Dah pole sana mkuu!
Kwa uzoefu wangu majini mahaba yapo na yanatusumbua sana hasa sisi wanaume na hata wanawake pia, katika kila binaadamu kumi jawakosi watano wanasumbuliwa na hiyo kiumbe japo wengi wetu hatujui sababu za matatizo zinazotuandama, jini mahaba hatoki ki urahisi kama mapepo wengine, ni mbishi kuliko ubishi wenyewe, hutoka na kurudi na akirufi lazma akushikishe adabu maana wewe unakiwa kama hekalu lake, naomba nikuulize maswali mawili matatu
1: kipinfi uko mdogo ( ama wakati wa balehe ) ulikuwa ukipenda kuwinda? Kuogelea kwenye mito mabwawa ama baharini? Kucheza pembeni ya majalala pia.
2: huwa unajisikia usingizi baada ya kuamka asubuhi? Mfano umeamka saa 12 asubuhi, ikifika saa 3 unajisikia hali flani ya usingizi?
3: unakuwa ukipanga kufanya jambo flani la kimaendeleo lakini hulit3kelezi? Unadharau ile sauti ya ndani mwako?
4: majini mahaba ka amekaa ndani ya mwili wako kwa mida mrefu hiwa wanajidhihirisha, wanajionyesha, ushawahi kuhisi ama kuona? Maswali haya machache yatakuongoza kujua kama una jini mahaba ama una kiumbe kingine, duniani kuna viumbe vingi sana, sisi huita majini lakini kuna viumbe zaidi ya majini kama utaamia kufuatilia mamno kwa undani zaidi.
Hapa chini nakupa kisa cha jini mmoja alikuwa akinisumbia sana, nahisi bado tunasumbuana lakini kwa sasa ni yeye ndiye anapata taabu kirudi kwenye jumba ambalo yeye alinifanya mm ni makazi yake..mwisho siku amefeli yeye..sitoeleza yoote kutokana na nafadi niliyonayo hapa nitakuoelekeza jinsi huyo mpuuzi alivyokuwa akijifhihirisha kwangu.. ushuhuda ntaweka mmoja tu ama miwili.
Mara ya kwanza ilikuwa morogoro, ilipokuwa stand ya daladala ya zamani, kule town kwa wenyeji watakuwa wanapaelewa.
Siku hiyo nilikuwa naelekea mazimbu ndani, hivyo nikaenda pale kupanda daladala la mazimbu kupitia tumbaku( modeco ) nilikuta lile daladala linakaribia kujaza kasoro seat mbili tu, diti ya kwanza iliyopo mlangoni, yaan ukikaa pale unakuwa jirani na makalio ya konda, na ya pile ni ile seat ya bench, ile unaangalia nyuma, seat hizi zilikuwa zikitazamana, yaani mkikaa lazma mppishanishe miguu nadhani hapo tumeelewana.
Baada ya mimi kukalia ile seat ya benchi nikiwa naangaliana na abiria wenzangu, ilibaki seat moja ambayo atakayekuja kukaa lazma tupishanishe miguu, basi kwa mbaali nikaanza sikia harufu nzuuti ya marashi kama yale wayatumiayo wanawake wa kiarabu, kisha nikamuona mwanamke mmoja mzuri sana, nakiri ni mzuri haswaa, mweupe kama muarabu lakini alikuwa amevaa blauz ya pink na mauwa mauwa na amevaa kimini kimoja cha haja, mapaja yake manene yakawa yakionekana kunivutia ,akaja akakaa katika ile seat, tukapishanisha miguu, akanisalimia ( Asallam aleykum, nikaitikia, sasa lile joto la mappaja yake likawa linapenya mpaka ndani ya [emoji158] yangu, ila kuna fasta nikaanza hisi kichwa kikiniuma kwa mbaali, kwa uzoefu wangu moja kwa moja nikahisi huyu si kiumbe wa kawaida, na nilikuwa sahihi sababu wakati namkazia macho, kuna vitu nilikuwa naona ktk mboni zake, kwanza mboni zake ni za kijivu alaf kwa mbaali kama **** wekundu na ukijani, pia lililonodtua zaidi ni pale alipokuja jamaa( abiria mwingine akaja akakaa kwenye ile seat aliyokaa yule mwanamke, yaani amekaa kama amekalia seat tupu wakati ile seat kuna mwanamke kakaa, basi akamkalia, dijui niseme akakaa kwenue ile seat na safari ikaanza, jamaa ka relax kabisa hana noma, huye mwanamke nae namuona pia, yaani yule mwanamke kawa kama seat, kamvaa sijui hata sielewi, basi baada ya gari kutoka, pale mbele kuna round about, yule mwanamke nguo zake zikaanza kubadilika kutoka pink na kuwa za rangi ya blue, wakati tunafika masika zikawa za zambarau, akawa anabadilika badilika na tuko tunaangaliana na jamaa aliyemkalia hana anachojua kama kuna kiumbe pale alipokaa, tumeenda mpaka pale idara ya maji moruwasa, daladala likasimama, bila kudimamishwa, kwenye ile bums pale, konda akafungua mlango yule mwanamke akashukia pale ikabidi na mimi nishukie pale nikalipa nikaanza mfuata nyuma, akili yangu kawaida ni mbovu siku zote, nikasema huyu leo ntaujua mwisho wake, badi yeye mbele mimi nyuma, sasa tunapandisha kile kimwinuko cha kuelekea njia panda ya kushoto ambayo inaelekea msikiti wa mungu mmoja kule, yeye mbele mimi nyuma, tukakunja ile njia ya mafiga nipo nyumba anaenda kwa madaha mwenyewe na bado anabadilisha tu rangi, he likatokea zee moja ata sijui limetokea wapi bwana ananijua si akanisalimia? Kasimama kabisa, vipi kijana habari za madiku umepotea sijui maneno kibao, mi nikawa namjibu short short tu ili ajikatae, mwisho yule mwanamke nikaona kakata kona kanipotea, ikabifi na mimi nitoke nduki mpaka pale alipokata kona wallah sikumwona kanipotea, nilizunguka yale maeneo kama nusu saa lakini sikumuona, ikabidi nighail na mazimbu sikwenda tena, nikaenda msamvu, nikakata tiketi ya bus, nakumbuka ilikuwa ni Abood, nikapata seat ya kwanza kabisa ukiingia mlangoni, nikakaa hapo. Bus likaza kama baada ya dakika 40 45 hivi, wakati tunatoka pale geti kwa mbele ambapo trafki huwa wanaingia ktk bus na kuwaambia abiria wafunge mikanda naye yule mwanamke akapanda akamwingia yule trafki akatokea kwa mbele yake, akatabasamu mbele yangu alaf akasema shauri zako. Huyoo akaenda kumuingia mtu seat namba 3. Chuma hiyoo ikaanza safari, dikufika hata mikese, boonge la usingizi likanipitia, nakuja stuka tupo bwanawi, akashukia hapo na akaniaga kwa jina..
Hayo madubwana yapo ila ukitaka kuyatoa kwanza hakuna anayeweza kuyatoa zaidi ya wewe mwenyewe, unaweza pia kuonana nae ukimwita na mkaongea ikiwemo kumfukiza kama unajua namna gani ya kumtoa, lakini kulitoa jini amabalo liko na wewe kwa zaidi ya miaka 20 huko si kazi ndogo ila inawezekana kwa imani yako na kwa nguvu tulizonazo ndani ya miili yetu.