NATO na EU wapo katika tope ambalo huenda wakahitaji watolewe na walio nje ya taasisi hizo

Duh! Uchambuzi wa Warusi wa Wabongo bwana, hadi unatamani kucheka!
 
Hoja kinzani ni jambo la busara na linaonesha ni wakomavu wa fikra na binadamu huru. Ukiona unaona na au kufikiri tofauti jua kuna mahali huenda uko sawa. Lete hoja yako. Maana hapa hakuna muegemo wa kimawazo. Na nadhan nafanyia kazi udhaifu wa Urusi kwa sasa. Kwa hio nikiandika napo nitakua Mmarekani au Muulaya mbongo?
 
Sijui kama uko well informed au la. Lakini kama ni mfutiliaji utagundua viongozi wa Ulaya wana wasiwasi juu ya Trump na hata wamelazimika kuanza kua na mipango ya ndani ya Ulaya namna gani inaweza ku deal na matatizo yake ndani ya Ulaya.

Na pia unaweza kupitia katika maazimio mbalimbali ya Senate na ripoti mbali mbali juu ya adui namba moja wa Marekani. Ni CHINA sio RUSSIA. Angalia Gallup, CNBC na hata Wikipedia (hii si shauri sana, ila inaweza kukupa pa kuanzia) hapo utaona kulingana na chanzo chako URUSI ni adui namba 3,4 au 5 kwa Marekani kwa taarifa za hadi July, 2024.
So, karibu tena ukiwa na latest updates.
 
Warusi wanashindia mihogo ya kukaanga na maji, hali mbaya kule usiskie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…