Kuna siku nilienda ofisi fulani nilikuwa na shida na marketing manager katika hiyo ofisi kubwa tu.
Baada ya kumweleza secretary kwa ufupi akaenda kuniitia bwana.
Yule jamaa alikuwa mzungu inaonesha anatokea london mjini kabisa kwa akina blair, kingereza chake kilikuwa hakieleweki yaani anacharaza kama cherehani, labda akiongea ufanye kuandika kwanza. Yaani ilikuwa aibu pale.
Ili kujinasua, nikatema yai broken mfulululizo bila kumpa nafasi ya kuongea halafu nikasema thank you, nikamwambia secretary utamwelekeza vizuri kama nilivyokwambia eeh!
Ndio maana hiyo lugha siipendagi kabisa.