Au acha nikupe ilimu kidogo
Kimeo au( Palatine Uvula or simply Uvula kwa kitaalamu)
mtu huzaliwa nacho huku pakiwa hakuna ulazima wa kukikata kama hakuna sababu maalumu ya kitabibu!!
jamii nyingi zimekua na tabia ya kuwakata watoto wakiwa wadogo kienyeji mwishowe kuishi kupoteza damu (severe anemia) mtoto anakua katika hali ya hatari(heamorrhagic schock) hata wakati mwingine kupoteza maisha kwa uzembe wa wazazi ivyo basi elimu hutolewa kwa wazazi wawepeleke watoto hospitali na kama kutatokea ulazima sababu za kitabibu basi watakatwa bure..
sasa dalili za kitabibu zinazoweza kupelekea mtu kukatwa kimeo ni
/ kushindwa kupumua( air way obstruction)
2/kushindwa kula vizuri( obstructed feeding)
3/ kushindwa kuongea vizuri
4/ kukoroma ambapo hupelekea mtu kushindwa kuvuta hewa ( snoring and sleep apnea)
5/maambukizi katika kimeo ( infection)
Operation iyo (surgical procedure) hufanyika ambayo kitalaam tunaiita (Uvulectomy ) ikiwa na maana kuondoa kimeo (removal of uvula) ivyo basi hospitalini hufanyika na ni procedure ndogo ( minor surgery) ivyo huwa na matokeo chanya mda wote..
sasa tukija katika swala lako umesema kimerefuka sana mpaka kinafika kwenye ulimi na kama kinaleta usumbufu!!
Kwangu nitakupa ushauri mzuri personally maana siwezi toa tiba hapa maana sijakuona sijaona kina urefu gani maana inabidi tufanye kitu kinaitwa ( E.N.T) examination ili tuscore chance za kukuiondoa pale tutakapo jiridhisha by the way (E.N.T) exam..ni ukaguzi wa Sikio(E!ar),,Pua(N!ose) na Koo(T!hroat)..
sasa nenda hosptal ya karibu watakagua na kama kutakua kuna sababu ya kitabibu then watakueleza maana wao watakua wameshakuona physically na pia washafanya ukaguzi(examination) then kama kutakua nasababu ya kitabibu kitaondelewa na operation ya mda mchache wale usiwe na hofu... inafanywa kwa msaada wa ganzi,, then kinaondolewa..utapewa dawa za kukausha kidonda na kuua wadudu ili kuepuka maambukizi(antbiotics) thn kama utakua na maendeleo mazuri unaruhusiwa.
wala usiendelee kuteseka (uncomfortability) wahi hosptal mapema mkuu utakua sawa
Habari zenu wapendwa naombeni msaada nina tatizo kimeo kimerefuka sana mpaka kinagusa ulimi wakati mwingine naskia kinaninyoka kooni sasa sielewi nifanyaje maana wako wanaoniambia nikakate wengine wananiambia usikate hairusiwi sasa sielewi kipi ni sahihi naombeni mchango wenu wa mawazo juu ya hili tatizo