Natamani watu kama Spika Tulia, Lissu, Shivji, Mwakyembe, Kabudi, Halima na Masereka waandae kongamano. Tuone jinsi Tulia atakavyowatoa jasho

Mi mwenyewe naitamani sana hii battle. Niliona Tulia alivombana Halima Mdee njia nyembamba siku ile bungeni Halima akaanza kuweweseka nikasema dah huyu Tulia anapaswa kuandaliwa battle na watu design ya uliowataja
Tulia anabebwa na nafasi yake tu, kwa shughuri zinazofanyika Bungeni, na yeye kuziongoza. Nje ya hapo, hana lolote.
Sina shaka wengi mnakumbuka ule MPAMBANO wa Tundu Lissu na Ndugai uliokuwa umeandaliwa na ITV na kuongozwa na Masako. Ndugai alizidiwa sana na Lissu, kiasi kwamba, kuna kipindi alikuwa anamlazimisha kunyamaza, mpaka Masako akawa anaingilia kumtuliza .Mwishoni Lissu akasema Ndugai, kazoea kuonea watu na amri zake,huko Bungeni, hivyo anafikiri hapa tupo Bungeni, anataka kuendeleza ubabe wake.
Na hao wanasheria waliopo Bungeni, au wapo nje lakini ni makada wa CCM, hawana budi kutetea huo mpango, kwani umeletwa na Chama chao, hata kama wanajua kuwa hauko sawa. Rejea yale makelele ya Mwita Waitara, kuwa, ambaye haungi mkono hana budi kujitoa CCM!
 
GPA Ni Nini mkuu. Maisha halisi hayahitaji first class ya cjui.

Tulia haiwezi bishana na shivji Bali anapaswa kumsikiliza. Hata km Ni Spika. Atasikiliza na kujifunza.
 
Hao wote ni wanasheria. Sasa sijui nani yuko sahihi. Ila ukizingatia Tulia ni Mwalimu wa lissu. Kabudi ni Mwalimu wa Shivji nk.

UMEKUNYWA KILEVI GANI? UKO SIRIAZI!
 
Labda iwe bungeni kwenye kiti chake. Lakini kwenye fare graundi hatoboi
 
GPA siyo kuwa bingwa. 4.9 anajiita Jalala
 
KUnawakati uwezo wa mtu haupimwi kwa matokeo ya mitihani, weka kivhwani hilo kunasiku litakusaidia
 
Tulia atatulia kimyaaaa kama mbwa aliyeona chatu
 
Mi mwenyewe naitamani sana hii battle. Niliona Tulia alivombana Halima Mdee njia nyembamba siku ile bungeni Halima akaanza kuweweseka nikasema dah huyu Tulia anapaswa kuandaliwa battle na watu design ya uliowataja

..Tulia alitumia zaidi rungu la Spika.

..Tulia hawezi kupambana na Mdee ktk mjadala wa wazi wenye usawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…