Nateswa sana na jini mahaba

Nateswa sana na jini mahaba

PierreLiquid

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2019
Posts
596
Reaction score
2,298
Habari za muda huu ndugu zangu.

Mimi ni kijana Me 26 nimekulia maisha yenye furaha sana mpaka nilipofikia umri wa miaka 24 na kugundua mwili wangu haupo sawa. Yani nasumbuliwa na kiumbe aitwa jini mahaba apo awali nilikuwa nahisi furaha kupata ndoto ya jima na mwanamke ila hasara za huyu kiumbe nimeziona nilipoingia kwenye mahusiano na binti mcha mungu sana.

Ni miaka miwili sasa nateseka kwa aliewahi kupata tatizo langu ni rahisi kunielewa. Nimezungu kwa waganga wa jadi wengi sana wenye uweledi ila nimekuwa nikilitatua tatizo langu kwa kipindi kifupi na kurudi. Tokea nimemtambua uyu kiumbe na kuanza vita nae amezidi kuniandama na kufunga mpaka riziki zangu. Nimefukuzwa kazi, nakataliwa na watu, nadhulumiwa kwenye jasho langu nimekuwa mtu wa kulia sana na kuomba lakini wapi.

Sifahamu ametokea wapi au ametumwa na nani? Ngoja niwaelezee kidogo kuhusu uyu kiumbe na mateso yake kwangu...Uyu kiumbe sio kama mashwetani wa kawaida ukisema akiitwa atazungumza na kueleza dhamira yake. uyu kiumbe anapoona kuna makali ya kumuumiza mfano maombi au dua hutoka na kuondoka na baada ya dawa kuisha hurudi hiyo ndio sababu kubwa ya kushindikana kuondoka kwa huyu kiumbe.

Baada ya kufuatilia mlolongo wa maisha yangu ya nyuma baada ya kutambua nina kiumbe huyu ndani mwangu nimegundua, mwanamke hunipenda ila mimi sitompenda nitamtumia na mwishowe nitamuachia huzuni ya kumuacha, kosa kubwa ni mimi nikimpenda mwanamke zitafanyika hila zozote za kunifanya nishindwane na huyo mwanamke, mfano nitashindwa kumuingilia uyo mwanamke kila nikitaka kufanya hivyo uume hutoweza kufanya lolote ila nikienda kwa mwanamke mwingine naweza niliwahi kuambiwa ni kwamba anapata wivu ndio sababu ya kuniharibia "nimewapoteza bila sababu wengi sana niliokuwa nawapenda nimeumia sana" nipo na mwanamke mcha mungu amekuwa akiniombea na ni strong nadhan ndio moja ya sababu kumshindwa kiumbe huyu

Nimemuingiza katika vita sababu ya upendo wake anapambana sana na mimi katika vita hii, anapata mandoto usiku ya kumtisha anaona wanawake wanamjia na kumwambia umeamua kumfanya unavyotaka sio, baada ya kuwa natumia gharama nyingi kwa waganga kwa ajili ya tatizo langu aliamua kufunga riziki zangu nisipate hata 100 ili nisiweze kufanya jitihada zozote za kumuondoa. Nimeachishwa kazi bila sababu. Apa nilipo sina hata senti.

Vihoja vya mateso kwenye maisha yangu ni vingi sana hata kukumbuka nashindwa nimekuwa kwenye kifungo kikubwa sana nimeenda madhabau mengi na tofauti kanisani, kwa mashekh, kwa waganga ila sijapata auheni zaidi ya uyu kiumbe kuzidi kunipatia mateso. Hivi ninanyoandika nimechoka na kuishi kwa sasa ni mwanamke wangu ambae sina imani katika safari yangu kama nitafika nae.

Nateseka nateseka haswa. Siku uyu binadamu wa karibu yangu pekee atakapo kata tamaa na mimi basi na mimi sitokuwa na budi kuiacha dunia na kupata pumziko la milele, sioni faida ya kuishi apa nilipo nmeuza mali zangu nyingi nilizokuwa nazo ila napota ela bila kujua kufahamu. huu ni moja ya mfano mmoja kati ya mingi ya ajabu iliyonikumba niliwahii kuchukua simu ya mtu nimelekee mteja ili niipaate elf20 ya udalal ila nilienda kushikwa na kuambiwa nimeiiba ile simu na kuwekwa ndani ila baada ya siku2 iligundulika ile simu sio ya wizi imefananishwa nikaachiwa, niliwahi kuitwa interview nilizunguka saa nzima naupita mlango wa chumba cha inteview mpak mda ukaisha.

Katika ndoto usiku naambiwa nawaona wanawake wananiambia wewe si mbishi tutakuonyesha. Nimechoka nahitaji msaada kwa njia yoyote ile inatosha naitaka amani, kuna wakati nalia sana usiku nakuomba...Mwili wangu ni wa nyama vita yang ni ya kiroho Mungu wangu ameniacha. Kuna wakati nawaangalia watu fulani na kutamani kuwa wao na kujiona mimi ni mkosi...Maisha yangu ni ya kulia tuu barabarani, nyumbani, kanisani.

