Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg hivi karibuni alifanya ziara nchini Marekani, lengo likiwa ni kujadili mwendelezo wa kuiunga mkono Ukraine na kuhakikisha mwendelezo wa upatikanaji wa silaha kwa Ukraine, wakati vita kati ya nchi hiyo na Russia ikiendelea. Hii inajumuisha kuridhiwa kwa msaada wa ziada wa dola za kimarekani bilioni 60 na bajeti ya miaka minne ya dola za Marekani bilioni 54.5 kuiunga mkono Ukraine.
Wakati wa mahojiano ama hotuba alipokuwa nchini Marekani, Bw. Stoltenberg alirejea mara kwa mara kuitaja China, kiuhalisia akiitaja kama ‘changamoto’ kwa NATO. Inaonekana kama kiongozi wa shirikisho kubwa la kijeshi duniani hausishi mgogoro wa Russia na Ukraine kwa Ulaya pekee, bali anauona kama kiashiria cha mgogoro mpana wa siasa za kijiografia duniani.
Matokeo yake, anatafuta uhalali wa upanuzi wa NATO duniani. Haja kuu ya ndani ya NATO ni kupanuka Zaidi, huku vita ikiwa ni haja yake ya nje. Bila ya vita, shirikisho hili la kijeshi litapoteza sababu ya uwepo wake, hivyo ni lazima liwe na sababu ya wazi, na kama hakuna, basi linalazimika kutengeneza sababu.
Baada ya kuvunjwa kwa Mkataba wa Warsaw kufuatia kumalizika kwa Vita ya Baridi, NATO imekuwa ikitafiti mwelekeo wake wa baadaye. Desemba, 1998, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Madeline Albright aliweka wazi mtazamo wa Marekani kuhusu marekebisho ya kimkakati ya NATO katika mkutano mmoja. Bi. Albright aliamini kuwa, kanuni ya ‘ulinzi wa pamoja’ inapaswa kupewa ufafanuzi mpya kama ‘kulinda maslahi ya wenzi,’ ili kuiwezesha NATO kujibu kwa haraka migogoro iliyo nje ya eneo lake la ulinzi.
Kwa kuwa Russia imeendelea kupinga upanuzi wa NATO kuelekea mashariki, sababu kwa sasa imeelekezwa moja kwa moja kwa Russia, na kuibuka kwa vita kati ya Russia na Ukraine kumeimarisha mshikamano wa NATO, japo kwa kuwafanya viongozi wa nchi wanachama wake kuamini kuwa, shirikisho hilo linapaswa kuboresha na kupanua eneo lake, huku Asia ikiwa kituo kinachofuata.
Wakati wa ziara yake nchini Marekani, mara kwa mara Bw. Stoltenberg aliihusisha China na mgogoro wa Russia na Ukraine. Katika hotuba aliyoitoa Heritage Foundation, Stoltenberg alisisitiza kuwa ushindi wa Russia utazifanya nchi nyingine kama Korea Kaskazini, Iran na China kutumia nguvu.
Zaidi ya hapo, alipohojiwa na Shirika la Habari la Fox, Stoltenberg alimpongeza sana aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump kwa kurekebisha mkakati kuhusu China mwaka 2017, na kuiwezesha NATO kuwasaidia wenza wak wa Ulaya kukabiliana na kile alichokiita ‘changamoto zinazoletwa na China.’
Mkakati wa marekebisho wa NATO unaweza kuboresha masikilizano yake ya ndani kwa muda mfupi na kuendelea kudumisha nafasi yake kama nguvu kubwa ya kijeshi duniani inayoongoza na Marekani na nchi za Magharibi. Hata hivyo, hatua hii katika kipindi kirefu itasababisha mtengano na mvutano duniani, na hivyo kuathiri sana uhusiano wa kimataifa na mazingira ya usalama kwa China. Mara NATO itakapoanza kuingia Asia, sio tu kwamba itachochea mivutano ya siasa za kijiografia duniani, bali pia inaweza kuongeza kasi yam bio za silaha na vurugu za kikanda.
Hatari ya vita haitakwepeka kuongezeka wakati NATO ikijiendeleza na kujiimarisha duniani, na wale watakaoathirika hatatoka bara la Asia peke, bali dunia nzima!