Natarajia kufungua kufungua kesi mahakamani nimshtaki mkuu wa mkoa kwa uonevu dhidi yangu

ZOPPA

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
2,729
Reaction score
2,891
Husika na kichwa cha habari wana jf

Mimi ni kijana mwenzenu ninae tafuta hela kwa hali na mali, mwaka 2013 nilifanikiwa kununua eneo lenye ukubwa hekari 25 wilaya ya Mvomoro kata ya Kimambira kijiji menge mwaka 2016 eneo hili nikawa nalima matikiti na nyanya nikawa najipatia mapato maisha yanaenda, nahudumia familia na kusomesha. 2019 kukatokea migogo baina ya wakulima na wafugaji nikaona isiwe shida nikaamua kubadilisha matumizi nikatengeneza mizinga nikawa nafuga nyuki, nikawa navuna asali maisha yakawa yanaenda.

Sasa kukaibuka mgogoro baina ya wanakijiji na wenye mashamba ndipo ikafikia hatua ya kumuita mkuu wa mkoa mwezi huu 13, 21 alikuja katika kijiji akatoa tamko wenye mashamba kuanzia heka kumi wapokonywe wapewe raia pasipo kuwa na utaratibu wakaaribu miundombinu ya ufugaji wa nyuki, wakanipa hasara kubwa sana nimepoteza ardhi.

Je nikitaka nimshtaki huyu muheshimiwa nitakua nimekosea! Je pia taratibu zipoje?

MSAADA
Ushauri pia unahitajika
 
Punguza hasira andika ueleweke, Kimambira haijawahi kuwa na matatizo kama unayoyaongelea.

Najua kuna watu walijiongezea kinyemela au maeneo kwa sababu zamani walikuwa wanaambiwa tu heka 10 kutokea mti ule mpaka kibwawa kile hadi mwanzo ule wa barabara. Au kwa sababu ya uwepo wa mapori watu walivamia.

Kwanza unalimaje Kimambira, wanakijiji wanaingia ndani saa 1 usiku, wanatoka saa 1 asubuhi amri ya kiusalama ya serikali, tembo wanaingia saa 1 usiku hadi saa 1 asubuhi. Tembo anavuruga kila kitu mpaka alizeti anakula masinia.

Kamshitaki sijui wapi mahakama ya ardhi au baraza la ardhi kata??

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Soma bandiko vizuri kata ya kimambira kijiji cha menge au vianzi
 
tafuta mwanasheria Akueleze hatua za kufata maana kuishtaki serikali ni tofauti na Kumshtaki mtu mwingine...

Inshort inabid utoe notice ya siku 90 kwa mkuu wa mkoa kama unataka kuipeleka serikali yake mahakaman kama sijakosea...
 
Pole sana mwekezaji mzawa kwa hiyo changamoto iliyokupata. Nchi yetu inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria.

Kama unahisi umeonewa, mtafute mwanasheria then kaa nae chini ili akusaidie namna ya kudai haki yako. Ikibidi huyo mkuu wa mkoa awajibike kukulipa fidia kwa kutumia hela zake za mfukoni! Iwapo tu alikurupuka.
 
Husika na kichwa cha habari wana jf

Mimi ni kijana mwenzenu ninae tafuta hela kwa hali na mali, mwaka 2013 nilifanikiwa kununua eneo lenye ukubwa hekari 25 wilaya ya Mvomoro kata ya Kimambira kijiji menge mwaka 2016 eneo hili nikawa nalima matikiti na nyanya nikawa najipatia mapato maisha yanaenda, nahudumia familia na kusomesha. 2019 kukatokea migogo baina ya wakulima na wafugaji nikaona isiwe shida nikaamua kubadilisha matumizi nikatengeneza mizinga nikawa nafuga nyuki, nikawa navuna asali maisha yakawa yanaenda.

Sasa kukaibuka mgogoro baina ya wanakijiji na wenye mashamba ndipo ikafikia hatua ya kumuita mkuu wa mkoa mwezi huu 13, 21 alikuja katika kijiji akatoa tamko wenye mashamba kuanzia heka kumi wapokonywe wapewe raia pasipo kuwa na utaratibu wakaaribu miundombinu ya ufugaji wa nyuki, wakanipa hasara kubwa sana nimepoteza ardhi.

