Natoa angalizo kwa wana Yanga wenzangu kuelekea fainali ya FA

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Nashauri uongozi wa Yanga, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Yanga tusije kubweteka na mpasuko uliojitokeza Simba kwa maneno ya Haji Manara yanayosambazwa mitandaoni na kuacha kujipanga ipasavyo ili kushinda mechi ya tarehe 25.

Tuwaachie wenyewe hayo mambo na tujipange kimchezo ili tubebe kombe la FA hiyo jumapili. Kuachiwa video ya namna ile huku tukielekea kwenye Derby inaweza kuwa ni namna ya kuwafanya Yanga waone wameshaumaliza mchezo mapema sana na huku wapinzani wao wakawa wanaendeleza nguvu na mikakati na mipango ya ushindi kama vile hakijatokea kitu vile.
 
Mnaendeleza utoto mpira wa Tanzania. Yaani wachezaji wa Yanga waathiriwe na bifu la Manara na Barbra? Mkifungwa fungweni tu wala hicho unachoongea hakihusoani na saikolojia ya wachezaji.
 
Mnaendeleza utoto mpira wa Tanzania. Yaani wachezaji wa Yanga waathiriwe na bifu la Manara na Barbra? Mkifungwa fungweni tu wala hicho unachoongea hakihusoani na saikolojia ya wachezaji.
wanacho fanya simba ni ku- create 'mind game' ili kuwahadaa yangaa, jumatatu ndiyo utaujua ukweli kama kweli hao 'wazungu' wawili wame itilafiana…. kuna mchezo mchafu nachezwa apooo ….Mind game !
 
Sasa maneno yanaathiri vp wachezaji wa Yanga?Uwezo mdogo wa kufikiri.Unajua Pyschology kweli ww?
Mnaendeleza utoto mpira wa Tanzania. Yaani wachezaji wa Yanga waathiriwe na bifu la Manara na Barbra? Mkifungwa fungweni tu wala hicho unachoongea hakihusoani na saikolojia ya wachezaji.
Labda haujui mind game. Mechi za Simba na Yanga huwa zinaanzia kuchezwa nje ya uwanja kabla ya kuingia uwanjani. Naposema nje ya uwanja namaanisha mambo ya hamasa, motisha, n.k hivi vyote vinafanywa kuwapa hari na morali wachezaji. Hili bifu la Manara kwa CEO wake lipo kimkakati zaidi haiingii akilini mpasuko utokee kuekea kwenye Derby. Hapa Yanga wanafubazwa tu
 
Jidanganye na endelea kujitoa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…