Ewe binadamu unaefahamu msaada wa tatizo langu naomba unisaidie kutoka kufungoni Kwa namna yoyote. Na mungu atakubariki sana.

Asante sana
 
ENDELEA KUMWOMBA MUNGU TU, NO WAY OUT .../
USISAHAU KUTOA SADAKA ../
NA PIA ONDOA HOFU KWAKUWA SHETANI HUPENDA KUWAINGIA WALE WENYE HOFU NA WASIWASI.../
NA KUMBUKA KUWA MUNGU HAWEZI KUMTUPA MJA WAKE [emoji120][emoji123]

[emoji117]KUWA NA AMANI KILA KITU KITAKUWA SAWA[emoji120]
 
Kwanin unaimani za hovyo namna hio mkuu...

Mimi naishi nikiamin..

No shetan
No majin
Nikifeli lazima nijue tatizo na Mara nyingi inakuwa kutokuwa makini..

Kukataliwa na watu I don't care kwan huwez pendwa na kila MTU hapa duniani ..

Acha kuwa na mawazo ya kigiza giza
 
Sasa mkuu mbona njia tayari umeshaipata.

Komaa na mwanamke wako kwenye maombi,na wewe mwenyewe go deeper kwe nye kusali.

Halafu hilo dude lidharau tu,litaondoka.fanya hata kila siku jioni au asubuhi mnapiga maombi.
 
Kwanza nakuona una udhaifu na unalipenda hilo dubwana, pili sijui ni Mungu yupi unaye kwenda kuongea naye kwa kipindi chote hiko.

Yaani kwa Mungu sijui nini kinashindikana ndiyo maana ukiwa kwenye maombi ya nguvu linasepa na kukaa nje likisubiri umalize lije tena.

Nakushauli piga mfungo wa mlimani kwa siku saba ukiwa unakunywa maji tu baada ya hapo njoo utoe ushuhuda.
 
Mungu wetu ni Mungu wa hajabu.

Mfalme Selemani anasema “ usiyachochee mapenzi, yaacha mapenzi yaamuwe yenyewe “. Tatizo lako lilianza pale ulipo Barehe . Vijana wengi wanapo Barehe wanaanza kufanya mapenzi kwenye hisia na mawazo tatizo linaanzia hapa kwa sababu wanaanza kuchochea mapenzi.

Tatizo uliokuwa nalo siyo Jini Mahaba. Kuna Kitu kinaitwa msingi wa uumbaji, unapokwenda tofauti Na huu msingi kuna vitu vitakutokea.
Utamaliza kwa mashehe, makanisani, kwa waganga wa kienyeji tatizo bado lipo pale pale badala yake wanakujaza mapepo wengine.

Usiende kanisani kwa lengo la kuombewa nenda kanisan kwanza upate kumjuwa Yesu Na kumfahamu uponyaji utaanza.

Unapomuona mwanamke yeyote usipeleke mawazo kwenye Ngono.
 
Nimezunguka katika madhabahu za kiganga tofauti na jibu ni hilo hilo, ata kanisani nikiombewa mtumishi akitaja neno mahaba jini katika maombi mwili lazma utetemeke kama hali ya kupatwa na ubaridi
Sijaona sehemu uliyoeleza viashiria vya kujua kwamba una jini mahaba. Uligunduaje au uliambiwa na nani?
 
Amen
ENDELEA KUMWOMBA MUNGU TU, NO WAY OUT .../
USISAHAU KUTOA SADAKA ../
NA PIA ONDOA HOFU KWAKUWA SHETANI HUPENDA KUWAINGIA WALE WENYE HOFU NA WASIWASI.../
NA KUMBUKA KUWA MUNGU HAWEZI KUMTUPA MJA WAKE [emoji120][emoji123]

[emoji117]KUWA NA AMANI KILA KITU KITAKUWA SAWA[emoji120]
 
kula hot chair every day na kisha weka mfupa chini ya mtoo

hakikisha huwazi mapenzi/jinsia ya kike...kuwa bize kupangilia shughuli zako, fanya mazoezi mepesi na mazitoo kila uchaooo
 
Mimi sio mtu wa mawazo ya ngono mkuu wangu. Ila nimekuelewa
Mungu wetu ni Mungu wa hajabu
Mfalme Selemani anasema “ usiyachochee mapenzi, yaacha mapenzi yaamuwe yenyewe “....
 
Mkuu wangu, kutumia iko kitu kila siku ww utakuwa mtu wa uchumi wa juu kbs kwa dsm hii kg1 12,000/=, sio uwezo wng
kula hot chair every day na kisha weka mfupa chini ya mtoo

hakikisha huwazi mapenzi/jinsia ya kike...kuwa bize kupangilia shughuli zako, fanya mazoezi mepesi na mazitoo kila uchaooo
 
Back
Top Bottom