Je nikitaka nimshtaki huyu muheshimiwa nitakua nimekosea! Je pia taratibu zipoje?

MSAADA
Ushauri pia unahitajika
Unaye mwanasheria au unataka mwanasheria wa kujitolea?
 
Ulifuata sheria zote kupata hiyo ardhi? Ilikuwa ya kijiji au ya mtu binafsi? Pitia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 uone kama utatoboa. Ila RC anashtakiwa vizuri tu.
 
Soma bandiko vizuri kata ya kimambira kijiji cha menge au vianzi
Ulinunua kwa mwanakijiji au tokea serikali ya kijiji??
Naifahamu na changamoto zake, sasa unamshtaki Mmaasai au serikali??
Au unawashtaki waliokuharibia miundo mbinu, ila kama unajiamini kabisa 100%, kwamba makaratasi yako nyaraka zipo sahihi, uliuziwa kwa kikao cha kijiji na siyo FOJARI ya muhtasari basi nenda mahakamani kuishtaki Jamhuri.
Kimambira tetesi ni wengi waliuziwa kwa FOJARI za mihutasari, na walijua na waliridhia hiyo janja janja. Majina tu ya wajumbe na sahihi bila mkutano halisi. Wakalipa chini ya laki 3 sijui wakapewa maeneo.

Kama unajiamini, ulihudhuria mkutano wa kijiji wa kukujadili wakati wa maombi yako kupewa ardhi, basi kaishtaki serikali, ila kama hukuwahi kushiriki, ndugu achana na hizo hasira, zitakuletea hasara.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Dili na waliopo kwenye hiyo ardhi na ealioharibu achana na mkuu wa mkoa huyo atakuja kuwa shahidi tu mahakami kwa lazima
 
tafuta mwanasheria Akueleze hatua za kufata maana kuishtaki serikali ni tofauti na Kumshtaki mtu mwingine...

Inshort inabid utoe notice ya siku 90 kwa mkuu wa mkoa kama unataka kuipeleka serikali yake mahakaman kama sijakosea...
Hiyo ya kutoa notosi ilishafutwa mzee unapeleka mahakamani tu fasta.
 
Husika na kichwa cha habari wana jf

Mimi ni kijana mwenzenu ninae tafuta hela kwa hali na mali, mwaka 2013 nilifanikiwa kununua eneo lenye ukubwa hekari 25 wilaya ya Mvomoro kata ya Kimambira kijiji menge mwaka 2016 eneo hili nikawa nalima matikiti na nyanya nikawa najipatia mapato maisha yanaenda, nahudumia familia na kusomesha. 2019 kukatokea migogo baina ya wakulima na wafugaji nikaona isiwe shida nikaamua kubadilisha matumizi nikatengeneza mizinga nikawa nafuga nyuki, nikawa navuna asali maisha yakawa yanaenda.

Sasa kukaibuka mgogoro baina ya wanakijiji na wenye mashamba ndipo ikafikia hatua ya kumuita mkuu wa mkoa mwezi huu 13, 21 alikuja katika kijiji akatoa tamko wenye mashamba kuanzia heka kumi wapokonywe wapewe raia pasipo kuwa na utaratibu wakaaribu miundombinu ya ufugaji wa nyuki, wakanipa hasara kubwa sana nimepoteza ardhi.

Je nikitaka nimshtaki huyu muheshimiwa nitakua nimekosea! Je pia taratibu zipoje?

MSAADA
Ushauri pia unahitajika
Kwanini usimroge tu ?
 
Pole sana mwekezaji mzawa kwa hiyo changamoto iliyokupata. Nchi yetu inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria.

Kama unahisi umeonewa, mtafute mwanasheria then kaa nae chini ili akusaidie namna ya kudai haki yako. Ikibidi huyo mkuu wa mkoa awajibike kukulipa fidia kwa kutumia hela zake za mfukoni! Iwapo tu alikurupuka.
nashukuru kwa hilo ipo hivi nimefuata talatibu zote shamba nimeuziwa na selikali ya kijiji
 
Back
Top Bottom