NATO na EU wapo katika tope ambalo huenda wakahitaji watolewe na walio nje ya taasisi hizo

SaintErick

Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
90
Reaction score
53
Muungano wa kijeshi wa NATO pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa zaidi tangu kumalizika kwa mzozo wa vita baridi miaka ya 1990s.

NATO ilijisahau na kua na utegemezi wa Marekani kwa asllimia kubwa. Lakini katika kipindi cha Urais wa Donald Trump (2016-2020), NATO ilijikutq inaingia katika mzozo wa kibajeti na Marekani. Kwa sasa NATO inahofia kama Trump atashinda ni nini ataamua? Nchi nyingi za Ulaya kama Finland zinajaribu kwanza kujiimarisha zenyewe.

Mgogoro wa Ukraine kwa sasa ni kipimo cha uthabiti wa NATO lakini ingawa Ukraine sio Mwanachama wa NATO ilikua ni muhimu kuisaidia. Lakini mpka sasa ni kwamba ni kama NATO imetegwa. Hitaji la Ukraine ni kutumia Silaha za NATO na au kutoka washirika wa Umoja wa Ulaya lakini nchi zote hazina mtazamo sawa. Kuna baadhi zinaruhusu kama Finland na nyingine zinakataa kama Ujerumani. Na kuna tofauti kati ya nchi waanzilishi wa NATO na hawa waliojiunga karibuni. Nchi za mwanzo hasa kipindi cha kati ya 1970s-1990s zinatazama katika namna tofauti sana kwa kuhesabu hatua zilizobakia Ulaya kutumikia katika vita kamili na URUSI ambayo Warusi walikua wakijiandaa nago kwa muda sasa ila Ulaya bado ndio wameanza kujiandaa haswa kati ya 2022/23.

Tatizo la NATO ilikuwa ni kujitanua kusiko kua na nidhamu kinyume kitu ambacho marais werevu kama George HW Bush na Bill Clinton walijaribu kuzuia wakati huo na ukikukwaji miongozo na makubaliano ya mwanzo na labda kwa sababu waliidhafau Urusi hasa ya Boris Yelestin na Vladmir Putin.

Wakati NATO kwa sasa ikiwa matatani pamoja tatizo hilo liko Umoja wa Ulaya. Nchi nyingi sasa zina mitazamo tofauti ndani ya Umoja huo wenye nguvu zaidi duniani. Kwa sasa Hungary ambeye anashikilia kijiti cha Uenyekiti wa Umoja wa Ulaya anasimama badharani kuukosoa umoja huo. Utakumbuka miaka kadhaa hapa tumekua na Bri-Exit. Umoja wa Ulaya hauko kama ulivyokua.

Changamoto kubwa sasa kwa Umoja huo inatoka katika bara la ASIA hasa ukuaji wa China na pia muungano wa BRICS+. Hivi karibuni walikua wanataka kuongeza kodi kwenye bidhaa za magari ya umeme kutoka china kwa hadi 100% kuna nchi ziliunga mkono hoja, kuna nchi zilipinga na kuna nchi zilijizuia kupiga kura. Kwa mpasuko huu nani atawaokoa?

Lakini Urusi pia imekua na changamoto kubwa kwa Umoja huo lakini kuna namna wamekubaliana kuishi naye. Wasichoweza kukiri ni kwamba walikosea sana kutoendana na Urusi katika njia ya mazungumzo wakiamini katika kuisaidia Ukraine kupigana vita ya Umoja wa Ulaya na Urusi. Ukraine ametumikia kama "Proxy" tu. Kwa sasa tayari EU inaona vita hii ni ya muda mrefu na kwa yanayoendelea, huenda kwa vyovyote vita itavyoisha URUSI atakua na advantage.

Lakini uhalisia wa kwambakwa vyovyote vile Urusi atanufaika na vita hii ni ngumu kwa EU kukubali lakini wanahitaji kuzinduka na kuona tayari wanafikia ukikongoni katika kutoa msaada ambao Ukraine inautaka. Wataendelea kutoa msaada ambao bado sio suluhisho la mwisho kwa Ukraine.

Nguvu ya China na India zinaweza kusaidia EU na NATO kufichama na au Donald Trump anaweza wasaidia. Akichaguliwa, vita vya Ukraine vitaisha ndani ya muda mfupi sana.
 
China anazikopesha nchi za ulaya, uingereza ikiwemo,unasemaje ni ghost economy!?..uchumi wa china ni really,tazama marekani anavyohaha kuweka vikwazo bidhaa za china
Kukopeshana siyo ishu hata Ulaya inakopesha china mkuu
 
Yaani India iisaidie NATO? Uchumi wa china na India ni ghost economy Mzee.
Swali kwako? Unavuta bangi?
Not Bad. Sababu ikiwa haujaelewa badala ya ku jump kwene conclusion ungeomba clarification. Hio ni njia nzuri ya kujenga hoja. Wanaweza kumaliza matatizo ya NATO na EU sio kwa kuwapa pesa unapaswa kuelewa kwamba NATO na au EU wana uchumi mzuri kuliko China na India. Ila India na China zina nafasi kubwa ya kua Mediators katika mzozo wa Ukraine kwa sababu hasa India ina maintain mahusiano na nchi zote mbili. Kwa hio kama actors wakubwa pale wanaweza kusaidia juhudi za Usuluhishi na baada ya mzozo NATO na EU zitakua zimeondoka katika tatizo walilokuepo.
Swali uliniuliza nikuulize au basi umeelewa.?
 
