Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Tulia anabebwa na nafasi yake tu, kwa shughuri zinazofanyika Bungeni, na yeye kuziongoza. Nje ya hapo, hana lolote.Mi mwenyewe naitamani sana hii battle. Niliona Tulia alivombana Halima Mdee njia nyembamba siku ile bungeni Halima akaanza kuweweseka nikasema dah huyu Tulia anapaswa kuandaliwa battle na watu design ya uliowataja
Sina shaka wengi mnakumbuka ule MPAMBANO wa Tundu Lissu na Ndugai uliokuwa umeandaliwa na ITV na kuongozwa na Masako. Ndugai alizidiwa sana na Lissu, kiasi kwamba, kuna kipindi alikuwa anamlazimisha kunyamaza, mpaka Masako akawa anaingilia kumtuliza .Mwishoni Lissu akasema Ndugai, kazoea kuonea watu na amri zake,huko Bungeni, hivyo anafikiri hapa tupo Bungeni, anataka kuendeleza ubabe wake.
Na hao wanasheria waliopo Bungeni, au wapo nje lakini ni makada wa CCM, hawana budi kutetea huo mpango, kwani umeletwa na Chama chao, hata kama wanajua kuwa hauko sawa. Rejea yale makelele ya Mwita Waitara, kuwa, ambaye haungi mkono hana budi kujitoa CCM!