GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wamiliki wa Daladala nchini Denmark wamebuni Mbinu mpya kwa Abiria ambao hawataki Kuoa kama GENTAMYCINE au Kuolewa kama wengine ili waweze kuwapata Wenza wao ndani ya hizo Daladala.
Ni kwamba sasa katika kila Daladala nchini Denmark huwa zinaachwa wazi Siti Mbili ambapo Yule Abiria ambaye anatafuta Mwenza wake hutakiwa Kukaa Kwanza katika Moja ya Siti hizo na Kutakiwa Kutabasamu muda wote bila Kuchoka kisha Abiria ambaye atavutiwa nae ( hasa na Tabasamu lake ) hilo atatakiwa Kukaa katika ile Siti nyingine na baada ya hapo harakati zao za Kutongozeka, Kuoana na Kubaiolojiana zitaanzia hapo.
Wasiwasi wangu GENTAMYCINE ni kwamba kuna Wengine Sura zetu zilivyo hata tujilazimishe vipi Kutabasamu bado tu tutaonekana tuna Usununu ( Tumenuna ) na huenda badala ya Kuwavutia Abiria ndiyo wanaweza ama wakatukimbia kabisa au kuomba hata Kushuka na wapande nyinginezo zenye Watu ( Wanaume ) wanaojua Kutabasamu Kimahaba.
Taarifa hii ya hili Tukio la Denmark nimelitoa Radio One katika 'Segment' yao nzuri ya Habari Nyepesi Nyepesi ya Leo Jumatatu Saa 2 Kamili iliyosomwa ( iliyoletwa ) na Mtangazaji Mtani wangu wa Kihaya ( Kagera ) Mkuu Deogratius Rweyunga ( Boss Deo )
Je, na Daladala zetu za Bongo ziwaige?