Babaako aliuza ng'ombe ili apate fedha ya kukupeleka ng'ombe wewe shule
Mchina ana usongo na hela yaani wachina wanauza mpaka makande na togwa Africa na hela wanatuma kwao.Us wao uchumi wao ulikuwa very selective yaani kuna baadhi ya sector ilizipuuzia,sasa kilichotokea Mchina akaanza kwenye uchumi mdogo mdogo akaja wa kati then akampandia kwa juu kwenye upande wa technology.Ukweli mchungu CHINA 🇨🇳 kwasasa anampumulia US kisogoni,njia pekee ya US kuchomoka ni kuanzisha vita sasa wandewa kwavile walijipanga WANAMKABIA KWA JUU mpaka kwenye upande wa vita 😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Not Bad. Sababu ikiwa haujaelewa badala ya ku jump kwene conclusion ungeomba clarification. Hio ni njia nzuri ya kujenga hoja. Wanaweza kumaliza matatizo ya NATO na EU sio kwa kuwapa pesa unapaswa kuelewa kwamba NATO na au EU wana uchumi mzuri kuliko China na India. Ila India na China zina nafasi kubwa ya kua Mediators katika mzozo wa Ukraine kwa sababu hasa India ina maintain mahusiano na nchi zote mbili. Kwa hio kama actors wakubwa pale wanaweza kusaidia juhudi za Usuluhishi na baada ya mzozo NATO na EU zitakua zimeondoka katika tatizo walilokuepo.
Swali uliniuliza nikuulize au basi umeelewa.?
Aliyekwambia ukraine/nato wanahitaji mediator kwenye mgogoro wao na russia ni nani,

Russia anatepeteshwa mdogomdogo mpaka alegee, huo mfupa kapewa ahangaike nao kwanza
 
Yaani India iisaidie NATO? Uchumi wa china na India ni ghost economy Mzee.
Swali kwako? Unavuta bangi?
Uchumi wa marekani ndiyo ghost wanategemea fadhila ya dunia kutumia dollar hivyo wao ni kuprint pesa tu na kukuza uchumi wao ...wenye akili tunasema kama dollar ikifutwa leo hii kuwa pesa ya dunia basi.leo hii hii uchumi wa marekani utakuwa chini ya india
 
Muungano wa kijeshi wa NATO pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa zaidi tangu kumalizika kwa mzozo wa vita baridi miaka ya 1990s.

NATO ilijisahau na kua na utegemezi wa Marekani kwa asllimia kubwa. Lakini katika kipindi cha Urais wa Donald Trump (2016-2020), NATO ilijikutq inaingia katika mzozo wa kibajeti na Marekani. Kwa sasa NATO inahofia kama Trump atashinda ni nini ataamua? Nchi nyingi za Ulaya kama Finland zinajaribu kwanza kujiimarisha zenyewe.

Mgogoro wa Ukraine kwa sasa ni kipimo cha uthabiti wa NATO lakini ingawa Ukraine sio Mwanachama wa NATO ilikua ni muhimu kuisaidia. Lakini mpka sasa ni kwamba ni kama NATO imetegwa. Hitaji la Ukraine ni kutumia Silaha za NATO na au kutoka washirika wa Umoja wa Ulaya lakini nchi zote hazina mtazamo sawa. Kuna baadhi zinaruhusu kama Finland na nyingine zinakataa kama Ujerumani. Na kuna tofauti kati ya nchi waanzilishi wa NATO na hawa waliojiunga karibuni. Nchi za mwanzo hasa kipindi cha kati ya 1970s-1990s zinatazama katika namna tofauti sana kwa kuhesabu hatua zilizobakia Ulaya kutumikia katika vita kamili na URUSI ambayo Warusi walikua wakijiandaa nago kwa muda sasa ila Ulaya bado ndio wameanza kujiandaa haswa kati ya 2022/23.

Tatizo la NATO ilikuwa ni kujitanua kusiko kua na nidhamu kinyume kitu ambacho marais werevu kama George HW Bush na Bill Clinton walijaribu kuzuia wakati huo na ukikukwaji miongozo na makubaliano ya mwanzo na labda kwa sababu waliidhafau Urusi hasa ya Boris Yelestin na Vladmir Putin.

Wakati NATO kwa sasa ikiwa matatani pamoja tatizo hilo liko Umoja wa Ulaya. Nchi nyingi sasa zina mitazamo tofauti ndani ya Umoja huo wenye nguvu zaidi duniani. Kwa sasa Hungary ambeye anashikilia kijiti cha Uenyekiti wa Umoja wa Ulaya anasimama badharani kuukosoa umoja huo. Utakumbuka miaka kadhaa hapa tumekua na Bri-Exit. Umoja wa Ulaya hauko kama ulivyokua.

