Nateseka Kimeo kimerefuka sana

tembocard

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
247
Reaction score
121
Habari zenu wapendwa naombeni msaada nina tatizo kimeo kimerefuka sana mpaka kinagusa ulimi wakati mwingine naskia kinaninyoka kooni sasa sielewi nifanyaje maana wako wanaoniambia nikakate wengine wananiambia usikate hairusiwi sasa sielewi kipi ni sahihi naombeni mchango wenu wa mawazo juu ya hili tatizo
 
Wataalamu wa kukuata wapo.
Nipo kibondo nipo tayari kukupa msaada wa kukutafutia mtaalam wa kukikata.
Pole sana
 
Au acha nikupe ilimu kidogo

Kimeo au( Palatine Uvula or simply Uvula kwa kitaalamu)
mtu huzaliwa nacho huku pakiwa hakuna ulazima wa kukikata kama hakuna sababu maalumu ya kitabibu!!

jamii nyingi zimekua na tabia ya kuwakata watoto wakiwa wadogo kienyeji mwishowe kuishi kupoteza damu (severe anemia) mtoto anakua katika hali ya hatari(heamorrhagic schock) hata wakati mwingine kupoteza maisha kwa uzembe wa wazazi ivyo basi elimu hutolewa kwa wazazi wawepeleke watoto hospitali na kama kutatokea ulazima sababu za kitabibu basi watakatwa bure..

sasa dalili za kitabibu zinazoweza kupelekea mtu kukatwa kimeo ni
/ kushindwa kupumua( air way obstruction)
2/kushindwa kula vizuri( obstructed feeding)
3/ kushindwa kuongea vizuri
4/ kukoroma ambapo hupelekea mtu kushindwa kuvuta hewa ( snoring and sleep apnea)
5/maambukizi katika kimeo ( infection)

Operation iyo (surgical procedure) hufanyika ambayo kitalaam tunaiita (Uvulectomy ) ikiwa na maana kuondoa kimeo (removal of uvula) ivyo basi hospitalini hufanyika na ni procedure ndogo ( minor surgery) ivyo huwa na matokeo chanya mda wote..

sasa tukija katika swala lako umesema kimerefuka sana mpaka kinafika kwenye ulimi na kama kinaleta usumbufu!!

Kwangu nitakupa ushauri mzuri personally maana siwezi toa tiba hapa maana sijakuona sijaona kina urefu gani maana inabidi tufanye kitu kinaitwa ( E.N.T) examination ili tuscore chance za kukuiondoa pale tutakapo jiridhisha by the way (E.N.T) exam..ni ukaguzi wa Sikio(E!ar),,Pua(N!ose) na Koo(T!hroat)..

sasa nenda hosptal ya karibu watakagua na kama kutakua kuna sababu ya kitabibu then watakueleza maana wao watakua wameshakuona physically na pia washafanya ukaguzi(examination) then kama kutakua nasababu ya kitabibu kitaondelewa na operation ya mda mchache wale usiwe na hofu... inafanywa kwa msaada wa ganzi,, then kinaondolewa..utapewa dawa za kukausha kidonda na kuua wadudu ili kuepuka maambukizi(antbiotics) thn kama utakua na maendeleo mazuri unaruhusiwa.

wala usiendelee kuteseka (uncomfortability) wahi hosptal mapema mkuu utakua sawa

 
Asante sana my nmekuelewa, naomba nikuulize kwenye kukata kwani una pasuliwa kwa nje au kinakatwa ndani kwa ndani maana mm kinaburuza kwenye ulimi na ninakooa sana kikinigusa
 
Asante sana my nmekuelewa, naomba nikuulize kwenye kukata kwani una pasuliwa kwa nje au kinakatwa ndani kwa ndani maana mm kinaburuza kwenye ulimi na ninakooa sana kikinigusa
hahah mkuu usiogope haha hakuna kupasuliwa kwa nje ni ndani kwa ndani mdomo utatanuliwa then utapatiwa dawa ya ganzi au usingizi then kitakatwa ndani kwa ndani kitatolewa then utakua unatumia dawa za maumivu(ant pain) na za kuzuia wadudu na kukausha( antibiotics) baasi wataangalia mwenendo wako (daily vital monitoring) ukiwa sawa stable wanakurusu(discharge) wala usihofu
 
Nenda hospitali mkuu ukapate ushauri wa daktari. Ila mimi nimeshuhudia watu wengi sana wakikata na hata ktk familia yangu na maisha yakasonga vizuri kbs.
 
Fanya ukate kwa sisi tamaduni zetu mtoto anakatwa wakati akiwa mdogo hasa pale anaposumbuliwa n kikohozi
 
ni kweli wataalamu wa afya wana sababu za msingi kabisa kusema kisikatwe, ila ni kwa vile mtu hayajakukuta, kikikua kinaboa sana, bota kukata.
Shuhuda ni mi mwenyewe, pamoja na ubishi wangu na kusoma mwisho wa siku nilivyooha mikono, kikakatwa, saizi niko freeesh
 
Leo mke wangu pia amekata baada ya kuambiwa kimekua kirefu na kugusa ulimi amekua akikooa,kula ni tatizo na muda mwingine pumzi kukata anashindwa pumua vyema na mushukuru Mungu maana zoezi limefanyika ndani ya dakika 1 tu mzee wa watu akawa amemaliza kazi yake tena bure kabisa Mungu amusimamie katika kazi zake ni mikasi miwili mmoja wa kukashikia mwingine wa kutia bila ganzi mzee kiboko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulipata matibabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…