Nateswa sana na jini mahaba

Pole sana ndugu kwa huo mkasa unaokutesa. Hapa kitu ulichokosea kabisa ni kwenda kwa waganga. Amini huyo jini hatakuacha, na hutakuja kufanikiwa kumkimbia hata kwa kujiua.

Kikubwa; Fanya maombi sana, tubu zambi zako na ufunge ukifanya maombi. Watu tunapitia mengi. Pia huwa nasumbuliwa sana na ndoto za hovyo lakini sijawahi enda kwa mganga. Zaidi huwa napambana kukemea hadi nakuwa sawa.

Ipo siku ntasimulia mwanzo mwisho wa hizi ndoto nazoota mara kwa mara.
 
Ni kweli magonjwa ya akili yapo ila pia na haya yanayoelezwa humu pia yapo, sehemu zenye hizi imani na hayo mambo ndio yapo.
 
Unaweza ukawa sahihi kwa mtazamo wa maeneo ambayo hakuna sana imani za kishirikina na hivyo watu hawajishughulishi sana na ushirikina hivyo huwezi kusikia visa kama vya chuma ulete, issue kama ya kurogwa tatizo huwezi kutofautisha kurogwa na tatizo la kawaida kwa kuangalia kwa macho tu kwa sababu huo uchawi unaweza kuwa ni chanzo cha tatizo ambalo ni tatizo la kawaida ambalo laweza kusababishwa na sababu zengine za kawaida.
 
Kuna uwezekano mkubwa sana hauko "possessed" na "evil spirits" tafuta msaada wa kisaikolojia huku ukimwomba Mungu, vijana wengi wanapata shida za kiakili na kisaikolojia (mf. Personality disorders, depression, stress, schizoid behavior nknk) sasa kwa vile jamii yetu haina uelewa Wa mambo haya, watu wanakimbilia kuaminishana uchawi, majini, mapepo, kulogwa n.k. ukipata mtaalamu mzuri wa magonjwa ya akili au ya kisaikolojia, utashangaa na utarudi kutushukuru.
 
Ndio nadhan ni wa asili yetu aliwah mpata marehem babu yng...kukutana nae nawezaje na nifanyaje nimkatae assinisumbue kbsa
 
Nielekeze namna hiyo
 
Wapo wanaowah kuitambua hali na wapo wanaochelewa kuitambua hali
Unajua hii mada imekuja hapa si kwa bahati mbaya, tena ukute kuna wahanga wengi sna ila hawajui watapata suluhisho wapi, hebu km una majibu tupeni tupate kupona, hii ni vita tutumie silaha zoteee.
 
Amen Amen
 
Amen Amen
 
Amen Ame
 
Matatizo yeyeto ya mtu utatuliwa na mtu mwenyewe.Kwenda kwa mganga au mchungaji ni maamuzi ya pili.
Wewe umeriruhusu jini lifanye makao mwilini mwako na wewe ndiwe mwenye uwezo wa kulitoa kupitia imani.
 
Mkuu polle kwa maswaibu hayo..ni kweli majini mahaba ukishaingia agano nao..ni wagumu kutoka. Kumbuka kama kuna siku uliwahi ota unafunga ndoa ...kama ishakutokea..basi jua huyo atakusumbua milele hadi uvunje agano nao. Binafsi lilinisumbua sana hadi nilipokabidhi maisha yangu kwa Yesu ndipo nikaweza vunja maagano nae. Na kuvunja agano sio kazi..ni kuweka maisha yako kwa Kristo Yesu..kwa kukiri kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako. Hatua itayofuata ni kuvunja maagano yote uliyoweka na huyo jini, waganga wa kienyeji..maana nao hawana tiba ya kweli..ni kuuingiza zaidi kwenye vifungo vya shetani. Ukivunja kwa jina la Yesu na kwa damu ya yesu shatani hana ujanja. Ila inabidi uwe unamaninisha sana..ukiweza funga siku 7 ukiomba kila siku. Mungu ni mwaminifu sana.

Na kwa kuwa mwenza wako kakubari kusimama na wewe, shikamana nae..mfanye maombi na mungu atakufungua. Au tafuta wachungaji wa kweli..maana sikuhizi waganga ndio wachungaji wengi mjini..usipokuwa makini..utazinguliwa tu..ukate tamaa.
 
Asante, ni kwel nilishawah ota kuhusu ndoa ila nishaanza maombi naamini nitapona kwa jina la yes, ilikuchukua mda gan mpka kupona kwako mtumishi kabisa
 
Unachosema nakubaliana na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…