Natamani watu kama Spika Tulia, Lissu, Shivji, Mwakyembe, Kabudi, Halima na Masereka waandae kongamano. Tuone jinsi Tulia atakavyowatoa jasho

Mi mwenyewe naitamani sana hii battle. Niliona Tulia alivombana Halima Mdee njia nyembamba siku ile bungeni Halima akaanza kuweweseka nikasema dah huyu Tulia anapaswa kuandaliwa battle na watu design ya uliowataja
Tukianza kuangalia nani ni nani wengine wamebobea katika sheria za mirathi ila hiyo haiwazuii kuwa vyema kwingine
 
Tuandae Mdahalo wa wanasheria nguli, wanaharakati, viongozi wa Serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wale wa dini, ili tukaujue ukweli wa mkataba huo upoje kati ya wanaounga mkono na wasiounga mkono, uwe wa wazi kitaifa na urushwe live na vyombo vyote vya habari.
 
Wenye serikali hawato kubali
 
Watanzania mnapenda sana maneno maneno kuliko kazi. Wenzenu wanatumia fursa kuongeza na kufanya uwekezaji nyie mnataka mijadala.

Ndo mana umaskini hauwezi kuwaacha
 
Aliyekuambia Kabudi ni mwalimu wa Shivji nani? Kinyume ndivyo ilivyo. Shivji alikuwa akifundisha UDSM wakati Kabudi anasoma hapo shahada yake ya kwanza.
 
Tulia anayetembelea PhD ya maandishi bila uzoefu ndo awatoe jasho magwiji. Hajawahi kusimamia kesi za kimataifa ndo asimame na Lisu, Rugemeleza, n.k?
Tulia akiwa Naibu AG ndiye aliokoa Mahakama kunyongwa na Mawakili wakali pale alipowapangua Mawakili hao kuhusiana na shauri la uchaguzi la kukaa mita 200 (viwanja 2 vya mpira) baada ya kupiga kura, nchi ikapumua. Ila kwenye hili la DP World nashuhudiwa kuwa Segerea panamhusu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Hata kuelewa mtu alichoandika huwezi....wapi nimemtaja Shivji?..
Au Shivji yupo kichwani mwako??...
Jihurumie wewe kwa ujuaji wa kipumbavu
Wewe ni zee la hovyo sana, unaefanya ujinga unaouonea aibu hata wewe mwenyewe, usijue kilicho ndani yako ulishakiandika, hata huoni wapi ulipomtaja Shivji!.

Tazama paragraph yako ya pili mwanzo kabisa, umemtaja mjomba wako?
 
Alafu matokeo ya huo mdahalo yataenda kufuta signatures za Samia na Mbarawa kwy mkataba ulioko Dubai? Matokeo ya mdahalo yatafuta Azimio la Bunge lililopitisha mkataba?

Mimi nilidhani ungesema tuanze kukarabati Gereza la Ukonga lenye ulinzi mkali kuwa na hadhi ya kutunza V.I.Ps.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mi mwenyewe naitamani sana hii battle. Niliona Tulia alivombana Halima Mdee njia nyembamba siku ile bungeni Halima akaanza kuweweseka nikasema dah huyu Tulia anapaswa kuandaliwa battle na watu design ya uliowataja
Kwani spika kazi yake ni kusimamia bunge au kubana hoja za wabunge? Ficha aibu ndogo ndogo unadharirisha ukoo wako
 
Shida ya Tanzania aliyekosea kufanya siasa kuwa chanzo cha kuchumi (kujipatia kipato), hivyo taifa limezalisha ugonjwa wa utegemezi wa siasa. mwanasiasa hawaheshimu taaluma za watu, hawaheshimu madaktari, hawaheshimu wanasheria, hawaheshimu walimu, ilmradi ukiwa mbuge, waziri mkuu, waziri, dc, rc, raisi wewe unajua kila kitu.

kwa mtu yeyeto mwenye uwelewa suala la mikataba ni swala la kisheria, la liko wazi, whether ni investment laws, or corporate law, criminal law or chochote lakini ni swala la kisheri.

kwa Tanzania huwezi kumzalau Prof. shivji, hata hao unao waona wanongelea sheria, wamepita mikononi mwake, na mwalimu akiona wanafunzi wanakengeuka kuweka mambo sawa ni safi, mpe heshima yake mzee kwa taaluma yake.

anasema kwa ajili ya nchi yake, na dhamira ya mkataba inasomwa kwenye mkataba, haielezwi majukwaani eti serikali ina nia nzuri, nia tuione kwenye mkataba, nyingine ni mbwembwe za majukwaani
 
Kwani haiwezekani mwalimu akawa kilaza lakini mwanafumzi akawa bright kumzidi mwl wake? Mbona walimu wengi Wana div three lakini wanaenda kufundisha bright and talented students mzumbe, kibaha na ilborou
 
GPA ya UDSM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…