Uchaguzi 2020 Nategemea kumuona Tundu Lissu akitufafanulia ilani ya CHADEMA badala ya kulalamika lalamika wakati wa kampeni!

Uchaguzi 2020 Nategemea kumuona Tundu Lissu akitufafanulia ilani ya CHADEMA badala ya kulalamika lalamika wakati wa kampeni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
CCM imefanya mambo makubwa ndani ya hii miaka 5 ya Rais Magufuli na hili wananchi wote wanalijua.

Tundu Lissu amekuwa ni mtu wa kulalamika na kushutumu huku akipinga kila jambo litendwalo na CCM. Nampa tu angalizo kuwa urais wa JMT siyo sawa na ule wa TLS, watanzania watataka kusikia malengo yake na siyo malalamishi yake.

Tupingane kwa hoja na data na tusionyeshane ubingwa wa kutema povu, maana Lissu povu ndio zake.

Nawatakia kila la kheri, tukutane kwenye kampeni.

Maendeleo hayana vyama!

cc: Daudi Mchambuzi Pascal Mayalla na mmawia & mrangi
 
Wananchi gani wanayajua hayo mambo makubwa? Wafanyabiashara? Wafanyakazi? Wahitimu wa vyuo? Wakulima au kina nani?

Acha uoga wewe
 
Ana cha kuongea sasa hapo ukute hata ilani ya chama haijui anachojua yeye ni kutukana nchi yake na viongozi basi huyu na alaaniwe.
 
... ni katika kampeni hizi zijazo Ilani ya chama cha siasa itafafanuliwa kwa ufasaha kuliko kipindi kingine chochote cha uwepo wa taifa hili. Ni ufafanuzi ambao hata mwendawazimu barabarani atauelewa sema hamkawii kusema mmetukanwa kisa hofu na kiwewe kisicho na mashiko! Ha haha!
 
Wakati wa kampeni za Magufuli tulisikia Million 50 kila kijiji, Laptop kwa kila mwalimu ..... hatukusikia kuhamia Dodoma, SGR wala Stiegler gorge. Hizo ndizo kampeni za Africa .... zinaendana na mood ya watu!!
 
Mambo makubwa yamefanywa mikoa mitatu kati ya 25 iliyopo so maendeleo ya jiwe yamekuwa ya kikanda zaidi na mikoa michache imenufaika huku mingi tukiambulia zii so jamaa ajipange watz tumeamua kwenda na lissu
 
Mimi ni mkazi wa shinyanga vijijini naomba nitajiwe mambo mawili makubwa aliyofanya jiwe ktk huu mkoa
... Mkuu REA haijapita pande hizo? Ule mradi wa maji L. Victoria tunaogombana na wamisri?
 
Hata wakazi wa mikoa jirani nao wanaomba watajiwe mambo makubwa mawili tu aliyofanya jiwe, mikoa yenyewe ni simiyu, tabora, kigoma na mwanza
 
Mambo makubwa yamefanywa mikoa mitatu kati ya 25 iliyopo so maendeleo ya jiwe yamekuwa ya kikanda zaidi na mikoa michache imenufaika huku mingi tukiambulia zii so jamaa ajipange watz tumeamua kwenda na lissu
Sema wewe sio watz wote
 
... Mkuu REA haijapita pande hizo? Ule mradi wa maji L. Victoria tunaogombana na wamisri?
hayo yote yalifanywa na kikwete tangia jamaa aingie hakuna kipya kikubwa kilichofanya aiseee!
 
Ila kama ni mimba bora huitoe, sijui kama utafika 28/10/2020, unaangaika sana.
 
johnthebaptist ,

..kilichonishangaza mimi ni watia nia kugombea ubunge kupitia CCM kutaja changamoto na mapungufu, badala ya kuisifia serikali kwa mambo makubwa iliyoyafanya.

..kazi ya mwanasiasa wa upinzani ni kuzitambua changamoto ambazo utawala uliopo umeshindwa kuzitatua na kuwashawishi wapiga kura kuwa mabadiliko ya utawala yataleta ufumbuzi wa changamoto hizo.

..hebu msikilize mmoja wa watia nia wa ccm hapa:
 
Back
Top Bottom