NATO hatakiwi kishinda vita hii maana hana nia nzuri na dunia hii

NATO hatakiwi kishinda vita hii maana hana nia nzuri na dunia hii

Natumai hamjambo wana JF wenzagu,

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiuchukulia mzozo/vita ya Ukrein kwa mitazamo tofauti tofauti na hata baadhi yao kumtupia lawama Putin kwa kuanzisha balaa hilo,ila ukweli ni kuwa si Putin wala Urusi kuwa ndio mwanzilishi katika mgogoro huo na vita kwa ujumla katika Ukrein.

Mataifa haya yamekuwa na historia ndefu kidogo katika mahusiano yao kiuchumi ,kijamii na kidiplomasia
Kiukweli mvutano wa mataifa haya umekuwa ukichangiwa sana na sera chochezi kutoka mataifa ya magharibi hasa Marekani na washirika wake.

Malengo ya mataifa haya ya magharibi ni kutaka kuiweka dunia kwapani na ndo kitu pekee nchi kama Urusi ni mhasimu mkuu wa umoja wa NATO

Kwa nini Urusi ilichukua maamuzi magumu ya kuingia kijeshi nchini Ukrein? Je kama isingeingia kijeshi amani ingekuwepo baina ya Urusi ,Ukrein na bwana zake NATO,

Hiyo ni hapana,vita hivi hata kama visingetokea katika miaka hii vingetokea tu siku zijazo. Kwa nini ilimlazimu Putin kupeleka vikosi Ukrein,we jiulize una ugomvi na mtu harafu jirani yako wa karibu kabisa na wewe anamuarika adui yako kwake.

Na huyo adui yako anaweka kambi kwa jirani yako, wanapika ,wanakula na kunywa,na wanaweka makubaliano kuwa na umoja wao wa kusaidizana kwa lolote baya ama jema. Ina maana tayari adui yako yupo mpakani mwako kupitia jirani yako. Na jirani yako una mwambia aachane na huyo rafike yake mana hana lengo zuri na nyumba wala familia yako.

Jirani yako anakujibu kuwa usimpangia kwani yupo huru kufanya urafiki na mtu yoyote hata kama ni mtu hatarishi kwako,na wala usimpangie cha kufanya .

Wewe ungefanyaje hapo, kama adui yako alikuwa mbali na mlikuwa hamuelewani tangu awali sasa leo yupo karibu na kwako, kuna usalama hapo? Na huyo adui unamjua wazi tabia zake za kuponda mawe juu ya paa za nyumba za watu wengine kwa masirahi yake binafsi,yani kwa choko choko hajambo, na ni mbabe hasa na kuna wengine alisha watandika ngumi za uso pindi tu walipo pishana nae kauli kidogo

Kusema umemtukania kiungo chake cha ndani ya mwili kisha kuja kukuponda hapo hapo kwako ni kawaida kabisa,uwe umetukana au hujatukana utajua mwenyewe,yeye akisema fulani kanitusi basi inatosha
Na wala huwa hahitaji ushauri kutoka kwa mtu yoyote katika kutimiza adhima yake. Maana ana kikundi chake kilicho tayari ki shali popote pale akitaka msaada anapata ,naye ndo mwenye sauti hapo.

Sasa leo yupo karibu na wewe. Kama wewe ungefanyaje, na mwelekeo wa lengo la adui yako unajua kuwa sio wa kheri. Ndicho alicho fanya Mrusi kwa Ukrein.

Nchi za magharibi kama una tumia akiri vizuri sio za kuzipigia promo hata kidogo,ni watu walio jaa ubinafsi wa kutosha,huwa wanaona wengine kama wapo kwa bahati mbaya duniani.

Wapo tayari kufanya lolote kwako pindi tu ukienda kinyume na matakwa yao.Wamejawa na tamaa na ni wachoyo kupita kiasi, chochote atakacho kupa jua tu utakilipia hata kama sio leo. Mambo yao siku zote ni meme ila ya wenzao ni mabaya kila kuchwao.

NATO eti ni kikundi cha kujihami, wanajihami na yupi wakati wao ndo waanzisha shari kila kuchwao.

Tuombe Mungu sana vita hii mrusi ashinde,kinyume na hapo dunia itakuwa imeangukia kwenye shimo ambalo kamwe haitakuja kuokolewa na yeyote tena.
Umeandika meeengi ila nakuuliza maswali machache tu, la kwanza inamaana hapo unapoishi ukigombana na adui Yako basi wote waishio karibu na ww wanatakiwa pia waingie kwenye ugomvi?

Swali lingine, Urusi ana majirani wangapi na je wote ni maadui wa NATO?

Swali la tatu, Toka Urusi aingie kijeshi Ukraine ni majirani wangapi wa Urusi wamejiunga NATO? Na je Urusi ameingiza majeshi kwenye hizo nchi?
 
