Natangaza rasmi kumuunga mkono Paul Makonda kuanzia sasa

Natangaza rasmi kumuunga mkono Paul Makonda kuanzia sasa

kichongeochuma

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2024
Posts
1,669
Reaction score
2,864
Mimi ni miongoni mwa watu ambao walimchukia sana makonda hasa enzi za mwenda zake , na hii ni kutokana na namna alivyo kuwa akiwatenda baadhi ya watu kwa jeuri na kibri kwa wakati huo.

Lakini sasa naamini kuna mambo aliyo yatenda wakati huo amesha yaombea toba kwa mungu ingawa sijajua kama kaomba toba pia kwa wale alio watendea hilo sina hakika nalo.

Lakini kwa sasa namuona makonda ni mtu mpya katika utekelezaji wake wa majukumu na hasa kwa kujali maslahi mapana ya wananchi wanao nyanyasika sana na watendaji wa serikali wasio waadilifu,wezi na mafisadi.

Huyu angetufaa kuwa Rais tena kwa nchi hii ilivyo jaa wahujumu uchumi, wezi na wanyanganyi, huyu angetufaa sana sana , nasisitiza ATATUFAA SANA ili aturudishe kwenye mstari mnyoofu na hii ni kutokana na uthubutu wake, kujiamini , na kusimamia kile alicho kiamini ni chema ,nankuwa na maamuzi, tunahitaji kiongozi mwenye maamuzi na si vinginevyo.

Ni hivyo tu.
 
Mkuu kichongeochuma , asante kwa kuliona hili leo jumhusu mtu huyu, angalia akina sisi tulianza nae wapi...
Mimi nilianza nae hapa Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni.

Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .

Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Na mwisho nikapendekeza Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM! Apunguze.

Ili kujua kama hiki ni chuma kile kile au ni chuma kipya karibu mitaa hii Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli

Ila pia kijana ni msikivu sana, alianza kwa moto sana, tukampooza Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka! sasa anakwenda vizuri!.

Hiki ni chuma Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?

P
 
Mimi ni miongoni mwa watu ambao walimchukia sana makonda hasa enzi za mwenda zake , na hii ni kutokana na namna alivyo kuwa akiwatenda baadhi ya watu kwa jeuri na kibri kwa wakati huo.
ili aturudishe kwenye mstari mnyoofu na hii ni kutokana na uthubutu wake, kujiamini , na kusimamia kile alicho kiamini ni chema ,nankuwa na maamuzi, tunahitaji kiongozi mwenye maamuzi na si vinginevyo.

Ni hivyo tu.
Shida kubwa, wengi wetu hatujui tukitakacho kama NCHI.
Alikuwepo 'JIWE' alifanya kazi kwerikweri na watu walimpiga spana mno.
Now, amekuja 'MAMA' bado tunalalamika. Sasa tunataka tuongozwe na mtu wa namna gani?!
 
Back
Top Bottom