Changamoto kubwa sasa kwa Umoja huo inatoka katika bara la ASIA hasa ukuaji wa China na pia muungano wa BRICS+. Hivi karibuni walikua wanataka kuongeza kodi kwenye bidhaa za magari ya umeme kutoka china kwa hadi 100% kuna nchi ziliunga mkono hoja, kuna nchi zilipinga na kuna nchi zilijizuia kupiga kura. Kwa mpasuko huu nani atawaokoa?

Lakini Urusi pia imekua na changamoto kubwa kwa Umoja huo lakini kuna namna wamekubaliana kuishi naye. Wasichoweza kukiri ni kwamba walikosea sana kutoendana na Urusi katika njia ya mazungumzo wakiamini katika kuisaidia Ukraine kupigana vita ya Umoja wa Ulaya na Urusi. Ukraine ametumikia kama "Proxy" tu. Kwa sasa tayari EU inaona vita hii ni ya muda mrefu na kwa yanayoendelea, huenda kwa vyovyote vita itavyoisha URUSI atakua na advantage.

Lakini uhalisia wa kwambakwa vyovyote vile Urusi atanufaika na vita hii ni ngumu kwa EU kukubali lakini wanahitaji kuzinduka na kuona tayari wanafikia ukikongoni katika kutoa msaada ambao Ukraine inautaka. Wataendelea kutoa msaada ambao bado sio suluhisho la mwisho kwa Ukraine.

Nguvu ya China na India zinaweza kusaidia EU na NATO kufichama na au Donald Trump anaweza wasaidia. Akichaguliwa, vita vya Ukraine vitaisha ndani ya muda mfupi sana.
Ukisikia NATO sio US peke yake zipo nchi tele, ata huyo Trump hataachwa akihatarisha usalama wa taifa la marekani pamoja na washirika wake, kuhusu kulinda usalama wa nchi za NATO sio kwamba rais ajaye anaweza kufanya chochote atakacho, ile ni mikataba rais yoyote anayeshika anawekewa documents juu ya meza apende asipende adil nazo.

Ndio mana hata Trump akishinda urais lakini akionekana anasera kuhatarisha usalama wa US kabla hajafanya hivyo wajumbe seneta wata m-disqualify, ndio mana siku hizi kuna hoja anafuatiliwa Trump amekuwa akiwasiliana na putin mara ngap na wanaongea nini, sababu rais yoyte wa marekani atakayeshika madaraka lazima afahamu adui no.1 wa nchi za ulaya na Marekani ni Russia.
 
Aliyekwambia ukraine/nato wanahitaji mediator kwenye mgogoro wao na russia ni nani,

Russia anatepeteshwa mdogomdogo mpaka alegee, huo mfupa kapewa ahangaike nao kwanza
Sawa mimi sijaambiwa basi wewe uliyeambiwa na Blinken, Rutte au Austin, Stemer, Macron au kiongozi nwingine una kheri.
Ikiwa viongozi wa EU wanaona haja ya kua na kusitisha mapigano. Kama Marekani inaona hiyo haja lakini wewe huoni ni pia sawa. Ndio maana wanatoa silaha za kujilinda zaidi ya kushambulia. Huoni logic yao bado?
 
Yaani India iisaidie NATO? Uchumi wa china na India ni ghost economy Mzee. Wachina kwao maisha magumu wanarandaranda duniani.
Swali kwako? Unavuta bangi?
Unajielewa mkuu!?
China nchi ambayo imewavusha 75%+ ya raia wake kwenye poverty line unaita uchumi wake ni ghost economy!?
China ambayo WB na IMF wametoa ripoti ni nchi pekee duniani imekopesha mataifa sawia na WB imekopesha mataifa zaidi ya 138 na imesamehe mataifa 38 madeni unawaita uchumi wao ghost!?
Na WB ikamalizia kusema kama USA ingejaribu kufanya kama China basi ingeenda bankrupt.
Vivyo hivyo kwa nchi za Ulaya.
Embu msiropoke tu pasi na kujua uhalisia wa mambo.
 
Aliyekwambia ukraine/nato wanahitaji mediator kwenye mgogoro wao na russia ni nani,

Russia anatepeteshwa mdogomdogo mpaka alegee, huo mfupa kapewa ahangaike nao kwanza
Bahati mbaya kwa US na NATO ni kwamba Russia haiwezi kutepeta kwasababu ina sapoti kubwa kutoka China.
Kutepeta ilibidi itepete 2023 kwa vikwazo walivyowekewa na EU.
Ila hadi ikavuka 2024 wanadiplomasia wa West wengi tu walikiri kuwa Russia haiwezi ikashindwa tena kama imeweza kuvuka vikwazo vyote vile vya kiuchumi.
 
Back
Top Bottom