mambo mengi yanafanyika yanafuata mlengo wa kisiasa na hata hao Yanga wanachokifanya ni funika kombe mwanaharamu apite.
Mechi ipo na mgeni rasmi atakuwa rais na ujumbe wake.