Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Baada ya siku chache, nchi wanachama wa Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) zilikutana huko Washington, ili kusherehekea miaka 75 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo. Kwenye mkutano huo, NATO ilitoa kauli zisizo za kweli kwamba China kuwa ni mhimizaji muhimu wa vita kati ya Russia na Ukraine. Kabla ya hapo, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Jens Stoltenberg pia alidai kwamba China inapaswa kuwajibika na vita hivyo. Wachambuzi wanaona kuwa, madhumuni ya kisiri ya NATO kufanya hivyo ni kupata kisingizio cha kuingia barani Asia.
Zikiwa jumuiya za kikanda, katika miaka ya hivi karibuni, SCO na NATO zimekuwa na mwelekeo tofauti na kufanya maamuzi tofauti kabisa katika kudumisha usalama na utulivu wa kikanda na kimataifa.
Tangu kuanzishwa kwake miaka 23 iliyopita, SCO imetoa mchango mkubwa katika kukuza amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda. Kutoka kwenye kushirikiana kupambana na “nguvu tatu za uovu” ambazo ni ugaidi, ufarakanishaji na misimamo mikali, kuzuia kwa pamoja kuenea kwa dawa za kulevya, kufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya kupambana na ugaidi, na kuanzisha mifumo ya mikutano katika ngazi zote, hadi kuhimiza utatuzi wa suala la Afghanistan, uwezo wa SCO kutatua suala la amani na usalama umeendelea kuboreka, na kuanzisha utaratibu mzuri katika kukabiliana na changamoto za kikanda. Jambo la kupongezwa zaidi ni kwamba, badala ya kutegemea hatua za kinguvu, SCO inazingatia zaidi maendeleo ya kiuchumi katika kutatua migogoro na kudumisha amani na usalama.
Kwa upande wa NATO, jumuiya hiyo iliyoanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ina historia ya miaka 75, ilikuwa ikipingana na Jumuiya ya Warsaw Pact iliyoongozwa na Umoja wa Kisovieti. Baada ya kuvunjwa kwa Umoja wa Kisovieti na kumalizika kwa vita baridi, NATO ambayo ilipaswa kutoweka kabisa, imeendelea kutumika, na kuanzisha vita mara kwa mara duniani, na kuwa tishio kubwa kwa amani ya dunia. Katika miaka kadhaa iliyopita, vita nyingi zilizotokea duniani ikiwemo katika nchi za Kosovo, Iraq, Afghanistan, Libya zimeanzishwa na jumuiya hiyo. Vita inayozidi kupamba moto kati ya Russia na Ukraine pia ni matokeo ya moja kwa moja ya NATO kupanua nguvu yake katika eneo la mashariki.