Nikola24
JF-Expert Member
- Aug 26, 2024
- 222
- 517
Habari yenu ndugu na jamaa zangu !
Kwanza ninge elezea kuwa hiki nilicho andika hapa sio hadithi ya kufikirika bali ni mambo halisi yaliyopo mitaani na kwenye yetu.
Kwanza nianze na historia Fupi ya maisha yangu shuleni.
Nisingependa kutaja jina langu ,ila kwa ufupi nilianza shule ya msingi ya msasani A iliyopo hapa dar.
Nilipata marafiki wengi shuleni na Mungu alinijalia uwezo wa kiakili darasani.
Katika mtihani wa taifa darasa la 7 nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kawe ukwamani secondary school.Pia rafiki yangu wa darasa la saba aliyeitwa MENGI FESTO alifaulu sio kivile ,ila alichaguliwa kwenda GOBA secondary school.
Nikiwa nasoma secondary, watu wa mtaani ,wanao jua na kuutumia sana ushirikina/uchawi wakaanza kunichezea bhana.
Nilipata ugonjwa wa masikio ghafla ,nikawa sisikii vizuri.
Baada ya wiki nikapigwa homa kali sana,tukaenda kwa mganga nikapona.
Mambo hayakuishia hapo Kuna kipindi nikiamka asubuhi kwenda shule ,naamka nikiwa nimechoka sana.
Watu fulani mitaani walikuwa wakiniangalia kwa jicho baya sana, sikutilia maanani.
Pia sikuwa najua chochote kuhusu teknolojia ya ushirikina.
Basi nikawa mdoli wa kuchezea ,Mara nachukiwa shuleni ,naadhibiwa bila sababu, kusinzia hovyo darasani, Kuna kipindi nilikuwa napoteza KumbuKumbu.
Kuna baadhi ya wanafunzi nilikuwa nakaa nao mtaa mmoja. Hao walikuwa ni washirikina pia. Hawa washenzi hawakuwa na akili sana ,ila waliishi kwa raha huku wakinipiga kijicho kisha wanapeleka ujasusi wao huko uchawini.
Kuna kiongozi wa dini , shekhe aliwahi kutuambia shuleni , HATA USOME VIPI KAMA HUJUI MANBO YA ULIMWENGU WA NGUVU ZA GIZA HUJAKAMILIKA.
Nilimdharau huyu shekhe ila leo ninaamini.
Mtaani niliona matangazo ya waganga.
*TUNA SAFISHA NYOTA
*TUNAONDOA NUKSI
*TUNATOA TIBA
*TUNAWEKA KINGA MWILI, BIASHARA,NYUMBA
Matangazo hayo niliyadharau pia.Niliamini mimi Nina akili sana.
Nilipofika form 4 nikafanya mtihani wa taifa mwaka 2014.Siku tunayo Fanya mtihani nilishuhudia mwanafunzi akichanganyikiwa kisha akatoka kwenye chumba Cha mtihani na kukimbia kurudi nyumbani kwao.
Naamini ni Shambulio la kishirikina.
Mimi pia machozi yalikuwa yakinitoka bila kujizuia.Sio kama nilikuwa nalia huku nafanya mtihani,hapana machozi yalikuwa yakinitoka tu kama maji.
Lakini nashukuru nilimaliza mtihani salama.
Matokea yalipotoka nilikuwa nimefaulu.Rafiki yangu MENGI FESTO wa GOBA alifeli .
Habari za kufaulu mtihani wangu zikasambaa mtaani kwetu.Aisee majimama na vibibi hivyi mnavyo vionea huruma, walikuwa na vijicho vya husuda sana.
Waliniangalia huku wakibinua midomo.
Nikaanza shule ya makongo high school,kule kawe jeshini.
Vijicho mtaani vikawa vikali zaidi .
Baada miezi mnne mambo yangu yalianza kuharibika.Nilipata ugonjwa wa miguu kufa ganzi,ute joints za mwili ukapungua nikawa siwezi kutembea .Hivyo sikuenda shule tena.
Siku zilikatika ,miezi ikapita na mwaka ukasonga ,maisha yangu yakawa kupambana na Hawa washenzi.Nimeshuhudia mauza uza mengi aisee.
Mpaka Leo hii ninapo andika haya napambana.Ndani nimeweka box la dawa asilia na nina vitabu vya tiba asilia.
Hapa nilipo mimi ni mgonjwa.
Karibia viungo vyangu vyote vya mwili vimerogwa.
Ubongo,ngozi,pua,macho,misuli,tumbo,damu,mifupa,nywele,joints , vyote hivi vimerogwa . Nina magonjwa yote hapo.
Pia nina jini mbaya mwilini,Nina nuksi kali na vifungo vya kichawi yaani nisipate mafanikio.
Nilienda kwa mwaposa lakini wapi hali iko palepale.Naendelea kupambana.
Wakati huu rafiki yangu MENGI,anaendelea kuishi kwa raha na mafanikio tele.Sio kwa sababu ana akili sana bali ni mwenye maarifa ya uchawi.
Natamani shuleni tungekuwa tunafundishwa kuhusu technology hii ya nguvu za Giza ,hakika mitaani wasingekuwa na uwezo wa kuharibu maisha yangu.
Naendelea kutafuta msaada nipate tiba. Shukrani!