Ukitaka ujue kuwa watanzania uwezo wao wa kufikiria ni mdogo weka Uzi kama huu
 
Mbona Ukraine imeshashindwa. Nchi nyingi zilizokuwa zinamsaidia Ukraine kwa shinikizo la marekani zimeshakula kona. Imebaki marekani pekeyake na marekani anaamini eti urusi imeishiwa silaha kwahiyo akikomaa kidogo tu urusi itachemsha[emoji23][emoji23][emoji23]
Urusi mbona kaishiwa silaha sasahivi anaomba silaha korea kaskazini

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo lazima wakubwa wakupangie ili mambo yao yaende.mbona Marekani ndo bingwa wa kuwapangia Watu.Tumieni akili kufikiri.
Mbona Urusi imeshindwa kuipangia Finland iliyojiunga NATO??
 
Mda utazungumza ,mambo ni mengi mda ni mchache
 
mkund wako

KWANINI UTUKANE?

ULITAKIWA UMSHINDE KWA HOJA SIO KWA MATUSI.

WAKUWAHISHE DODOMA UKALE ZABIBU PAMOJA NA KUPUNGA UPEPO PALE KARIBU NA GEREZA LA ISANGA.

HII ITAKUSAIDIA KUWA MZURI WA KUJENGA HOJA HUKO MBELENI.
soma alichoandika na alivyojibiw , hajatukanwa mtu
 
Shoga yoyote hawezi kukaa na mwanaume wakaongea kiume wakamaliza tofauti zao,Ukrein haina raisi bali inakivuli cha NATO kinachoongoza nchi ya Ukrein
nazan Zele ni bora kuliko Putin , Putin anajificha na hajavamiwa Urusi
 
Kutarajia nchi huru ijilegeze na kujiachia itekwe na kukaliwa na mvamizi ni wazo lisilo na mantiki kabisa. Sio kwa nchi makini.

Ni ajabu sana kuwa kuna watu wana hamu kubwa ya kuona Ukraine ikiacha Urusi iichukue kirahisi rahisi tu eti ili kuwakomoa NATO! You’ve no clue what you’re wishing for! Sijui huu ujinga wa kutegemea ukombozi wa dunia toka Russia unatoka wapi?
unategemea nin kwa nchi inayosaini mikataba ya hovyo
 
Ndiyo lazima wakubwa wakupangie ili mambo yao yaende.mbona Marekani ndo bingwa wa kuwapangia Watu.Tumieni akili kufikiri.
una akil za kishoga , ukiambiwa binuka tukusugue utakubal tu ?
 
Mbona Ukraine imeshashindwa. Nchi nyingi zilizokuwa zinamsaidia Ukraine kwa shinikizo la marekani zimeshakula kona. Imebaki marekani pekeyake na marekani anaamini eti urusi imeishiwa silaha kwahiyo akikomaa kidogo tu urusi itachemsha[emoji23][emoji23][emoji23]
kwamb wewe na Marekan nan ana data za uongo? ebu endeleeni kupikia kuni na gesi ipo mtwara
 
Uzi wako umejaa ushabiki na unafiki kwa urusi kwa akili ya kawaida ukiangalia bila mihemko urusi hana sababu za msingi kuivamia Ukraine sababu zake huwa zinabadilika alianza kusema anawaondoa wanazi maomboleo je Zelesky anawezaje kuwa mnazi ili hali ndugu zake wayahudi waliuawa na Hitler, akaja na kisingizio kingine kuna mauaji ya halaiki mashariki mwa Ukraine anaenda kuwatetea ili hali ushahidi wa hayo mauaji ya kimbari,alisema tena eti kuna maabara ya silaha za kibaologia na ushahidi hakuna kiukweli urusi ndio aliyeanzisha vita vya kichokozi ili kuiteka Ukraine na kuchukua mali za Ukraine.

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app

Sababu kuu ya urusi kuivamia ukraine ni moja tu kurudisha USSR... putin ni kizazi cha USSR tena mhafidhina haswa wakat inasambaratika putin aliluwa comrade hasa wa USSR na kilimuuma sana aliamini kuwa viongoz wake walizembea kuruhusu mgawanyiko .. aliamin ilitakiwa Nchi iongozwe na Iron fist maaana utawala wowote wa kicomunist unaamin katika iron first ruling

So putin anataka kurudisha USSR akimaliza na ukraine atahamia nchi zingine ambazo zilikuwa ni USSR na hata irudisha kw mfumo wa kizaman anataka afanye kama belarus anaweka kiongoz puppet maana yake kremlin ndo itakuwa inaamua nini kifanyike ukraine.. kama ilivyo belarus

Hizo sababu zingine ni geresha
Tu maana anajua ukraine wakijoin Nato basi wengine watafata na ndoto yake haitatimia..
 
Back
Top Bottom