Natangaza rasmi dhamira ya kugombea Ubunge 2010

Natangaza rasmi dhamira ya kugombea Ubunge 2010

Hongera John !! Nakutakia kila la kheri na mafanikio lkn zingatia go to the people na uwe sehemu yao utafanikiwa
 
Mnyika you are honest. Hiyo peke yake inaweza kuwa credit kubwa itakayokufanya ushinde kwenye uchaguzi wa 2010. Wengi wanaotaka kugombea huwa wanasema nimetumwa na wazee na wazee wameniomba, uongo mtupu na wizi mtupu, at leat wewe unasema umeona haja ya kugombea na kuanisha sababu za kutaka kufanya hivyo. Ntakuwepo kwenye kampeni zako.
 
Kila la heri Mnyika,.. God of Isack will never let you alone....
 
Kazana bwana Mnyika jihadhari na watu kama GAME THEORY ambao wanahoji elimu yako kuwa una Zero. mtu wao Zitto kabwe ana elimu gani?

Some people do not know this Guy very well. He was one of the very talented and successful student in one of the best schools in tanzania. I happen to school for 3yrs with this guy, i know him well and therefore it is hard to doubt about his education.
 
Tuko pamoja.Nakutakia kila la heri Mkuu...Naamini this time unachukua jimbo..Je umelkabili vipi hili suala la uandikishaji daftari la kupiga kura?naona jamaa wameshaanza mbinu zao chafu.
 
Omba CCM wakuwekee mama Mwangunga pale. Utakuwa kama unasukuma mlevi! Na kama vijana niliowaona kwenye foleni za kuboresha daftari letu watajitokeza kupiga kura una nafasi kubwa zaidi. Naambiwa vijana hawa wanavitafuta vikadi vile ili viwe kama vitambulisho tu.
 
Ubungo kunatakiwa umakini katika ulinzi wa kura tu basi. Mna kura nyingi sana wekeni mpango madhubuti wa kuzilinda.
 
Mnyika,

1. Nini msimamo wako kuhusu Tanzania kuwemo kwenye EAC, na 'soko la pamoja'.

2. Pana udaku kwamba ulipewa 'michuzi/rujua/ulua/bakshish/takrima/kitu kidogo' ili matokeo ya uchaguzi wa mwaka ulee yaende kwa mpinzani wako, akikuahidi kwamba 'atakuachia na kukupigia debe' mwaka huu. Wasemaje?


Mlenge

Do I miss a reply on No 1? No 2 can be ignored.
 
Do I miss a reply on No 1? No 2 can be ignored.


Mlenge

Asante kwa swali lako la kutaka msimamo wangu kuhusu EAC na 'soko la pamoja'. Ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo hatua moja wapo ya juu ya kuwa na soko la pamoja kama dhana/nadharia ni nzuri kwa nchi ambazo zina fursa ya kutumia ushirikiano huo kuendeleza uchumi wa nchi husika na watu wake kupitia ushirikiano wao kwa kupanua masoko, mzunguko wa bidhaa, watu na hata kuunganisha mitaji.

Hata hivyo, EAC imeanzishwa, inaendeshwa na imepangwa kuendeshwa katika mfumo ambao hauelekei kuwa na tija ya kutosha kwa Tanzania, watu wake na hata EAC kwa ujumla wake (kama tukiitazama EAC kama mshindani katika soko la kimataifa) . Hii ni kutokana na udhaifu wa kidira, kimfumo, kitaasisi na kiuongozi. Hali hii ya muda mrefu imefanya watanzania wengi kuwa na mashaka ya wazi dhidi ya EAC na hata soko la pamoja.

Hivyo, kabla ya kukurupukia ushirikiano kuna hatua za msingi lazima kuzichukua kama taifa. Ni katika hali hiyo hiyo, ni muhimu kabla ya soko la pamoja kuanza hatua za msingi zikachukuliwa; ndio maana niliwahi kutoa tamko mwezi Januari kutaka tamko la serikali kuhusu suala husika; unaweza kurejea tamko hilo hapa: http://www.chadema.or.tz/habari/habari.php?id=108.

Katika hali hii tunahitaji kufanya mabadiliko ya uongozi na mfumo wa utawala ili Tanzania iwe kinara wa kiuchumi na hata kisiasa. Tukiendelea kwenda tunavyokwenda tunaweza tukapelekwa shimoni!

Hata hivyo, zingatia hapa nazungumzia ushirikiano wa kiuchumi; sijatoa msimamo wangu kuhusu ushirikiano wa kisiasa kuelekea shirikisho (EAF).

JJ
 
Asante Bwana Mnyika kwa majibu,

Je, nitakuwa nimekupata vizuri kwamba wewe unaunga mkono EAC ila hutaki EAF?

Mlenge
 
Back
Top Bottom