Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Siku za mwanzo mwanzo zitakua ngumu sana, utakosa usingizi, utaota ndoto za ajabu ila pambana humo humo, mimi nina zaidi ya miaka kumi tangu niache ulevi.
Mkuu usemayo ni kweli hata mi nishajaribu kuacha wiki ya kwanza nilikuwa nakesha usiku kucha usingizi nakuja kuupata saa 11 alfajiri, na nikipata usingizi ni full nightmare mwanzo mwisho mindoto ya ajabu haiishi, sometimes naota nipo chimbo ambazo Huwa na kunywa na washkaji tunapiga vyombo mara naota nimelewa mpaka nashindwa kutembea, Lakini nikijaribu kusema siku hiyo nishtue vyombo nalala kama mtoto na Wala sioti, mwisho wa siku kwenye hiyo acha na kurudia pombe nikajikuta nimeimaster hiyo hali nikaamua Toka moyoni nisinywe mwezi mzima nikaweza na baada ya hapo hata Ile kiu au hamu ya pombe Sina washkaji wanakunywa mi nawaangalia tu
 
Dawa yake inabid utengenezewe wewe Bila kuona inatiwa kwenye pombe na inabid iyandaliwe na mtu ambaye Ana roho ngumu maana ukishakunywa tuu pombe iliyowekwa dawa utatapika nusu kufa kila ukihisi harufu ya pombe utatapika sasa Hali hiyo itafanya kila ukiona mtu au pombe au harufu lazima utapike mzee utakuwa unakimbia vijiwe vya watu walevi,, Nina ndugu yangu sasa hivi Ana wiki hagusi pombe kbsaaa alikuwa analewa mpaka kujisaidia sasa hv yupo safiiiii kbsaaaaa yaaan akiona mtu amebeba bia kinacho muokoa ni mbio!
 
usikate tamaa kuna msaada ikiwa wewe mwenyewe una nia thabiti ya kuacha uraibu, tumepitia huko ila tunapambana na hatutaka tamaa msaada upo nitakushauri kama utapenda nitafute 0717551211 au 0767551211
 
Huwezi kuacha pombe kirahisi hivyo kama tayari umeshakuwa addicted,hapo inahitajika uamue kwa hiyari yako kumgeukia Mungu na kuacha maisha ya dhambi,kumbuka hiyo ni roho kabisa ya kishetani inayokutesa kwahiyo huwezi kuiondoa kwa nguvu zako mwenyewe kwakua mpango wa shetani ni kuua,kuiba na kuharibu...
 
Umeongea vema. Nami ninarudia,"HAJAAMUA".
 
Pole mkuu. Mimi nilikuwa na issue kama hiyo. Hebu Google 'how to quit alcohol timeline ' hii kitu kwangu binafsi ilinisaidia sana.
 
Bro labda unatumia Kvant, maana ile ni kifutio.

Anyway , pombe mbaya .

Ila mm kuacha bado aisee, ntapiga hivi vilite vyangu kadhaa huku napiga soga .
Kistaff kabisa.
Weekend ndio najiloweka. Weekdays bia zako 5-6 upate hamu ya kula usiku.
 
Mnakunywa vipi pombe mpaka hamjui ilikuaje? au kutapika ?

Tumieni kwa kiasi, maisha ni yako, mwili ni wako, fanya starehe kiasi.
Watu hawajua hata kunywa pombe vizuri unakuta mtu ndani ya dakika 10 kamaliza chupa ya bia , anaagiza nyungine πŸ€” wengi tu hawajui kunywa pombe kwa kustarehe mtu anagida ila alewe haraka bila kujua madhara ya unywaji wa pombe kwa mtindo huo
 
muangalieni afya,....wengi hukata tamaa wakishajua ni positive,...
 
Dr am 4 real PhD

Castle_Lite

Evelyn Salt

Huyu mwenetu eti anataka kuacha pombe 🀣 si bora aseme tu ameishiwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Anakunywa Kvant huyu. Lazima pombe aione mbaya. Ule mzinga ukiishusha mwenyewe inafuta kumbukumbuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Utaweza kusema unasave hela kumbe ukikolea ndio unatumia hela zaid maana una stimu za kiwaki , unaweza nunulia wahudumu bia na chakula na watu wengne hata huwajui.
+ asubuh unaamka mchovu hata kazin/dili zingne unanisikia uvivu wa kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…