NATO na EU wapo katika tope ambalo huenda wakahitaji watolewe na walio nje ya taasisi hizo

NATO na EU wapo katika tope ambalo huenda wakahitaji watolewe na walio nje ya taasisi hizo

Muungano wa kijeshi wa NATO pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa zaidi tangu kumalizika kwa mzozo wa vita baridi miaka ya 1990s.

NATO ilijisahau na kua na utegemezi wa Marekani kwa asllimia kubwa. Lakini katika kipindi cha Urais wa Donald Trump (2016-2020), NATO ilijikutq inaingia katika mzozo wa kibajeti na Marekani. Kwa sasa NATO inahofia kama Trump atashinda ni nini ataamua? Nchi nyingi za Ulaya kama Finland zinajaribu kwanza kujiimarisha zenyewe.

Mgogoro wa Ukraine kwa sasa ni kipimo cha uthabiti wa NATO lakini ingawa Ukraine sio Mwanachama wa NATO ilikua ni muhimu kuisaidia. Lakini mpka sasa ni kwamba ni kama NATO imetegwa. Hitaji la Ukraine ni kutumia Silaha za NATO na au kutoka washirika wa Umoja wa Ulaya lakini nchi zote hazina mtazamo sawa. Kuna baadhi zinaruhusu kama Finland na nyingine zinakataa kama Ujerumani. Na kuna tofauti kati ya nchi waanzilishi wa NATO na hawa waliojiunga karibuni. Nchi za mwanzo hasa kipindi cha kati ya 1970s-1990s zinatazama katika namna tofauti sana kwa kuhesabu hatua zilizobakia Ulaya kutumikia katika vita kamili na URUSI ambayo Warusi walikua wakijiandaa nago kwa muda sasa ila Ulaya bado ndio wameanza kujiandaa haswa kati ya 2022/23.

Tatizo la NATO ilikuwa ni kujitanua kusiko kua na nidhamu kinyume kitu ambacho marais werevu kama George HW Bush na Bill Clinton walijaribu kuzuia wakati huo na ukikukwaji miongozo na makubaliano ya mwanzo na labda kwa sababu waliidhafau Urusi hasa ya Boris Yelestin na Vladmir Putin.

Wakati NATO kwa sasa ikiwa matatani pamoja tatizo hilo liko Umoja wa Ulaya. Nchi nyingi sasa zina mitazamo tofauti ndani ya Umoja huo wenye nguvu zaidi duniani. Kwa sasa Hungary ambeye anashikilia kijiti cha Uenyekiti wa Umoja wa Ulaya anasimama badharani kuukosoa umoja huo. Utakumbuka miaka kadhaa hapa tumekua na Bri-Exit. Umoja wa Ulaya hauko kama ulivyokua.

Changamoto kubwa sasa kwa Umoja huo inatoka katika bara la ASIA hasa ukuaji wa China na pia muungano wa BRICS+. Hivi karibuni walikua wanataka kuongeza kodi kwenye bidhaa za magari ya umeme kutoka china kwa hadi 100% kuna nchi ziliunga mkono hoja, kuna nchi zilipinga na kuna nchi zilijizuia kupiga kura. Kwa mpasuko huu nani atawaokoa?

Lakini Urusi pia imekua na changamoto kubwa kwa Umoja huo lakini kuna namna wamekubaliana kuishi naye. Wasichoweza kukiri ni kwamba walikosea sana kutoendana na Urusi katika njia ya mazungumzo wakiamini katika kuisaidia Ukraine kupigana vita ya Umoja wa Ulaya na Urusi. Ukraine ametumikia kama "Proxy" tu. Kwa sasa tayari EU inaona vita hii ni ya muda mrefu na kwa yanayoendelea, huenda kwa vyovyote vita itavyoisha URUSI atakua na advantage.

Lakini uhalisia wa kwambakwa vyovyote vile Urusi atanufaika na vita hii ni ngumu kwa EU kukubali lakini wanahitaji kuzinduka na kuona tayari wanafikia ukikongoni katika kutoa msaada ambao Ukraine inautaka. Wataendelea kutoa msaada ambao bado sio suluhisho la mwisho kwa Ukraine.

Nguvu ya China na India zinaweza kusaidia EU na NATO kufichama na au Donald Trump anaweza wasaidia. Akichaguliwa, vita vya Ukraine vitaisha ndani ya muda mfupi sana.
Duh! Uchambuzi wa Warusi wa Wabongo bwana, hadi unatamani kucheka!
 
Hoja kinzani ni jambo la busara na linaonesha ni wakomavu wa fikra na binadamu huru. Ukiona unaona na au kufikiri tofauti jua kuna mahali huenda uko sawa. Lete hoja yako. Maana hapa hakuna muegemo wa kimawazo. Na nadhan nafanyia kazi udhaifu wa Urusi kwa sasa. Kwa hio nikiandika napo nitakua Mmarekani au Muulaya mbongo?
 
Ukisikia NATO sio US peke yake zipo nchi tele, ata huyo Trump hataachwa akihatarisha usalama wa taifa la marekani pamoja na washirika wake, kuhusu kulinda usalama wa nchi za NATO sio kwamba rais ajaye anaweza kufanya chochote atakacho, ile ni mikataba rais yoyote anayeshika anawekewa documents juu ya meza apende asipende adil nazo.

Ndio mana hata Trump akishinda urais lakini akionekana anasera kuhatarisha usalama wa US kabla hajafanya hivyo wajumbe seneta wata m-disqualify, ndio mana siku hizi kuna hoja anafuatiliwa Trump amekuwa akiwasiliana na putin mara ngap na wanaongea nini, sababu rais yoyte wa marekani atakayeshika madaraka lazima afahamu adui no.1 wa nchi za ulaya na Marekani ni Russia.
Sijui kama uko well informed au la. Lakini kama ni mfutiliaji utagundua viongozi wa Ulaya wana wasiwasi juu ya Trump na hata wamelazimika kuanza kua na mipango ya ndani ya Ulaya namna gani inaweza ku deal na matatizo yake ndani ya Ulaya.

Na pia unaweza kupitia katika maazimio mbalimbali ya Senate na ripoti mbali mbali juu ya adui namba moja wa Marekani. Ni CHINA sio RUSSIA. Angalia Gallup, CNBC na hata Wikipedia (hii si shauri sana, ila inaweza kukupa pa kuanzia) hapo utaona kulingana na chanzo chako URUSI ni adui namba 3,4 au 5 kwa Marekani kwa taarifa za hadi July, 2024.
So, karibu tena ukiwa na latest updates.
 
Bahati mbaya kwa US na NATO ni kwamba Russia haiwezi kutepeta kwasababu ina sapoti kubwa kutoka China.
Kutepeta ilibidi itepete 2023 kwa vikwazo walivyowekewa na EU.
Ila hadi ikavuka 2024 wanadiplomasia wa West wengi tu walikiri kuwa Russia haiwezi ikashindwa tena kama imeweza kuvuka vikwazo vyote vile vya kiuchumi.
Warusi wanashindia mihogo ya kukaanga na maji, hali mbaya kule usiskie
 
Back
Top Bottom