NBC imeharibika kabisa, kwanza huduma zao mbovu halafu pia nadhani huenda ni kampeni za Mabank ya Nje hapa nchi yanayochipuka kila siku ili kuua bank kubwa kama NBC,Kwanza walicho fanya ilinunuliwa na Makaburu halafu Bank iliyo nunua ikauzwa kwa standard Bank,sasa standard Bank itaanza kukua kwa kasi huku NBC ikiendelea kufa kwa kuwa na uongozi Mbovu wa akina Mafuru ambao wanawanyima wafanyakazi wa chini bonus huku walio juu wanagawana Bonus peke yao,wengine viduchu na Mafuru alishasema anafurahi sana Mtu akiacha kazi wala hajali ndiyo maana yake kwakuwa eti watu wengi wanataka kazi, hivyo basi wafanyakazi wanakata tamaa kabisa na ndiyo maana kuna ubabaishaji wa hali ya juu NBC sijawahi kuona.
Haya yote yametokana na viongozi wetu kuuza Bank hii kwa Bei chee kwa kisingizio cha uwekezaji kumbe ni Unyonyaji wa na wizi wa mali ya umma sasa imebakia wanaua Bank na Bank a Nje zinakuwa siku Watanzania watakapo amka kwenye usingizi wa pono na kudai NBC yao itakuwa imekuisha kujifia na haina tena Mvuto kwa wateje na ndiyo itakuwa imetoka hiyo,Serikali imekuwa mara nyingi inaishia kukumbatia wawekezaji Matapeli wanao tumaliza Ndiyo maana tunataka katiba Mpya ya wananchi sio ya viongozi ili tudhibiti maozo kama haya yanayotia kinyaa jamani.
Mimi sio mtu wa mambo ya finance lakini mtu hawezi kunishawishi faida ya kuuza NBC BANK zaidi naona ni ujanja tu wa Bank za Nje ambao walikuwa contenders wa NBC ili waiue halafu wao wachukue soko,tukiamka hatuta dai Standard tutadai NBC ambayo itakuwa imekufa kibao kimeguzwa Bank za nje zinatamba.
Hata SPM Mgororo tulifanyiwa hivyohivyo walinunua kiwanda kikubwa amabcho kilikuwa competator wao wamekiua sasa aaa karatasi wanauza tu sisi tumefanywa wajinga ktk Nchi, hata Bora kiwanda kiko wapi? nilisikia limekuwa Godown aaaa wawekezaji wanaleta viatu huku wakulima wao wakiuza Ngozi zao na sisi kiwanda cha ngozi kinadidimia.jamani tuamke tukatae haya mambo ya mikataba ya akina karl peter.